Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
Baraza Jipya: Wananchi wapinga uteuzi wa Andrew Chenge
* Wadai mikataba mibovu ilianzia kwake
* Wasifu uteuzi wa Magufuli, Ngeleja,
Na Waandishi Wetu
UTEUZI wa Andrew Chenge kuendelea na wadhifa aliokuwa nao katika Wizara ya Miundombinu umewachanganya wananchi wakidai kuwa hafai kutokana na kuhusika kwake na mikataba mibovu akiwa Mwananshria Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu.
Pia walisema tangu ashike wadhifa huo mwaka 1996 hakuna mabadiliko makubwa katika ujenzi wa barabara zaidi ya yale yaliyoachwa na serikali ya awamu ya tatu.
Jijini Mwanza, wananchi wengi waliokuwa wakusanyika katika vituo vya taksi wakisikiliza matangazo kupitia radio waliduwaa baada ya kusikia jina la Chenge likitajwa kuwamo katika baraza jipya.
Elias Mhegera mkazi wa jijini Mwanza alisema pamoja na kupunguzwa kwa baraza hilo, bado hajafurahishwa na uteuzi wa Chenge kwa kile alichodai kuwa ni mtu asiye makini kwa vile amekuwa akihusishwa na kashfa za ufisadi na kutajwa kila mara.
Alisema kuwa Chenge wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye aliyeishauri vibaya serikali na hatimaye kupitisha sheria ya takrima, na ile ya kuzuia wagombea kupinga matokeo ya uchaguzi mpaka wamelipa Sh5 milioni mahakamani.
�Sidhani kama Chenge ni mtu mzuri sana mpaka astahili kubaki katika baraza hilo, kwanza tukumbuke ndiye aliyeanzisha sheria ya takrima, pia alitunga na kupitisha sheria ambayo ilikuwa inazuia wagombea kufungua kesi wanaposhindwa uchaguzi mpaka walipe Sh5 milioni, ambayo ilifutwa baada ya kukatwa rufani Mahakama Kuu katika kesi ya Julius Ndyanabo,� alieleza. ��
Haa hivyo, baadhi ya wananchi walishangilia kuwepo kwa mawaziri wawili kutoka mkaoni Mwanza ( Laurence Masha na Ngeleja) huku wengine wakishangilia kuenguliwa kwa Diallo.
Walisema wamefurahisha na uteuzi huo ambao umeonekana kuzingatia kauli yake ya kuwaengua baadhi ya mawaziri ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakijihusisha zaidi na biashara pamoja na kutajwa katika kashfa mbalimbali za ufisadi.
Mohamed Moledina ambaye Mfanyabiashara jijini Mwanza, alisema kwa wastani ni baraza zuri na kwamba limezingatia damu changa pamoja na wasomi.
�Nimefurahisha na uteuzi huo, ametuonyesha kwamba anania kwani tuliodhani hawastaili pia amewatema, kikubwa sasa tunangoja utendaji kazi wao tu maana kuteua ni jambo moja na kutimiza matakwa ya wananchi,� alieleza.
Jane Fabian (Mfanyakazi sekta ya Umma) alisema kuwa amefurahisha na uteuzi huo kwa vile unatoa sura ya kuwa rais ni makini kwa kuteua watu makini na kuepuka wafanyabiashara kama alivyotamka katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita.��
Jijini Arusha, Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), wilaya ya Arusha.
Lazaro alidai kuwa kambi ya upinzani inashangazwa na uamuzi wa kumrejesha Chenge ambaye anadaiwa kuhusika kwenye mikataba mibovu wakati wa serikali ya Awamu ya Tatu.
Mkazi wa mjini Morogoro, Rolland Leonard alisema anachompongeza Rais Kikwete kwa kuwapunguza mawaziri waliokuwa wazee lakini alidai kuwa hakurudhishwa na� uteuzi wa mawaziri Chenge na Steven Wassira.
Naye Leonard ambaye ni mmiliki wa duka la dawa baridi la Holland alisema kuwa kurudishwa kwa baadhi ya mawaziri wasiowaadilifu ni kinyume na matarajio ya watanzania walio wengi.
