Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Ikitokea tulia akagoma kuwafukuza itakuwaje

Tatizo mnakuwa wagumu kuelewa chadema haina shida wenyewe kuwa wabunge bali imewafuta Kwenye list ya Wanachama wake. Kama Tulia ataendelea kuwatambua aendelee lakini ajue wale sio Wanachama wa Chadema na chadema haina mbunge wa viti maalum bungeni. Waendelee kula pesa ya serikali ya vilaza wasio jitambua.
 
Faida ya kwanza ni kuonekana ni chama kinachosimamia katiba na itikadi zao ukizikiuka hata kama ni Tundu Lissu unafukuzwa!

Mzee Mdee na wenzake kuna mahala wameandaliwa ngoja uone wanakoenda
Mzee Mdee ni yupi?
 
Tokea jana katika kikao cha CHADEMA walifika wabunge 19 ambao kulikuwa na mzozo nani aliyewapa baraka wakati hakuna makubaliano.

Kitu ambacho tunaweza kushangaa kule bungeni hawata vuliwa na mwisho wa siku watapokelewa juu kwa juu wataingia ccm na watabaki kuwa bunge.

Hii topic msipuuze
 
Hakuna Cha Kushangaza hapo...Sakosi nyingi huwa Zinaendeshwa hivyo....!

Wakatafute Vyama Sasa na Sio Sakosi..!
 
Mimi nakushauri ujifunze kuandika kiswahili vizuri....mfano [waliwofukuzwa=waliofukuzwa]. Asante
 
Asa yale magwanda watapeleka wapi 😂😂😂
Inasikitisha! Lakini Maamuzi yaliyofanyika ni ya busara sana kwani yatakifanya chama kiwe na nidhamu ya hali ya juu sana. Kama kwerli hao covid-19 ni wanachadema kweli, bado kuna room ya kuludi chamani. Ni kuomba upya uwanachama
 
Mkuu hela huwa hazitoshi siku zote!!tena kama ulishawahi kuwa mbunge kwenye pesa za bure huko, ukitemeshwa hata kama umebakiza mwezi mmoja tu, lazima uumie tu, wapi utapata malipo ya milioni 12 kwa mwezi, hata ukiwa na elimu ya std seven?prof.mwenyewe hafiki huko.

Na kwa siasa za sasa hata kuhamia ccm ni ngumu, ili kupata vyeo kama wakati wa jiwe.Mama ana mapungufu yake kama kiongozi yoyote lakini ametutoa jehanamu ya siasa.MUNGU FUNDI.
 
Mimi nashauri waombe upya uanachama waendelee kubaki CDM! Wakienda huko kwenye vyama vingine watapotea kabisa katika ulimwengu wa siasa za nchi yetu.
Wabaki na kuomba uanachama upya, Watanzania na hususani Wana CDM watawaelewa wakiomba radhi kufuatia siasa za chuki visasi Mwendazake.
 
Kuna mbweha alisema atajitoa jamiiforum kama chadema watawafukuza covid-19.
britanicca yan huyu jamaa tangu Magufuli Afe na tangu Urusi avamie Ukraine amekua mjinga kwel kwel humu jukwaan ..kapoteza heshima yake kwel kwel kutokana nambo anayosimamia..Haya sasa ngoja tuone atafanyaje.

Pascal Mayalla naye sijui anasema nini kuhusu hil maana amekua akiamin jambo la covid19 lina baraka ya mwenyekit na kamati kuu...Mara kangaroo cort na mambo mengine meengi
 
Mkuu, unaweza kunieleza kufukuzwa kwa hao wanachama kuna faida gani kwa chadema?
usaliti kwa chama hautakiwi na imani kwa wanachama juu ya maumivu waliokuwanayo unapozeka sasa. Safi sana.
 
Wasaliti kama Hawa sijui hata watoto wao watajifunza nini!? Halima ulikamata kura feki ukathibitishia Dunia uchaguzi ulikuwa feki, iweje Tena uwe sehemu ya uchafu huo
 
Safi sn waende CCM au ACT wasaliti wakubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…