Baraka hutoka kwa Baba; Laana hutoka kwa Mama, utaamua mwenyewe

Baraka hutoka kwa Baba; Laana hutoka kwa Mama, utaamua mwenyewe

Hakuna haki ya kuonewa huruma Mkuu?

Wala hakuna sheria yoyote inayomtaka mtu kumuonea huruma mtu mwingine, huruma ni hiyari ya mtu.

Wanawake wanahaki ya kupendwa,

Na lile andiko lako lingine

MWANAMKE MPUMBAVU UPIGWA ILI UPUMBAVU UMTOKE..

Hapa kweli naona kuwa hakuna haki ya kuonewa huruma..
utawauwa mkuu.. hawa wanawake kuwa makini mkuu
 
Kama nimekuelewa vizuri wewe na mzee Robert ni kwamba, mzee Robert kaeleza facts za mambo yalivyo duniai, halafu wewe ungependa hiyo hali i balance; kwa maneno mengine wewe unapenda HAKI sawa na sio facts, yaani ungependa kama ingewezekana pia hata mama awe anatoa MBEGU na baba abebe mimba which is not possible.
Maelezo ya mzee Taikon ni kwa mtazamo wa ki fact sio anavyo penda yeye IWE, mfano, hivi unadhani yeye kama mwanaume HAPENDI kulaani mtoto wake msumbufu? May be anapenda but facts zinakataa, baba hana uwezo wa kulaani mwanae isipokua ana uwezo only wa kumbariki mwanae. Hebu msome tena, nadhani huyu mzee haja kurupuka. Labda ungemuuliza, hu ni utafiti wake binafsi au mambo ya IMANI? Binafsi nakubaliana nae kwa almost 95% ya aliyasema, nimeyaona, nimeyashuhudia!

Umeelewa tofauti mkuu hapo umetoa maelezo yako wewe unavyotaka maelezo yangu ni tofauti kabsa na wewe ulivyochambua vile unapenda
 
Na lile andiko lako lingine

MWANAMKE MPUMBAVU UPIGWA ILI UPUMBAVU UMTOKE..

Hapa kweli naona kuwa hakuna haki ya kuonewa huruma..
utawauwa mkuu.. hawa wanawake kuwa makini mkuu

Mbona Mimi naishi peace na wanawake, wanaonijua watasema.
Usije ukadhani natumia Fake ID nijisifu bure.

Ninachokisema ndio uhalisia,
Mwanamke Mpumbavu anapaswa apigwe mpaka upumbavu umtoke.

Kumbuka niliandika pia usiolewe na Mwanaume Masikini na Mpumbavu, ili kuepuka kupigwa kisa mambo ya kipumbavu.

Sema wewe hujanielewa tuu bado.
 
Na lile andiko lako lingine

MWANAMKE MPUMBAVU UPIGWA ILI UPUMBAVU UMTOKE..

Hapa kweli naona kuwa hakuna haki ya kuonewa huruma..
utawauwa mkuu.. hawa wanawake kuwa makini mkuu



Sipo hapa kumtetea au kuumiza yeyote
 

Sipo hapa kumtetea au kuumiza yeyote

Sitaki niilinganishe hii na mada ingine yeyote

Ukisema apigwe mkuu ina sound kupigwa kama ni haki yake vilee au wewe unaionaje? Ukimpiga unaweza ukamsababishia madhara fulani au kumuua kabsa katika kumpiga kwako..

Na kama ungeamua kumfundisha japo kwa udogo kwa mda mrefu atakuwa vyema kama anavyotakiwa awe atatokwa na upumbavu..

Kumpiga inaweza kuwa suluhisho kweli? Mkuu
 
Hivi mpaka umlaani mtoto wako wa damu yako anakuwa amekufanyia kosa gani kubwa hivyo?

Ni maandiko yanayosema msilaani msije kulaaniwa, sasa hizo laana kwangu zaona nyingi ni kazi ya shetani.
 