Nicodemas Mbilingi alisema amefurahishwa na uteuzi huo lakini alimkosoa �Rais kwa kuwateua Chenge na Juma Kapuya kwa madai kuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa wakitajwa katika kundi la mawaziri wasiofaa na pia kuwa wazee.
�Baraza safi lakini sijafurahishwa na uteuzi wa Chenge, huyu alitajwa katika masuala ya ufisadi, alitakiwa ajisafishe kwanza na kwa upande wa kapuya nadhani ni waziri ambaye alistaili kupumzika na kuwaachia vijana kwani hana jipya. Hapa nadhani rais hajawatendea haki wananchi,� alieleza.
Wakizungumza mara baada ya uteuzi huo, wakazi mbali mbali wa manispaa ya Arusha walipongeza uteuzi huo ambao umeendelea kuwabakiza mawaziri wawili toka mkoa wa Arusha, Dk Batilda Burian, Wizara ya Mazingira na Jeremiah Sumari ambye ni Naibu Waziri wa Fedha.
Geso Bajuta ambaye ni mfugaji maarufu mkoani hapa na Mkurugenzi wa maduka ya madawa ya mifugo ya Bajuta Agrovet, alisema sasa wana imani kuwa matatizo ya wafugaji yatapatiwa ufumbuzi.
"Sisi wafugaji tunampongeza sana rais kumtea Magufuli wengi wanamjua na sasa tunaamini tutakuwa naye� kushughulikia matatizo ya wafugaji," alisema.
Mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite, Rahim Massawe alipongeza mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini na kuamini kuwa matatizo ya wachimbaji wadogo yatapatiwa ufumbuzi.
Katibu wa wazazi wa shule ya Arusha Sekondari, Michael Sanga alipongeza sana Profesa Jumanne Maghembe kuteuliwa katika Wizara ya Elimu� na Profesa Peter Msola kuwa Wizara ya Kilimo na Ushirika.
Nicholaus Minja ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Biq Expedition Ltd ya Arusha pia alipongeza Wizara ya Utalii kupata mawaziri wapya
Naye Aristos Nikitas wa Morogoro alisema kuwa anampongeza raisi Kikwete kwa kufanya kile wananchi hasa kwa kulipa kipaumbele sula la kilimo cha umwagiliaji kwani wakulima walio wengi walikuwa wakikatishwa tamaa mfumo mbaya wa kilimo.
�Sisi wakulima tulikuwa nyuma sana nahisi tulisahaulika kabisa na serikali lakini kwa hili nampongeza sana raisi kwa kuwakumbuka wakulima hasa katika suala la umwagiliaji sasa nchi itakuwa kiuchumi kutokana na kilimo hicho cha umwagiliaji,� alisema.
�
Kwa upande wao Farida Msemwa, Alfred Samuel na Said Mkwinda waliwataka mawaziri walioteuliwa kufanya kazi kwa umakini zaidi na si kwa faida yao binafsi kwani dhamana waliokabidhiwa na rais ni kubwa.
Naye Alfred Samuel alisema kuwa hakuridhishwa na wizara aliyopewa Magufuli kwani alistahili wizara nyeti ili aweze kuwafichua watendaji wazembe.
�Kwa upande wangu sijaridhika kabisa na Magufuli kuwekwa wizara hiyo, alitakiwa kuwekwa wizara kama Miundombinu, Maliasili au hata angerudi Ardhi, ndizo wizara zinazomfaa hivyo kwa hilo rais hajatutendea haki watanzania ,� alisema Samuel.
Mji wa Moshi na vitongoji vyake jana jioni ulirindima kwa hoi hoi na vifijo baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza Baraza lake la Mawaziri ambapo baadhi ya wananchi, hususan wazee walisema 'Mwalimu Nyerere amefufuka'
"Huyu Rais Kikwete kwa kweli Mungu amjalie, tunadhani Baraza hili ameliunda kwa maelekezo ya hayati Baba wa Taifa, mwalimu Nyerere. Kwa kifupi ni baraza zuri tuliombee kwa Mungu, "alisema Ally Iddi mkazi wa Maili Sita.
