Koba, unachobisha ni kipi hasa? Mfano mdogo ameshakupa YN, sasa unataka nini tena? Evidence is always both qualitatively and quantitatively attribiutable! Sisi tuliopo katika career hii ya elimu ya juu tunajua na wenzetu wakenya na waganda wanajua hivyo kwamba sisi kwenye mambo ya academics tupo juu. Na hapa sisi tunaongelea ubora wa elimu, sio wingi. Kwa wingi ni sawa wametuzidi kama vile ambavyo wametuzidi kila kitu katika wingi isipokuwa idadi ya watu. Ukiacha hiyo data aliyokupa YN, sisi tuna PhD holders wengi kuliko wao, tuna academic journals nyingi kuliko wao, tupo cited zaidi kwenye international journals kuliko wao, our standing in intenational academic fora ipo juu kuliko wao, tuna mitaala bora kuliko wao, you mention every aspect of quality higher education tunawazidi. Unapokuja kwenye academics kupata kazi katika international scientific organisations sisi tupo juu, ndio hao akina Tibaijuka, Mgongo, Lipumba et al wanatuwakilisha. Isipokuwa inapokuja kwenye kazi za kupitia mlango wa nyuma tupo nyuma kwa sababu watanzania sio kasumba yetu kutafuta vitu ambavyo hatuna sifa nazo. Sasa wewe umeng'ang'ania idadi ya mavyuo, wenzako wanapopima ubora wa vyuo hawahesabu idadi ya vyuo wanaangalia quality, na quality inapimwa kwa knowledge production and intellectual contribution-na hivi vitu vinaangaliwa kwa vigezo kama vya hapo juu.
Ni kweli watz tu wanyonge katika mambo kibao, lakini sio hili la ubora wa elimu ya juu, hili hapana. Pale tunapofanya vizuri kidogo tusisite kusema na kujipongeza. Waswahili wanasema "You cannot be inferior unless you feel that you are inferior"!
Mkuu Kitila,
Kama msomi hapo juu naona unakosea. Unalinganisha nyanya na maembe, wakati unapolinganisha vitu inatakiwa ulinganishe vinavyofanana kwa mfano wangu hapo juu nyanya kwa nyanya.
Ukilinganisha ubora wa UD inatakiwa ulinganishe na chuo kingine Kenya au Uganda.
Ninapoona unakosea ni pale unapochukulia ubora wa UD kama kiwakilishi cha Tanzania nzima na kutokuwa bora kwa chuo kimoja kenya kama weakness ya Kenya nzima.
Kwasababu unaongela nchi mbili basi lazima uende deep zaidi na kuangalia sio
UD ni wa ngapi kwenye ranking ukilinganisha na vyuo vya Kenya bali ulinganishe value inayoletwa na hawa graduates wa Tanzania kwa kulinganisha na Kenya.
Tanzania tuna vyuo vichache sana na mpaka sasa vyuo ambavyo wanaofaulu wanaenda kwa mapenzi yao ni UDSM, Muhimbili na Sokoine. Vingine mara nyingi
inakuwa second choice (ingawaje kuna wanafunzi wachache ambao wanaenda huko kama first choice). Sasa kama una pool la wanafunzi laki moja, unatakiwa kuchagua wanafunzi 1000, ni lazima utapata wanafunzi wazuri, maana mchujo unaondoa wale wote ambao ni weak. Hivyo hivyo kwa walimu, matokeo yake UDSM kinakuwa chuo bora zaidi.
Kama unazungumzia ubora wa elimu ya Kenya na Tanzania, basi lazima uwahusishe wale wanafunzi bora toka vyuo mbalimbali vya Kenya na kulinganisha na vile vya Tanzania.
Tatizo ninaloliona hapa, tunalinganisha kwa kutumia vitu viwili ambavyo hata siku moja haviwezi kufanana.
Ni sawa na mwandishi anayesema Mbeya yaongoza kwasababu tu ya ST. Francis wakati kuna mikoa mingine ina shule nyingi za wanafunzi waliofaulu vizuri hasa ukilinganisha na mazingira ya ST.Francis kwamba inachukua wakali wa nchi nzima.