Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Hizi mambo za udini zimekuwa nyingi sana siku hizi sijui shida ni kitu gani,ikiendelea hivi nafkiri tutavuna tulichokipanda mana ukizungumzia neno tu dini tayar ushagawa maelfu ya watu...

Huwa hizi fikra ndo zinaanza hiv hivi kama hapa jukwaani mwishoni yakilipuka hakuna wa kuzima yani hakuna kabisaaa wa kuzima huu mto nafikiri watu tuangalie vizuri hili tego na tunajua jinsi nchi za kiafrika zilivyo upuuzi mdogo tu unalipuka,mana hili jambo siyo chama kusema kuwa mtu ataliacha lipite ila dini inaishi moyoni kwa mtu ni hatari sana.

Leo hii vijana wadogo watakaosoma haya tuyaandikayo yatawaingia na kuanza kubaguana mana vjana Leo hii wanameza kila kitu,tutafakari vizuri kabla ya hatari kutokea
 
Acha ramli chonganishi na udini!
Hakuna aliyekuwa mchonganishi hapa zaidi ya magufuli, nimempigania nimemtetea, lakini kwa hili apana nampinga na sikubali.

Amefanya kosa kubwa sana, waislamu wanahaki ya kuandamana kupinga ubaradhuli huu kwa nguvu zote.

Magufuli umewahalalishia watu kuwa wafuasi wa Sheikh Ponda na kumuunga mkono.
 
Kwa kweli pamoja na ukatoliki wangu kwa afanyayo jpm kwa waislam ni precedence ambayo italeta tabu akichukua muislamu
Hahahahaha

Wachaga wakilalalmila kutokuwepo kwenye Cabinet sawa

Wanawake wakilalamika uchache wao kwny Cabinet sawa

Waislam hairuhusiwi kulalamika… ngoja atokee Rais Mwislam halafu waislam wafike 40% usikie kelele za vigango na parokiani kama wakati wa Jakaya walipofika 36 % hadi Mtikila akaandika Waraka eti Jakaya ni Gaidi anaetaka kusilimisha Nchi akaugawa kwny Mkutano wa Jukwaa la Kikristo akasifiwa sana na Ma Baba Askof kwa 'Uzalendo' akiitwa Mfia Kristo…
 
Kuwaridhisha waislamu ni kazi sana aisee!

Hebu ona viongozi wakubwa wote tangu makamu wa Rais hadi waziri mkuu wote ni waislam ila kwenye baraza tu ndio nongwa.
 
sisi sote tunajenga nyumba mmoja ya kuishi sisi na vizazi vyetu vya sasa na vijavyo hivyo hakuna haja ya kugombea tofali za kujengea
 
Rais angekuwa ni muislamu na akateua waislamu wakutosha (kama nusu tu ya baraza zima), leo jumapili makanisani zingesomwa nyaraka za maaskofu kuipinga serikali, mahubiri na maombi yangekuwa ni kuipinga serikali, wakristo wangeambiwa wafunge siku kadhaa dhidi ya uislamu kushamiri hapa Tz nk.

Viongozi wa kikristo nawajua vizuri.
Ndo shida,yaani mungu atunusuru,najiskia kichefuchefu,hii nchi ni ya kikatoliki
 
wakati nyinyi mnaona kasoro baraza la mawaziri,mimi naona kasoro rais mwenyewe. niko mbali zaidi yenu kumbe
 
Kwa kifupi, teuzi nyingi za Magufuli zimekaa kuelemea upande mmoja wa dini

Nakumbuka Kikwete alishaandamwa sana na Baraza la maaskofu kisa tu teuzi zake ilikuwa unakuta kati ya watu 10 basi watu watano wakiwa muslim basi ni waraka kila kona
 
Moja: Balaza la Mawazili ni pamoja na manaibu, je manaibu wale hujawaona?!?

Mbili: Balaza la Mawazili ni pamoja na Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu, Raisi wa Zanzibar, hawa nao ni makafiri?!? ewe uliyedini ya 'kweli'

Tatu: Nafasi za uongozi si zawadi, kwa dini, makabila, mikoa; hadi liwe ni swala la kufa na kupona, kwamba ni lazima dini, kabila, mkoa upate
Wewe msukuma " balaza " ndo nini?! "mawazili" ndo nini?!
 
b) Hili ni baraza la Tanganyika, Yawezekana vipi usiwe na baraza lenye waziri kamili hata mmoja Mzanzibar?

Naomba nifahamishwe pia kwenye Baraza la Mawaziri Zanzibar kuna mtanganyika alishawahi kuteuliwa nafasi ya uwaziri[emoji23]
Kwa zanzibar haiwezekani kuteua waziri kutoka bara, kwa sababu SMZ ni ya wazanzibari peke yao. Ila katika serikali ya JMT zanzibar inahusika, hivyo kukosekana waziri kutoka zanzibar sio sawa, hasa ukizingatia kwamba kuna wizara zinazo husika moja kwa moja na mambo ya muungano.
 
Huwa mnaungana pamoja na kuteteana kwenye maslahi ya watu wa dini yenu.

Nahisi ningeishia kutaja wanawake na wazanzibar peke yake mgeunga mkono hoja, ila kitendo cha kutaja kuhusu umuhimu wa kuwepo kwa notable inclusiveness ya waislamu kwenye baraza mmeona hii mada haijakaa sawa hahaha

Kemeeni teuzi za udini, nchi hii ni yetu sote

Lakini tutaendelea kulisema hili maana halijakaa sawa

Duu we jamaa kiboko. Umemaliza la vyama, sasa umeanza la uteuzi. It's good that you accepts the power of appointer, the man himself together with the appointees but only the composition. This's a remarkable mileage.
 
Magufuli ni mdini, waislamu ni wengi zaidi hii nchi lakini teuzi zote zinaenda kwenye dini moja. Hii hata sisi wafia chama tumekiona
 
mwaka huu ni maajabu WAZIRI WA MUUNGANO

Ummy Mwalimu
naibu
Mwita Waitara

wote wanatoka tanganyika na ni mawaziri wanaotakiwa kuonyesha sura ya muungano

Tunaamini Makamu Samia kashirikishwa pamoja na hussein mwinyi
 
Wakati wa KIKWETE unakumbuka mawaziri waislam walikuwa wangapi???,, achana na hilo, serikali kuu na wakuu wa mashirika ya Umma. Nakumbuka kwa mfano, Rais Kikwete alikuwa Muislam,,makamu wa Rais Muislam..jaji mkuu muislam,ukienda kwenye mashirika ya umma kama Nssf walikuwa waislam..ATC, mkaguzi mkuu hesabu za serikali.......ACHA UDINI

Kwahiyo tuendekeze Ubaguzi
Kikwete pamoja na yote alihitahidii kubalance makundi yote
 
Back
Top Bottom