Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

Baraza Jipya La Mawaziri hili hapa

Baraza Jipya: Wananchi wapinga uteuzi wa Andrew Chenge
* Wadai mikataba mibovu ilianzia kwake
* Wasifu uteuzi wa Magufuli, Ngeleja,

Na Waandishi Wetu

UTEUZI wa Andrew Chenge kuendelea na wadhifa aliokuwa nao katika Wizara ya Miundombinu umewachanganya wananchi wakidai kuwa hafai kutokana na kuhusika kwake na mikataba mibovu akiwa Mwananshria Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu.

Pia walisema tangu ashike wadhifa huo mwaka 1996 hakuna mabadiliko makubwa katika ujenzi wa barabara zaidi ya yale yaliyoachwa na serikali ya awamu ya tatu.

Jijini Mwanza, wananchi wengi waliokuwa wakusanyika katika vituo vya taksi wakisikiliza matangazo kupitia radio waliduwaa baada ya kusikia jina la Chenge likitajwa kuwamo katika baraza jipya.

Elias Mhegera mkazi wa jijini Mwanza alisema pamoja na kupunguzwa kwa baraza hilo, bado hajafurahishwa na uteuzi wa Chenge kwa kile alichodai kuwa ni mtu asiye makini kwa vile amekuwa akihusishwa na kashfa za ufisadi na kutajwa kila mara.

Alisema kuwa Chenge wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye aliyeishauri vibaya serikali na hatimaye kupitisha sheria ya takrima, na ile ya kuzuia wagombea kupinga matokeo ya uchaguzi mpaka wamelipa Sh5 milioni mahakamani.

�Sidhani kama Chenge ni mtu mzuri sana mpaka astahili kubaki katika baraza hilo, kwanza tukumbuke ndiye aliyeanzisha sheria ya takrima, pia alitunga na kupitisha sheria ambayo ilikuwa inazuia wagombea kufungua kesi wanaposhindwa uchaguzi mpaka walipe Sh5 milioni, ambayo ilifutwa baada ya kukatwa rufani Mahakama Kuu katika kesi ya Julius Ndyanabo,� alieleza. ��

Haa hivyo, baadhi ya wananchi walishangilia kuwepo kwa mawaziri wawili kutoka mkaoni Mwanza ( Laurence Masha na Ngeleja) huku wengine wakishangilia kuenguliwa kwa Diallo.

Walisema wamefurahisha na uteuzi huo ambao umeonekana kuzingatia kauli yake ya kuwaengua baadhi ya mawaziri ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakijihusisha zaidi na biashara pamoja na kutajwa katika kashfa mbalimbali za ufisadi.

Mohamed Moledina ambaye Mfanyabiashara jijini Mwanza, alisema kwa wastani ni baraza zuri na kwamba limezingatia damu changa pamoja na wasomi.

�Nimefurahisha na uteuzi huo, ametuonyesha kwamba anania kwani tuliodhani hawastaili pia amewatema, kikubwa sasa tunangoja utendaji kazi wao tu maana kuteua ni jambo moja na kutimiza matakwa ya wananchi,� alieleza.

Jane Fabian (Mfanyakazi sekta ya Umma) alisema kuwa amefurahisha na uteuzi huo kwa vile unatoa sura ya kuwa rais ni makini kwa kuteua watu makini na kuepuka wafanyabiashara kama alivyotamka katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita.��

Jijini Arusha, Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), wilaya ya Arusha.

Lazaro alidai kuwa kambi ya upinzani inashangazwa na uamuzi wa kumrejesha Chenge ambaye anadaiwa kuhusika kwenye mikataba mibovu wakati wa serikali ya Awamu ya Tatu.

Mkazi wa mjini Morogoro, Rolland Leonard alisema anachompongeza Rais Kikwete kwa kuwapunguza mawaziri waliokuwa wazee lakini alidai kuwa hakurudhishwa na� uteuzi wa mawaziri Chenge na Steven Wassira.

Naye Leonard ambaye ni mmiliki wa duka la dawa baridi la Holland alisema kuwa kurudishwa kwa baadhi ya mawaziri wasiowaadilifu ni kinyume na matarajio ya watanzania walio wengi.

Nicodemas Mbilingi alisema amefurahishwa na uteuzi huo lakini alimkosoa �Rais kwa kuwateua Chenge na Juma Kapuya kwa madai kuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa wakitajwa katika kundi la mawaziri wasiofaa na pia kuwa wazee.

