Baraka hutoka kwa Baba; Laana hutoka kwa Mama, utaamua mwenyewe

Baraka hutoka kwa Baba; Laana hutoka kwa Mama, utaamua mwenyewe

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
BARAKA HUTOKA KWA BABA, LAANA HUTOKA KWA MAMA! UTAAMUA MWENYEWE!

Anaandika, Robert Heriel,
Mwanafalsafa.

Utaamua mwenyewe, utapima na kuamua maisha yako mwenyewe.

Baba ndiye mungu wa dunia, utake usitake, Mama ni msaidizi wa Baba upende usipende. Endapo hili halitatokea maisha ya mtoto huwa mashakani. Mtoto akigombana na Baba hukosa baraka, hata hivyo Baba hawezi kumlaani mtoto, Baba yu atoa baraka tuu, hana nguvu katika laana.

Mtoto akigombana na Mama hapo huchukua Laana, mama ndiye mwenye uwezo wa kutoa laana katika huu ulimwengu ikashika pasipo kizuizi. Lakini pamoja na umuhimu wa Mama hapa duniani lakini kamwe hana uwezo wa kumbariki mtoto aliyemzaa, hana mamlaka na hata akimbariki mara elfu moja mtoto hawezi kupata baraka hata moja. Labda sieleweki. Lakini mtanielewa tuu.

Unapoishi na wazazi lazima uelewe kila mzazi anamajukumu yake, anamipaka yake, ipo nafasi ya mama ambayo kamwe baba haiwezi ku-cover, lakini pia ipo nafasi ya Baba ambayo mama hata apinduke vipi kamwe hawezi kui-cover. Hata hivyo Mama anaweza beba majukumu karibu yote ya Baba na akayafanya kwa usahihi kabisa lakini jukumu la kumbariki Mtoto kamwe Mama hawezi kuli-Cover.

Kuna mtu anaweza akasema, mbona kuna watoto waliolelewa na Mama pekee, wakagombana na Baba zao, wakawatukana Baba zao, na bado wamefanikiwa kwenye maisha; Ukweli ni kuwa unaweza ukawa umefanikiwa kwenye maisha lakini maisha yako yasiwe ya baraka. Lazima ujue kutofautisha mafanikio na Maisha ya Baraka, aliyebarikiwa. Unaweza ukakuta mtu kafanikiwa lakini ni shoga, teja, anaharibu wanawake kwa kulala nao kama mnyama, amefanikiwa katika maisha lakini maisha yake hayana baraka kwa jamii.

Huwezi mkuta mtu aliyebarikiwa na Baba yake akawa na matatizo ndani ya jamii, hilo halijawahi kutokea na halitakuja kutokea kamwe.

Watoto wa zama hizi, najua mazingira ya karne hii ni magumu, huenda mama yako alitelekezwa akiwa na mimba yako, huenda Baba yako alikukataa, huenda Mama yako alifukuzwa na Baba yako, au sababu yoyote ile ambayo inakufanya usiwe karibu na Baba yako, inakufanya mchukie Baba yako, leo Taikon nakuambia kuwa, huyo ndiye Baba yako, huyo ndiye mwenye uwezo wa kukubariki ukapata baraka, huyo ndiye mungu katika nafasi ya hapa duniani, huyo Mama yako ni msaidizi wa huyo Baba yako tuu, atakupa kila kitu lakini kamwe hawezi kukupa baraka.

Lazima ujifunze kumheshimu Baba yako hata kama humjui, lazima ujifunze kumheshimu hata kama humuoni, heshima ndio ufunguo wa baraka zako katika maisha. Jamii zote duniani zilizoendelea na zilizostaarabika zinajua jambo hili, hata kama Baba atakuwa na mapungufu makubwa kiasi gani lakini huyo ndiye Baba, mungu mdogo aliyeshikilia dunia yako.

Kumkataa Baba ni sawa na wale wanaojiita Atheist, wasiomuamini Mungu, wasiotaka kutambua uwezo wa Mungu, lakini wanatambua uwepo wa Mama Dunia wanayemuona, Mama dunia anaweza kukupa yote lakini kuna mambo ya msingi kamwe hawezi kukupa. Uhai na baraka kamwe dunia haiwezi kukupatia.

Nisiandike sana, kuwachosha nafikiri nilichokuwa nataka kukisema mumekielewa, Msidanganywe na hawa wanawake ambao baadhi yao wanachuki na Baba zenu, tambueni kuwa wanawagombanisha na watu muhimu ambao ndio wenye uwezo wa kuwabariki mkabarikiwa, Wapendeni Mama zenu, lakini waheshimuni Baba zenu, nafikiri nimeeleweka.

Wababa nanyi mtambue kuwa hamna uwezo wowote wa kumlaani mtoto na laana ikashika, hakuna kitu kama hicho duniani,
Baba unachoweza kukifanya ni kutoa baraka. Wamama nanyi mtambue kuwa hamna uwezo wowote wa kubariki hata muwakumbatie watoto wenu kama dhahabu, mnachoweza ni kutoa laana ikashika. Hilo kila mmoja aliweke akilini.

