Baraka hutoka kwa Baba; Laana hutoka kwa Mama, utaamua mwenyewe

Baraka hutoka kwa Baba; Laana hutoka kwa Mama, utaamua mwenyewe

Hapo ukienda kwenye maandiko huwezi kupata baraka kutoka kwa mama bali baraka hutoka kwa baba kwa sababu hata mungu hakupenda kuwapa uwezo huo kwani anajuwa udhaifu walio nao wakina mama wao huenda kinyume na neno la mungu kilga mara. Na hiyo ndiyo sababu hakupenda hata wanawake waongoze ibada , lakini kwa uwezo alio kuwa nao mwanamke leo anaongoza ibada mwanamke anaonekana anamapenzi ya kweli kwa mtoto lakini mwenye mapenzi ya kweli kwa mtoto ni baba kwakuwa humfundisha ukweli mtoto , hivyo mama huangalia anaemsikiliza na hutaka kumfanya awe juu na balaa huanzia hapo . Ndio maana hakuna nabii wala mitume wanawake. Kibinadamu mwanamke ndiyo kila kitu .
 
Ukweli ni kwamba kwa binadamu wakwanza kusikia na kufanya dhambi ni mwanamke, ndiye mwanamke alimdanganya mwanamume na hata chuki mwalimu ni mwanamke ndiyo mwalimu wa uongo nahufurahi anapo pata mume muongo , mfano mdogo ndoa nyingi huwa za taabu majaribu chuki na hata vifo sababu mama , mama hupenda kulipa kisasi humfundisha mtoto awe wakike au wakiume hivyo kama wakiume alisikia zaidi neno la mama akaoa mwanamke aliekosa neno la baba hapo ni chenga kwani chanya na chanya moto amini hili.
 
Ebhana nakubaliana na hoja yako imepita:

Siku zote huwa naamini kuwa kwa baba tunapata maelekezo ili maisha yawe mazuri.

Halafu kwa mama tunapata maonyo ili maisha yasiwe mabaya. Umeona hapo.

Baba atakufundisha kuendesha pikipiki, lakini mama atakuusia usiendeshe vibaya. Usipomsikiliza mama utavunjikavunjika upate taabu [laana] lakini ukimkosa baba ndio hata kuendesha hutajua, hutapata raha [baraka] ya pikipiki. Huu ni mfano.

Single moms; hata kama humpendi baba wa mtoto jitahidi tu kuhakikisha mtoto anapata baraka za babaake. Hebu hizo chuki kwa mzazi mwenzio zisiuzidi ule upendo kwa mwanao
 
Hii mada imekuwa influenced na hadithi ya Esau na Yakobo namna walivyopambania Baraka za baba yao Isaka.
 
BARAKA HUTOKA KWA BABA, LAANA HUTOKA KWA MAMA! UTAAMUA MWENYEWE!

Anaandika, Robert Heriel,
Mwanafalsafa.

Utaamua mwenyewe, utapima na kuamua maisha yako mwenyewe.

Baba ndiye mungu wa dunia, utake usitake, Mama ni msaidizi wa Baba upende usipende. Endapo hili halitatokea maisha ya mtoto huwa mashakani. Mtoto akigombana na Baba hukosa baraka, hata hivyo Baba hawezi kumlaani mtoto, Baba yu atoa baraka tuu, hana nguvu katika laana.

Mtoto akigombana na Mama hapo huchukua Laana, mama ndiye mwenye uwezo wa kutoa laana katika huu ulimwengu ikashika pasipo kizuizi. Lakini pamoja na umuhimu wa Mama hapa duniani lakini kamwe hana uwezo wa kumbariki mtoto aliyemzaa, hana mamlaka na hata akimbariki mara elfu moja mtoto hawezi kupata baraka hata moja. Labda sieleweki. Lakini mtanielewa tuu.

Unapoishi na wazazi lazima uelewe kila mzazi anamajukumu yake, anamipaka yake, ipo nafasi ya mama ambayo kamwe baba haiwezi ku-cover, lakini pia ipo nafasi ya Baba ambayo mama hata apinduke vipi kamwe hawezi kui-cover. Hata hivyo Mama anaweza beba majukumu karibu yote ya Baba na akayafanya kwa usahihi kabisa lakini jukumu la kumbariki Mtoto kamwe Mama hawezi kuli-Cover.