�Baraza safi lakini sijafurahishwa na uteuzi wa Chenge, huyu alitajwa katika masuala ya ufisadi, alitakiwa ajisafishe kwanza na kwa upande wa kapuya nadhani ni waziri ambaye alistaili kupumzika na kuwaachia vijana kwani hana jipya. Hapa nadhani rais hajawatendea haki wananchi,� alieleza.

Wakizungumza mara baada ya uteuzi huo, wakazi mbali mbali wa manispaa ya Arusha walipongeza uteuzi huo ambao umeendelea kuwabakiza mawaziri wawili toka mkoa wa Arusha, Dk Batilda Burian, Wizara ya Mazingira na Jeremiah Sumari ambye ni Naibu Waziri wa Fedha.

Geso Bajuta ambaye ni mfugaji maarufu mkoani hapa na Mkurugenzi wa maduka ya madawa ya mifugo ya Bajuta Agrovet, alisema sasa wana imani kuwa matatizo ya wafugaji yatapatiwa ufumbuzi.

"Sisi wafugaji tunampongeza sana rais kumtea Magufuli wengi wanamjua na sasa tunaamini tutakuwa naye� kushughulikia matatizo ya wafugaji," alisema.

Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite, Rahim Massawe alipongeza mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini na kuamini kuwa matatizo ya wachimbaji wadogo yatapatiwa ufumbuzi.

Katibu wa wazazi wa shule ya Arusha Sekondari, Michael Sanga alipongeza sana Profesa Jumanne Maghembe kuteuliwa katika Wizara ya Elimu� na Profesa Peter Msola kuwa Wizara ya Kilimo na Ushirika.

Nicholaus Minja ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Biq Expedition Ltd ya Arusha pia alipongeza Wizara ya Utalii kupata mawaziri wapya

Naye Aristos Nikitas wa Morogoro alisema kuwa anampongeza raisi Kikwete kwa kufanya kile wananchi hasa kwa kulipa kipaumbele sula la kilimo cha umwagiliaji kwani wakulima walio wengi walikuwa wakikatishwa tamaa mfumo mbaya wa kilimo.

�Sisi wakulima tulikuwa nyuma sana nahisi tulisahaulika kabisa na serikali lakini kwa hili nampongeza sana raisi kwa kuwakumbuka wakulima hasa katika suala la umwagiliaji sasa nchi itakuwa kiuchumi kutokana na kilimo hicho cha umwagiliaji,� alisema.

�

Kwa upande wao Farida Msemwa, Alfred Samuel na Said Mkwinda waliwataka mawaziri walioteuliwa kufanya kazi kwa umakini zaidi na si kwa faida yao binafsi kwani dhamana waliokabidhiwa na rais ni kubwa.

Naye Alfred Samuel alisema kuwa hakuridhishwa na wizara aliyopewa Magufuli kwani alistahili wizara nyeti ili aweze kuwafichua watendaji wazembe.

�Kwa upande wangu sijaridhika kabisa na Magufuli kuwekwa wizara hiyo, alitakiwa kuwekwa wizara kama Miundombinu, Maliasili au hata angerudi Ardhi, ndizo wizara zinazomfaa hivyo kwa hilo rais hajatutendea haki watanzania ,� alisema Samuel.

Mji wa Moshi na vitongoji vyake jana jioni ulirindima kwa hoi hoi na vifijo baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza Baraza lake la Mawaziri ambapo baadhi ya wananchi, hususan wazee walisema 'Mwalimu Nyerere amefufuka'

"Huyu Rais Kikwete kwa kweli Mungu amjalie, tunadhani Baraza hili ameliunda kwa maelekezo ya hayati Baba wa Taifa, mwalimu Nyerere. Kwa kifupi ni baraza zuri tuliombee kwa Mungu, "alisema Ally Iddi mkazi wa Maili Sita.

Katika mgahawa mmoja ambapo umati wa wananchi ulikusanyika wakimtazama na kumsikiliza Rais akitaja safu ya mawaziri walishangiliwa kwa nguvu zote hususan waliposikia majina mapya.

