Barabara za Tanzania zinajengwaje, mbona kama udongo mtupu?

Barabara za Tanzania zinajengwaje, mbona kama udongo mtupu?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
DARAJA LAKATIKA, BARABARA YA DODOMA- MOROGORO YAFUNGWA - Mawasiliano ya Barabara ( 360 X 640 ).jpg


Ukiangalia kwa makini sana hii barabara ya Morogoro - Dodoma, hasa eneo ambalo daraja limeng'olewa ni lazima upigwe na bumbuwazi!

Hakuna hata mawe wala kingo za maana, ujazo wa lami uliowekwa ndio kituko kabisa , unaweza kuichimbua hata kwa jembe la mkono, Tatizo liko wapi?

Hivi ndivyo nchi za wenzetu zinavyojenga barabara au ni sisi tu?
 
Mh Rais wa Tanzania,

Waziri aliekua na dhamana ya kujenga hio barabara ya "MOROGORO - DODOMA" kipindi cha Mkwere anatakiwa afunguliwe mashtaka ya "UHUJUMU UCHUMI".

Haiwezekani akatumia hela za umma kujenga barabara kwa Udongo Mfinyanzi. Hela za wanyonge zimetumika vibaya.
 
Erythrocyte,
Tatizo unatoa maoni baada ya kuona daraja limesombwa. Kama unaweza kuchimbua kwa jembe la mkono,hayo malori mazito yangedidimia basi.

Hiyo ni Geography ya kidato cha tatu, mambo ya soil profile, udongo ukishafukiwa unabadilika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, ndio mana kwa picha hiyo unaweza kuona kama kuna pande la keki tu hapo.
 
Lumumba siku hizi mmekua na akili ya matope sana. Ni mwendo wa kupinga hata mambo ya msingi, jamaa kahoji jambo la msingi sana we unaleta ujinga ujinga. We unazani huyo Magufuli mnaemshabikia akiona picha za hilo daraja atafurahi? Shwaini kabsa.
Kamanda ulichukulia wali degree yako ya uhandidi? Ebu tuonyeshe chochote ulichojenga wewe tuone na tujiridhishe kuwa wewe ni mbobea.
Wafuasi wa kamanda msaliti hamjambo kwa porojo [emoji1547]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu inaonekana huna idea yoyote ya high way engineering, kama unayo utakuwa zero kichwani. Thickness ya Lami ikiwa kubwa kama unavyotaka wewe basi barabara zitakuwa ghali mno kujengwa. Hiyo Lami unayosema ndogo ilikuwa designed baada ya kutest udongo maabara uliochini ya Lami ndiomaana unaona malori yanapita naibonyei, acheni kuingilia fani za watu wakati ulisoma HKL
 
Back
Top Bottom