Katika mgahawa mmoja ambapo umati wa wananchi ulikusanyika wakimtazama na kumsikiliza Rais akitaja safu ya mawaziri walishangiliwa kwa nguvu zote hususan waliposikia majina mapya.
Mwalimu mstaafu, Macsteven Mully mkazi wa Kijiji cha Chekereni amefurahishwa na uamuzi wa Rais wa kuboresha zaidi sekta ya elimu kwa kuweka maafisa elimu wa sekondari na shule za msingi kwenye wilaya.
Kwa upande wa aliyekuwa Waziri wa fedha, Zakhia Meghji, wananchi wengi wameiambia Mwananchi kuwa, waziri huyo alipaswa kuachia ngazi mapema kwa madai kuwa alishindwa kuiongoza wizara hiyo kwa muda wote aliokuwepo.
Mchungaji mmoja wa Kanisa la Kiiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT) Dayosisi ya Kaskazini, ambaye hakupenda kuandikwa jina lake, alilazimika kuendesha misa fupi katikati ya mji kuliombea baraza hilo la mawaziri na kumtakia afya njema Rais Kikwete.
Jijini Dar es Salaam watu walikusanyika katika vikundi mbalimbali katika mitaa ya kati kati ya jiji wakifuatilia kwa makini uteuzi wa mawaziri wapya katika baraza la mawaziri.
Watu haowalionekana wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete katika redio ndani ya magari ya serikali na binafsi na wengine katika redio ndogo za mkononi na wengine wakifuatilia kupitia katika redio zilizounganishwa katika simu zao za mkononi.
Kutokana na hali hiyo katika ofisi binafsi na zile za serikali walilazimika kuacha kufanya kazi zao za kila siku kwa muda na kwenda kusikiliza kutangazwa kwa baraza hilo.
Baadhi ya wananchi walionekana kufurahishwa na jinsi Rais Kikwete alivyounda upya baraza hilo na hasa hatua ya kupunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka mawaziri 61 hadi mawaziri 47.
Katika hatua nyingine, wafanyakazi wa Idara ya Uvuvi wameelezea kustushwa na wasiwasi wa kufanya kazi chini ya Waziri John Magufuli aliyeteuliwa jana kuwa waziri wa wizara hiyo.
Wakizungumza mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza Baraza lake jipya la mawaziri jana jioni, wafanyakazi hao walisema kutokana na utendaji kazi wa Waziri Magufuli watakuwa na wakati mgumu.
�Hivi kweli tutapona hapa kweli, � alisika akihoji mfanyakazi mmoja wa idara hiyo aliyekuwa akifuatilia hotuba hiyo ya Rais Kikwete ya kuunda baraza jipya.
�Kwa kweli hapa sasa tumekwisha yaani tunakuwa na Magufuli, hii ni balaa,� aliunga mkono mfanyakazi mwingine wa idara hiyo.
Mfanyakazi mwingine wa idara hiyo ambaye hakutaja jina lake alielezea kufurahishwa na hatua ya Rais Kikwete kuihamisha idara hiyo kutoka wizara ya Malia Asili na Utalii na kuiunganisha katika wizara ya Maendeleo ya Mifugo.
Waziri Magufuli ni miongoni mwa mawaziri waliojizolea sifa kubwa za uchapakazi,hasa katika serikali ya awamu ya tatu chini Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa,wakati huo akiwa Waziri wa Ujenzi.
Akiwa katika wizara hiyo Magufuli alionekana kuwa mwiba mchungu kwa watendaji wa serikali na kuweza kuwezesha kufanikisha ujenzi wa barabara nyingi,kazi ambayo bado inakumbukwa na Watanzania wengi.
Habari hii imeandikwa na Mussa Juma (Arusha), Lillian Lucas (Morogoro), Ally Sonda (Moshi), Frederick Katulanda (Mwanza) na James Magai (Dar es Salaam).