Mwalimu mstaafu, Macsteven Mully mkazi wa Kijiji cha Chekereni amefurahishwa na uamuzi wa Rais wa kuboresha zaidi sekta ya elimu kwa kuweka maafisa elimu wa sekondari na shule za msingi kwenye wilaya.

Kwa upande wa aliyekuwa Waziri wa fedha, Zakhia Meghji, wananchi wengi wameiambia Mwananchi kuwa, waziri huyo alipaswa kuachia ngazi mapema kwa madai kuwa alishindwa kuiongoza wizara hiyo kwa muda wote aliokuwepo.

Mchungaji mmoja wa Kanisa la Kiiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, ambaye hakupenda kuandikwa jina lake, alilazimika kuendesha misa fupi katikati ya mji kuliombea baraza hilo la mawaziri na kumtakia afya njema Rais Kikwete.

Jijini Dar es Salaam watu walikusanyika katika vikundi mbalimbali katika mitaa ya kati kati ya jiji wakifuatilia kwa makini uteuzi wa mawaziri wapya katika baraza la mawaziri.

Watu haowalionekana wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete katika redio ndani ya magari ya serikali na binafsi na wengine katika redio ndogo za mkononi na wengine wakifuatilia kupitia katika redio zilizounganishwa katika simu zao za mkononi.

Kutokana na hali hiyo katika ofisi binafsi na zile za serikali walilazimika kuacha kufanya kazi zao za kila siku kwa muda na kwenda kusikiliza kutangazwa kwa baraza hilo.

Baadhi ya wananchi walionekana kufurahishwa na jinsi Rais Kikwete alivyounda upya baraza hilo na hasa hatua ya kupunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka mawaziri 61 hadi mawaziri 47.

Katika hatua nyingine, wafanyakazi wa Idara ya Uvuvi wameelezea kustushwa na wasiwasi wa kufanya kazi chini ya Waziri John Magufuli aliyeteuliwa jana kuwa waziri wa wizara hiyo.

Wakizungumza mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza Baraza lake jipya la mawaziri jana jioni, wafanyakazi hao walisema kutokana na utendaji kazi wa Waziri Magufuli watakuwa na wakati mgumu.

�Hivi kweli tutapona hapa kweli, � alisika akihoji mfanyakazi mmoja wa idara hiyo aliyekuwa akifuatilia hotuba hiyo ya Rais Kikwete ya kuunda baraza jipya.

�Kwa kweli hapa sasa tumekwisha yaani tunakuwa na Magufuli, hii ni balaa,� aliunga mkono mfanyakazi mwingine wa idara hiyo.

Mfanyakazi mwingine wa idara hiyo ambaye hakutaja jina lake alielezea kufurahishwa na hatua ya Rais Kikwete kuihamisha idara hiyo kutoka wizara ya Malia Asili na Utalii na kuiunganisha katika wizara ya Maendeleo ya Mifugo.

Waziri Magufuli ni miongoni mwa mawaziri waliojizolea sifa kubwa za uchapakazi,hasa katika serikali ya awamu ya tatu chini Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa,wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi.

Akiwa katika wizara hiyo Magufuli alionekana kuwa mwiba mchungu kwa watendaji wa serikali na kuweza kuwezesha kufanikisha ujenzi wa barabara nyingi,kazi ambayo bado inakumbukwa na Watanzania wengi.

Habari hii imeandikwa na Mussa Juma (Arusha), Lillian Lucas (Morogoro), Ally Sonda (Moshi), Frederick Katulanda (Mwanza) na James Magai (Dar es Salaam).
 
Ninaelewa vizuri sana maana ya elimu na elimu ya juu na ninaongea hili with great intellectual authority wala sihitaji kusubiri maelezo ya ziada ya JK ili kuelewa!

Kwa nadharia pale UDSM mko fiti sana mkuu wangu, tatizo ni hamjawahi ku-practise!

Kwa uhakika research zenu zina mengi ya kufikirika... lakini ki-utendaji aaaah!!!

Mimi nadhani chuo chetu kinasaidiwa na mfumo wa 7 4 2, ambapo miaka miwili (2) ya form six ni kama pre-university wenzetu wote hawana...

