Baraka hutoka kwa Baba; Laana hutoka kwa Mama, utaamua mwenyewe

Mama hana kitu kingine ambacho anaweza kutoa zaidi ya laana ?

Unawakosea sana kina mama mkuu pengine ulipo soma ndio wamekufundisha hivyo na kama umetoa kichwani kwako jitafakari..

Kwanini mama umpe hasi Baba umpe chanya kwanini usingewape wote hasi au wote chanya na kuzichambua ueleweke .. watalaumiwa walimu wako sio wewe..

Mtoto akilelewa/akimuelewa na Baba kwa kawaida Baba ni mantiki yaani mtoto anakuwa na maendeleo ya kiuchumi anafanikiwa katika kipato na utawala uongozi wowote ulee na mambo yake mengine yanakuwa na mafanikio .. ndio mafundisho sahihi..

Na mtoto akilelewa/akimuelewa Mama kwa kawaida mtoto anakuwa na tabia njema na matendo ya kuwapendeza watu kwa sababu mama ni tabia mtoto atakuwa na hadabu atafanikiwa kwenye upendo na nidhamu kiujumla.. ndio mafundisho sahihi...

Na ikitokea mtoto akalelewa/kuelewa wote wawili Baba na Mama basi anapata vyote hivyo maendeleo kiuchumi/kifedha na utawala (utekelezaji )kwa Baba kwa kuwa Baba ni kiongozi/mantiki wa familia pia atafanikiwa ki-matendo na tabia njema kwa mama kwa kuwa mama ni mjumuiko ya tabia njema mtoto atakuwa na nidhamu nzuri na upendo pia yaani mapenzi bora kwa wenzake..

Na mtoto akiwa na vyote hivyo hakuna atayeweza kumuendesha popote aendapo kinyume chake akikosa kimoja au vyote ataendeshwa popote aendapo ..

Jitahidi mtoto wako apate vyote hivyo..
 
Andiko lako ni upotoshaji mkubwa otherwise utupatie marejeo ya andiko lako sio kutunga na kutulisha matango pori
 
Andiko lako ni upotoshaji mkubwa otherwise utupatie marejeo ya andiko lako sio kutunga na kutulisha matango pori

Sio kila mtu anarejelea, marejeleo ni Kwa watu waliojifunza Kwa wengine,
Mimi sijajifunza hili Kwa yeyote, ni Jambo nililoliona Kwa macho tuu ya kawaida, hata watu wengine wanaweza kuwa wameliona sema hawakuandika.

Ninyi ndio mtarejelea, mliozoea kujifunza Kwa watu wengine,
 
Vipi ambao baba zetu ambao walifariki tukiwa wadogo lakini tukalelewa na ndugu wengine wa kiume. Inakuaje hapa taikon na wametulea vizuri na majukumu ya ubaba wameyabeba kwa 100%.
Nb mama hakuolewa tena baada ya baba kufa.

Swali :je hao walionilea mf bamdogo, shemeji nk nao hutoa baraka?
 
Baba mzazi, achana na hao wanaojipa majukumu yasiyoyao
Hakika nakubalianq na wewe mkuu. Kwani hata biblia inasema
Ibrahim alimbariki Isaka akabarikiwa na uzao wake, nae Isaka alpokaribia kufa alimuambia mwanae aliempenda Esau akamfanyie mawindo ili amuandalie chakula akipendacho ale ashibe aweze kumbariki, lakini mama aliposikia alimuambia mwanae aliempenda nae ni Yakobo alete ndama ili aandae chakula apewe baba ili ambariki kwani tayari Isaka alishakuwa kipofu. Baada ya kushiba alimbariki yakobo, na Esau aliporudi alikuta baraka imeshatolewa kwa wingi wote kwa Yakobo mdogo wake. Sijaona popote mama akibariki bali baba. Hakika bataka hutoka kwa baba na liana hutoka kwa mama.
 


Watakubishia
 
Kama nimekuelewa vizuri wewe na mzee Robert ni kwamba, mzee Robert kaeleza facts za mambo yalivyo duniai, halafu wewe ungependa hiyo hali i balance; kwa maneno mengine wewe unapenda HAKI sawa na sio facts, yaani ungependa kama ingewezekana pia hata mama awe anatoa MBEGU na baba abebe mimba which is not possible.
Maelezo ya mzee Taikon ni kwa mtazamo wa ki fact sio anavyo penda yeye IWE, mfano, hivi unadhani yeye kama mwanaume HAPENDI kulaani mtoto wake msumbufu? May be anapenda but facts zinakataa, baba hana uwezo wa kulaani mwanae isipokua ana uwezo only wa kumbariki mwanae. Hebu msome tena, nadhani huyu mzee haja kurupuka. Labda ungemuuliza, hu ni utafiti wake binafsi au mambo ya IMANI? Binafsi nakubaliana nae kwa almost 95% ya aliyasema, nimeyaona, nimeyashuhudia!
 
Hakuna kitu chepasi kukifafanua kama baraka na laana katika maisha haya ya siku hizi. Yaaani we unakuwa tu unalazimisha matatizo na laana mafanikio na baraka. Unaduka lako ikatokea ukamzidishia chenji mteja kimakosa unasema laana hii inanisumbua. Ila siku unachukua bidhaa ukapewa zingine za mkopo hapo baraka za baba zinafanya kazi. Kwenye maisha lazima kipindi kigumu kiwemo ila pia kipindi cha furaha razima kiwemo. Mfano kitu ulichocheza na akili zetu nikuwa. Hata kama utafanikiwa pasipo baraka za baba basi lazima mafanikio yako yawe na shida kwenye jamii. So kwabinadamu wa sasa uwe na mafanikio kisha jamii ikuchukulie safi tu na haya mawivu ya watu siyo rahisi

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 

Hakuna haki ya kuonewa huruma Mkuu?

Wala hakuna sheria yoyote inayomtaka mtu kumuonea huruma mtu mwingine, huruma ni hiyari ya mtu.

Wanawake wanahaki ya kupendwa,
 

Na laana ni pale upo kipindi cha mafanikio lakini yanaleta madhara ndani yako, familia au jamii.
 
@ROBERT HERIEL
 

Mimi nimelezea Baraka na Laana, nikaeleza nani anauwezo wa kuamua kati ya hivyo.

Majukumu mengine ya mama ambayo ni mema sijayaeleza kama ilivyo kwa baba.

Labda kama unahisia kama ninawazingua kinamama, lakini sivyo, kama ningeongea kinyume chake ningekuwa nawazingua.
 
@ROBERT HERIEL

Yes huweza kutoa baraka, lakini baraka ni matokeo ya matendo mema uyatendayo, kutokumdharau Baba na mama yako. Iwe akiwa hai au akiwa amekufa.

Baba hawezi ruhusu watoto wamdharau mama yao hata kwa nini,
Ila wamama wanaweza kuruhusu mtoto amdharau Baba yake,
Ndio maana wa mama wengi(sio wote) husema mapungufu ya Baba kwa watoto wao, ila ni ngumu kumkuta baba akisema mapungufu ya mama kwa watoto.

ushahidi upo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…