Kuna mtu anaweza akasema, mbona kuna watoto waliolelewa na Mama pekee, wakagombana na Baba zao, wakawatukana Baba zao, na bado wamefanikiwa kwenye maisha; Ukweli ni kuwa unaweza ukawa umefanikiwa kwenye maisha lakini maisha yako yasiwe ya baraka. Lazima ujue kutofautisha mafanikio na Maisha ya Baraka, aliyebarikiwa. Unaweza ukakuta mtu kafanikiwa lakini ni shoga, teja, anaharibu wanawake kwa kulala nao kama mnyama, amefanikiwa katika maisha lakini maisha yake hayana baraka kwa jamii.

Huwezi mkuta mtu aliyebarikiwa na Baba yake akawa na matatizo ndani ya jamii, hilo halijawahi kutokea na halitakuja kutokea kamwe.

Watoto wa zama hizi, najua mazingira ya karne hii ni magumu, huenda mama yako alitelekezwa akiwa na mimba yako, huenda Baba yako alikukataa, huenda Mama yako alifukuzwa na Baba yako, au sababu yoyote ile ambayo inakufanya usiwe karibu na Baba yako, inakufanya mchukie Baba yako, leo Taikon nakuambia kuwa, huyo ndiye Baba yako, huyo ndiye mwenye uwezo wa kukubariki ukapata baraka, huyo ndiye mungu katika nafasi ya hapa duniani, huyo Mama yako ni msaidizi wa huyo Baba yako tuu, atakupa kila kitu lakini kamwe hawezi kukupa baraka.

Lazima ujifunze kumheshimu Baba yako hata kama humjui, lazima ujifunze kumheshimu hata kama humuoni, heshima ndio ufunguo wa baraka zako katika maisha. Jamii zote duniani zilizoendelea na zilizostaarabika zinajua jambo hili, hata kama Baba atakuwa na mapungufu makubwa kiasi gani lakini huyo ndiye Baba, mungu mdogo aliyeshikilia dunia yako.

Kumkataa Baba ni sawa na wale wanaojiita Atheist, wasiomuamini Mungu, wasiotaka kutambua uwezo wa Mungu, lakini wanatambua uwepo wa Mama Dunia wanayemuona, Mama dunia anaweza kukupa yote lakini kuna mambo ya msingi kamwe hawezi kukupa. Uhai na baraka kamwe dunia haiwezi kukupatia.

Nisiandike sana, kuwachosha nafikiri nilichokuwa nataka kukisema mumekielewa, Msidanganywe na hawa wanawake ambao baadhi yao wanachuki na Baba zenu, tambueni kuwa wanawagombanisha na watu muhimu ambao ndio wenye uwezo wa kuwabariki mkabarikiwa, Wapendeni Mama zenu, lakini waheshimuni Baba zenu, nafikiri nimeeleweka.

Wababa nanyi mtambue kuwa hamna uwezo wowote wa kumlaani mtoto na laana ikashika, hakuna kitu kama hicho duniani,
Baba unachoweza kukifanya ni kutoa baraka. Wamama nanyi mtambue kuwa hamna uwezo wowote wa kubariki hata muwakumbatie watoto wenu kama dhahabu, mnachoweza ni kutoa laana ikashika. Hilo kila mmoja aliweke akilini.

Mwisho; Kwa mustakabali mwema wa watoto lazima Mama na Baba muwe kitu kimoja, muwajenge watoto katika misingi mema, mkijua kuwa bila ninyi wawili maisha ya mtoto yapo hatarini,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam.
Nzuli sana
 
Wote ni wazazi, lazima wapendwe woote, ila mkitaka mtafute thamani ya yupi juu, basi thamani ya mama ni mara 3 ya ile ya baba
"heshimu baba na mama upate baraka hapa duniani" hiyo ya baraka ni ya baba sijui umeiokota wapi mzee!!? Na tukaambiwa "pepo zenu ziko chini ya nyayo za mama zenu"
 
Baba katupwa jela miaka 30 kisa kampa mimba mama Ili uzaliwe, hapa mtoto hawezi kuwa na upendo kwa mama
 
Back
Top Bottom