Nimesomea hapo mkuu...napafahamu saaaana tu.
 
kwa sasa naelekea DODOMA,nitatoa muhtasari kesho asubuhi ila kwa kuanzia.
1.nimesikitishwa sana,nimeonewa sana sababu LOWASSA KABAKi-nitaelezea
2.kwanini JK kaweka watu wa usalama zaidi ya 70%-tukianza na malima?
3.mambo ya kulindana bado yapo,kuna kipindi nilisema muungwana,shekifu na kapuya wanajiita RUNGU..HATA IWE VP LAZIMA WAFIKE 2015.
4.kwanini chenge?je ana siri gani na mkuu wa kaya?
5.kwanini msola?je matatizo ya BODI yameletwa na nani?
 
Katika Afrika and EA UD is the only University among 20 best in ranking! Vyuo vya Uganda na Kenya wako nyuma sana kwa hili!

Sijui na mimi ni kigezo gani kingine Kitila anatumia kulinganisha Kenya na Uganda!

Tunazungumzia ile ranking ambayo nasikia hata Mogadishu University ilipeta!!! Mimi university sijagusa lakini kweli tunaamini ndani ya nafsi yetu kwamba sisi ni among the top 20 universities in Africa! Kwa kipi hasa? Hivi vilemba vya ukoka vitatuua!
 
Sasa wewe umewahi kuona wapi unajilinganisha na wagonjwa wenzako ambao wanaumwa zaidi. Sisi ndio tunaongoza kwa elimu ya juu East Africa halafu unataka kutulinganisha na waganda na wakenya! Ninaelewa vizuri sana maana ya elimu na elimu ya juu na ninaongea hili with great intellectual authority wala sihitaji kusubiri maelezo ya ziada ya JK ili kuelewa!

....bro unaonekana unaleta rhetorical arguments tuu bila data na sijui nia yako ni nini? au inawezekana unaota tuu ndoto za mchana na sio vizuri kuja katika forum kama hii na kuongea vitu ambavyo hujui,kwa Taarifa yako kenya wana vyuo vikuu(with full accreditation) mara 6 na wanafunzi mara 10 zaidi ya Tanzania,idadi ya madaktari na wahandisi wanaomaliza vyuo vikuu kenya ni 6times ya wanaomaliza Tanzania na hata life quality ya campus zao kuanzia majengo,Lab,IT networks etc na idadi ya lectures/students,PHd holder faculty etc wako far ahead ukilinganisha na TZ...kwako ubora wa elimu sijui ni nini?
 
wakuu heshima mbele,kesho ni mbali so nakata ishu muda huu.
1.kama mnakumbuka wakati wa mjadala wa suala la buzwagi,katika kipindi cha je tutafika..mhe ADAM MALIMA a.k.a ALHAJ MALIMA,alimtetea sana karamagi kwamba alikuwa sahihi.Huyu ndiyo karamagi aliyerudishwa..na ni kibaraka wa LOWASSA,same wine but different bottle..jiandaeni kuunywa,sijui msimamo wa waziri wa nishati ila ni mtu wa sys. hana rekodi ya ufisadi labda aanze sasa,anamlinda JK
 
Mzee elimu ya juu tumeachwa sana hata kwa standard ya Afrika.

Hapana mkuu sio kweli; data zote zinaonyesha sisi tunaongoza kwa ubora japokuwa Kenya wanatuzidi kwa wingi wa mavyuo. Lakini kwa maana ya knowledge production and intellectual contribution, sisi tupo juu yao. Of course sote tu wagonjwa, lakini angalau sisi tunanafuu-yaani sisi bado tuna kauli wakati wao walishazimia kabisa, hawaongei tena imebaki roho tu inadudunda. Hili halina ubishi ndio hali halisi hata wao wanakiri hivyo.
 
kitila,

Nimefurahi sana kujua kuwa UD inaongoza. Mungu awajalie nyie mnaoendeleza kufundisha watanzania wenzetu ingawa pia mazingira yenyewe ni magumu ati!
 
Kosa kubwa tulilofanya Watanzania ni kusubiri kuona mazingaombwe au kuona mabadiliko makubwa sana.

Jiulize ukiwa kwenye viatu vya Kikwete, je ufanye mabadiliko makubwa ya kutisha ili kuonekana kuwa Uteuzi wa awali ulikuwa ni mbovu na kwamba wewe si makini ni mbabaishaji?

Pili, ili kumalizia malengo ya awamu, ni bora ulete watu wapya kabisa ambao ndio waanze kujifunza kazi na majukumu, au kuchukua wale walio japo bora kushikilia jahazi lisiende mrama na kuzama?