Sitaki niilinganishe hii na mada ingine yeyote

Ukisema apigwe mkuu ina sound kupigwa kama ni haki yake vilee au wewe unaionaje? Ukimpiga unaweza ukamsababishia madhara fulani au kumuua kabsa katika kumpiga kwako..

Na kama ungeamua kumfundisha japo kwa udogo kwa mda mrefu atakuwa vyema kama anavyotakiwa awe atatokwa na upumbavu..

Kumpiga inaweza kuwa suluhisho kweli? Mkuu


Mbwa Mzee hafundishwi kuwinda.

Kwa heri
 
Most of the things unasema.hua ni ukweli sema changamoto ni kwamba siku hizi utandawazi umeleta jam kubwa. Hapa hapa kuna millenials, kuna gen z na wengineo. Kimapokeo kuna ukinzani mkubwa sana. Kwa mfano mtu aliezaliwa kuanzia 1995 kurudi nyuma, andiko hili lina mashiko na ukweli wote na pia atalielewa sana. Lakini kijana aliezaliwa miaka ya 2000 kuendela hapa humwambii kitu, anaona huu ni uzushi na mgando wa akili.
Tena hawa watoto waliolelewa na single mother ndio kabisaaaa, wakipitia huu uzi watakua wanafyonza kimoyo moyo.
 
Nakuunga mkono marehemu.
Kheh!!! Yani nimeshtuka halafu nikajikuta nacheka tu.ROHO yangu bado ni hai,thats why bado whitney tribute ni nyingi,kuanzia muonekano,style ya nywele mpaka voice covers,nimekaa zangu kwa kutulia nawachora tu nione nani atafanya tribute ya dental figure na smile,teh!Teh! THE VOICE
 
Hivi mpaka umlaani mtoto wako wa damu yako anakuwa amekufanyia kosa gani kubwa hivyo?

Ni maandiko yanayosema msilaani msije kulaaniwa, sasa hizo laana kwangu zaona nyingi ni kazi ya shetani.
Kuna wazazi wengine mtoto hata akisahau kuosha viombo tu anamuapiza na kumlaani juu.
Kikubwa ni kujiepusha sana na tabia za kuapiza na kulaani hovyo hovyo maana hii hali hua inarithi toka kizazi hadi kizazi.
Kuna familia bibi alimlaani mwanae, mwanae nae baada ya kuzaa ikawa kila mara kuwalaani watoto na watoto (wajukuu) baada ya kupata watoto nao ni yaleyale.
Laana hua ina kawaida ya kutembee mpaka kizazi cha 3, cha nne mpaka kizazi cha tano.
 
BARAKA HUTOKA KWA BABA, LAANA HUTOKA KWA MAMA! UTAAMUA MWENYEWE!

Anaandika, Robert Heriel,
Mwanafalsafa.

Utaamua mwenyewe, utapima na kuamua maisha yako mwenyewe.

Baba ndiye mungu wa dunia, utake usitake, Mama ni msaidizi wa Baba upende usipende. Endapo hili halitatokea maisha ya mtoto huwa mashakani. Mtoto akigombana na Baba hukosa baraka, hata hivyo Baba hawezi kumlaani mtoto, Baba yu atoa baraka tuu, hana nguvu katika laana.

Mtoto akigombana na Mama hapo huchukua Laana, mama ndiye mwenye uwezo wa kutoa laana katika huu ulimwengu ikashika pasipo kizuizi. Lakini pamoja na umuhimu wa Mama hapa duniani lakini kamwe hana uwezo wa kumbariki mtoto aliyemzaa, hana mamlaka na hata akimbariki mara elfu moja mtoto hawezi kupata baraka hata moja. Labda sieleweki. Lakini mtanielewa tuu.

Unapoishi na wazazi lazima uelewe kila mzazi anamajukumu yake, anamipaka yake, ipo nafasi ya mama ambayo kamwe baba haiwezi ku-cover, lakini pia ipo nafasi ya Baba ambayo mama hata apinduke vipi kamwe hawezi kui-cover. Hata hivyo Mama anaweza beba majukumu karibu yote ya Baba na akayafanya kwa usahihi kabisa lakini jukumu la kumbariki Mtoto kamwe Mama hawezi kuli-Cover.