Mwisho; Kwa mustakabali mwema wa watoto lazima Mama na Baba muwe kitu kimoja, muwajenge watoto katika misingi mema, mkijua kuwa bila ninyi wawili maisha ya mtoto yapo hatarini,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam.
 
.
FB_IMG_1592947497760.jpg
 
Ikiwa baba atabariki lakini mama akalaani ni kipi kitazidi nguvu chenzake, ni baraka au laana?

Baraka ndizo zitaishinda Laana.

Hakuna Baba ambaye hataki mtoto wake asimpende Mama yake, lakini wapo wamama wengi ambao hawataki watoto kuwapenda Baba zao.

Baba ndiye chanzo cha kila jambo, hata huyo mama ametoka kwa Baba.

Ukiona Mpaka Mtoto anamfurahisha Baba yake ujue hata kwa mama ni vivyo hivyo, ila wamama wengi huweza kutoa laana kisa hataki mtoto ampende Baba.
 
Safi sana taikon. Sasa kaa vzuri ungoje ma feminist wakija hapa kwa spidi ya ndege kuja kupingana na misimamo yako.

Huwaga naheshimu hata mawazo ya wapumbavu, ila hayanishughulishi.

Nimeandika kwa wema tuu kwa wanaotaka kizai chao kiwe bora, hata kama mtu amegombana na mzazi mwenzake aijtahidi athari zisimfikie mtoto kwa chuki zao
 
Most of the things unasema.hua ni ukweli sema changamoto ni kwamba siku hizi utandawazi umeleta jam kubwa. Hapa hapa kuna millenials, kuna gen z na wengineo. Kimapokeo kuna ukinzani mkubwa sana. Kwa mfano mtu aliezaliwa kuanzia 1995 kurudi nyuma, andiko hili lina mashiko na ukweli wote na pia atalielewa sana. Lakini kijana aliezaliwa miaka ya 2000 kuendela hapa humwambii kitu, anaona huu ni uzushi na mgando wa akili.
 
Hahahahah!

Umesema kweli kabisa, dunia inabadilika sana
 
Baraka ndizo zitaishinda Laana.

Hakuna Baba ambaye hataki mtoto wake asimpende Mama yake, lakini wapo wamama wengi ambao hawataki watoto kuwapenda Baba zao.

Baba ndiye chanzo cha kila jambo, hata huyo mama ametoka kwa Baba.

Ukiona Mpaka Mtoto anamfurahisha Baba yake ujue hata kwa mama ni vivyo hivyo, ila wamama wengi huweza kutoa laana kisa hataki mtoto ampende Baba.
Kweli kabisa yaani,nimeshawahi ona kitu ya hivi.
 
Baraka ndizo zitaishinda Laana.

Hakuna Baba ambaye hataki mtoto wake asimpende Mama yake, lakini wapo wamama wengi ambao hawataki watoto kuwapenda Baba zao.

Baba ndiye chanzo cha kila jambo, hata huyo mama ametoka kwa Baba.

Ukiona Mpaka Mtoto anamfurahisha Baba yake ujue hata kwa mama ni vivyo hivyo, ila wamama wengi huweza kutoa laana kisa hataki mtoto ampende Baba.
... wako ma-single mom's wamejaa chuki kiasi kwamba sio tu atamjengea mtoto chuki kwa baba yake bali hata kumfahamisha mwanaye baba yako ni fulani hawataki kabisa. Hii ni mbaya sana kwa mtoto kutomfahamu mzazi wake wa kiume hata kama alishakufa mtoto aambiwe ajue damu yake ni akina nani.
 
Hakuna watakachopata Kwa HAO watoto, niamini
 
Swali langu, ni kwamba hata kama mtoto alipatikana mara baada ya mama KUBAKWA bado baraka zitakuwepo??
 
Huwaga naheshimu hata mawazo ya wapumbavu, ila hayanishughulishi.

Nimeandika kwa wema tuu kwa wanaotaka kizai chao kiwe bora, hata kama mtu amegombana na mzazi mwenzake aijtahidi athari zisimfikie mtoto kwa chuki zao
Baba yupi maana wahenga husema anaetoka chumbani kwa mama yako na taulo ndio baba yako. Kwa lugha nyepesi ni kwama alieingia kwa mama yako ndio baba yako.
Kuna haya maisha ya digitali watu wanaume huacha mbegu na kupotea wanaacha watoto, wakati mwingine wanajikuta watoto wanalelewa na watu wengine. Sasa yupi baba mwe.nye uwezo wa kubariki? Anaelea na kutunza mtoto au alieacha mbegu ikamea ikawa.tunda
 
Baba mzazi, achana na hao wanaojipa majukumu yasiyoyao
 
Back
Top Bottom