Tatu, je uko tayari kujenga mgawanyiko katika Chama na Serikali kutokana na makundi yaliyokwisha kujijenga?

Nne, je una uwezo Kikatiba kwenda nje ya wigo wa kawaida na kuleta watu wapya kabisa katika safu ya uwaziri bila watu hawa kuwa Wabunge?

Tano, je utateuwa watu watakaofuata "Nyayo" na kutekeleza maazimio au utatendelea kuwa na watu wenye utashi binafsi kutokana na nguvu zao "kichama" na ki mali?

Binafsi kuna majina ambayo nimeshangaa kuwa yamerudi, lakini naelewa ufinyu wa watu au uwezo wa Rais Kikatiba kuleta watu wapya ambao sisi tulikuwa tunawategemea. Watu kama Chenge, Msola, Mkullo, Nchimbi, Nagu si majina ambayo nilitarajia yangerudi. Lakini sisi si Kikwete kujua ni kwa mvuto gani wa kisiasa, kiutendaji au kiuwajibikaji hawa ndugu wamerudishwa madarakani.

Labda ni kutuliza zali linalokuja la utengano wa CCM. Yetu macho na masikio!
 
Heri yangu niliyeyusha mategemeo yangu (lower my expectation) katika hili na sasa ninafurahia tu nilichopata!

tik tak tik tak tik tak bado inaendelea
 
Hapana mkuu sio kweli; data zote zinaonyesha sisi tunaongoza kwa ubora japokuwa Kenya wanatuzidi kwa wingi wa mavyuo. Lakini kwa maana ya knowledge production and intellectual contribution, sisi tupo juu yao. Of course sote tu wagonjwa, lakini angalau sisi tunanafuu-yaani sisi bado tuna kauli wakati wao walishazimia kabisa, hawaongei tena imebaki roho tu inadudunda. Hili halina ubishi ndio hali halisi hata wao wanakiri hivyo.
Kitila,
Unaposema Tanzania inaongoza kwenye knowledge production and intellectual contribution, unatumia vigezo gani? na ni tafiti gani zinazotuweka sisi juu kuliko wenzetu? Hizo data zinazoonyesha kuwa sisi ubora wetu upo juu zaidi ya jirani zetu kwenye maeneo gani na je unakubaliana nazo hizo data wa kiasi gani?
 
Hapana mkuu sio kweli; data zote zinaonyesha sisi tunaongoza kwa ubora japokuwa Kenya wanatuzidi kwa wingi wa mavyuo. Lakini kwa maana ya knowledge production and intellectual contribution, sisi tupo juu yao. Of course sote tu wagonjwa, lakini angalau sisi tunanafuu-yaani sisi bado tuna kauli wakati wao walishazimia kabisa, hawaongei tena imebaki roho tu inadudunda. Hili halina ubishi ndio hali halisi hata wao wanakiri hivyo.

...toa data la sivyo stop misleading people kwa sababu unachoongea ni contrary na data zinazotumika kupima ubora wa elimu ya juu!
 
a 100% right.......

kwa mtu yeyote ambaye kasoma bongo mpaka 'versity level hasa sisi watu wa science, tunakubali kwamba elimu ya bongo mwisho ktk afrika!!! hata hao nigeria na SA wanatuzidi namba tu ya vyuo, lakini ktk kushusha nyanga tumewaacha flani(forget desa/mkoba...naongelea "ngunju" lenyewe)..tatizo ni kiingereza ndio kinapiga njenga!! wakenya na waganda wanatuogopa sana.
 
....sasa mkuu naona umeenda too far mpaka kusema Tanzania is better than South Africa isipokuwa namba ya vyuo tuu!
 
...toa data la sivyo stop misleading people kwa sababu unachoongea ni contrary na data zinazotumika kupima ubora wa elimu ya juu!

Research Council. Starting from the assumption that the Web has become one of the main sources to obtain information on academic and scientific activities, these rankings are based on several "webometrics" indicators: size, visibility, popularity and number of rich files. Click here to learn more on ranking methodology.