Kuna mtu anaweza akasema, mbona kuna watoto waliolelewa na Mama pekee, wakagombana na Baba zao, wakawatukana Baba zao, na bado wamefanikiwa kwenye maisha; Ukweli ni kuwa unaweza ukawa umefanikiwa kwenye maisha lakini maisha yako yasiwe ya baraka. Lazima ujue kutofautisha mafanikio na Maisha ya Baraka, aliyebarikiwa. Unaweza ukakuta mtu kafanikiwa lakini ni shoga, teja, anaharibu wanawake kwa kulala nao kama mnyama, amefanikiwa katika maisha lakini maisha yake hayana baraka kwa jamii.

Huwezi mkuta mtu aliyebarikiwa na Baba yake akawa na matatizo ndani ya jamii, hilo halijawahi kutokea na halitakuja kutokea kamwe.

Watoto wa zama hizi, najua mazingira ya karne hii ni magumu, huenda mama yako alitelekezwa akiwa na mimba yako, huenda Baba yako alikukataa, huenda Mama yako alifukuzwa na Baba yako, au sababu yoyote ile ambayo inakufanya usiwe karibu na Baba yako, inakufanya mchukie Baba yako, leo Taikon nakuambia kuwa, huyo ndiye Baba yako, huyo ndiye mwenye uwezo wa kukubariki ukapata baraka, huyo ndiye mungu katika nafasi ya hapa duniani, huyo Mama yako ni msaidizi wa huyo Baba yako tuu, atakupa kila kitu lakini kamwe hawezi kukupa baraka.

Lazima ujifunze kumheshimu Baba yako hata kama humjui, lazima ujifunze kumheshimu hata kama humuoni, heshima ndio ufunguo wa baraka zako katika maisha. Jamii zote duniani zilizoendelea na zilizostaarabika zinajua jambo hili, hata kama Baba atakuwa na mapungufu makubwa kiasi gani lakini huyo ndiye Baba, mungu mdogo aliyeshikilia dunia yako.

Kumkataa Baba ni sawa na wale wanaojiita Atheist, wasiomuamini Mungu, wasiotaka kutambua uwezo wa Mungu, lakini wanatambua uwepo wa Mama Dunia wanayemuona, Mama dunia anaweza kukupa yote lakini kuna mambo ya msingi kamwe hawezi kukupa. Uhai na baraka kamwe dunia haiwezi kukupatia.

Nisiandike sana, kuwachosha nafikiri nilichokuwa nataka kukisema mumekielewa, Msidanganywe na hawa wanawake ambao baadhi yao wanachuki na Baba zenu, tambueni kuwa wanawagombanisha na watu muhimu ambao ndio wenye uwezo wa kuwabariki mkabarikiwa, Wapendeni Mama zenu, lakini waheshimuni Baba zenu, nafikiri nimeeleweka.

Wababa nanyi mtambue kuwa hamna uwezo wowote wa kumlaani mtoto na laana ikashika, hakuna kitu kama hicho duniani,
Baba unachoweza kukifanya ni kutoa baraka. Wamama nanyi mtambue kuwa hamna uwezo wowote wa kubariki hata muwakumbatie watoto wenu kama dhahabu, mnachoweza ni kutoa laana ikashika. Hilo kila mmoja aliweke akilini.

Mwisho; Kwa mustakabali mwema wa watoto lazima Mama na Baba muwe kitu kimoja, muwajenge watoto katika misingi mema, mkijua kuwa bila ninyi wawili maisha ya mtoto yapo hatarini,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam.
Tarudi
 
Wanawake ni viumbe wenye roho mbaya sana..kila siku kuwalisha sumu watoto wawachukie baba zao
 
Mwanafalsafa Taikon, mtu na fasihi yake.

Nashukuru kwa ku-share nasi mawazo yako.
 
Back
Top Bottom