--------------------------------------------------------------------------------------------------^^^

The InternetLab Ranking of 30 Top African Universities
Rank University Country World Rank
1 University of Cape Town South Africa 398
2 Universiteit Stellenbosch South Africa 566
3 Universiteit van Pretoria - University of Pretoria South Africa 718
4 University of the Witwatersrand South Africa 720
5 Rhodes University South Africa 738
6 University of South Africa South Africa 1,449
7 University of the Western Cape South Africa 1,553
8 American University in Cairo Egypt 1,826
9 Noordwes Universiteit - North West University South Africa 1,857
10 University of KwaZulu-Natal South Africa 2,214
11 University of Johannesburg South Africa 2,323
12 University of the Free State South Africa 2,369
13 Université de La Reunion France 2,387
14 Nelson Mandela Metropolitan University South Africa 2,542
15 University of Dar Es Salam Tanzania 2,819
16 University of Zimbabwe Zimbabwe 3,072
17 Al Akhawayn University in Ifrane Morocco 3,174
18 Cape Technikon South Africa 3,414
19 University of Mauritius Mauritius 3,682
20 University of Zululand South Africa 3,724
 
Kuna kitu anachoshindwa kukifanya Kikwete kuhusu hawa watu wawili; na badala yake anabaki kutumaini tu kuwa labda wahusika watajiondoa wenyewe wakichoshwa na mizunguko: Watu hao ni Magufuli na mwenzake Mwandosya.

Lakini kwa mshangao mkubwa kwa Kikwete, jamaa hawa wanaendelea tu kunawili na kufurahia maisha kila waendako.
 
....sasa mkuu naona umeenda too far mpaka kusema Tanzania is better than South Africa isipokuwa namba ya vyuo tuu!

mkuu ni kweli, tupo fit......kama sio chuo, basi products zake na maandalizi toka high ni kiboko!!!ukiwa umemaliza six bongo ktk PCM au PCB unasukuma college popote duniani kama "unaendesha baiskeli kwenye mteremko," kiulaini hasa miaka miwili ya kwanza.

I KNOW THAT!!!.
 
1. Kwa taarifa yako, ile wizara iko chini ya Rais sio Simba au mtu mwingine. Waziri ofisi ya Rais ni Msaidizi tu.

2. Boss waa PCCB na Usalama wa Taifa ni Rais mwenyewe.

3. Waziri wa Utawala bora yupo tu kwa ku-manage budget na vitu vichache chache... kama tume ya maadili ambayo pia hu-ripoti kwa Rais moja kwa moja...

4. Nakubaliana nawe kwamba sitamani kuona huyu mama kama waziri but I have nothing i can do.

Muungwana Nielimishe,Hawa mawaziri katika ofisi ya Rais,Makamu wa Rais na Waziri mkuu hawapigi kura katika baraza la mawaziri?
 
Safi Sana Fisadi Mramba Kuondoka.

Ila Magufuri Ilitakiwa Atoke. Hawa Wawili Mkapa Alimuachia Maagizo Jk Lazima Wawe Kwenye Baraza Lake 2006 Hawa Ndio Wachukuwa Rushwa Wa Mkapa. Mramba Asikishwe Mahakamani Na Mtandao Wake Wa Tra Uondolewe.

Malaya Wa Mkapa Rita Mlaki Ulikuwa Mzigo Nae Ahojiwe Katoa Wapi Pesa Za Ajabu?

Membe Nae Kwanini Amerudi? Hadi Atuumize Ndio Tumtoe? Jk Acha Kuwa Na Marafiki Wajinga.

Mary Nagu,mahanga Na Mathayo David(mtoto Wa Msuya Cleopa Wa Nje) Ilitakiwa Watolewe Kwa Kuwa Na Vyeti Feki Phd Zao.

Dr Nchimbi Na Kamala Watoto Wa Professor Warioba Safi Sana Fikiraduni, Mbopo Na Kichuguu Wanaumia.
 
Just imagine this, Mwandosya, Magufuli, Wasira and Msolla all four heads focusing on 80% of Nations backbone!

Hili nimependelea hata kama watu tunamchukia Msolla.

This is revolution to have Magufuli nd Mwandosya who are industrious and competetive to lead Umwagiliaji, Mifugo na Uvuvi. So is Wasira with Tamisemi!

Hapa nampa JK heko, maana hakuwapa vilaza hizo kazi, kawapa wachapa kazi na wabunifu! Focus ya sasa ni kujenga vijiji, wakulima na kuleta mapinduzi ya uzalishaji mali vijijini!
 
Back
Top Bottom