Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Hata hivyo walisha kula sana; mwaka mzima? Naona kama ama watahamia ama ACT Wazalendo au CCM. Kokote watakokokwenda nadhani watakuwa na nyota inayong'ara kwani ndio watakaoutumika kukibomoa CHADEMA. Labbda washawishiwe wasiondoke ndani ya Chama.
Yani kina Slaa na Zitto washindwe kuibomoa CHADEMA ndo hizo Covid kumi na tisa ziweze? Duh! Think again. Maana hizo ni “wishful thinking”.
 
1. Point yako ya pili ndio ya msingi kwa hakina mama, CDM awawezi wavua ubunge wanachoweza washafanya kuwavua uanachama na kukosa sifa za kuwa wabunge.

Maana yake hakina mama awawezi kwenda mahakamani kutetea kuvuliwa ubunge wanachoweza kutetea uanachama wao ili wabaki na sifa za kuwa wabunge.

So kesi yao ni unfair dismissal ya kuvuliwa uanachama na mfumo dume kwa njia za uonevu.

2. Iwapo kesi ya wamama ya kufukuzwa uanachama itachukua muda na kufanya waendelee kubaki na sifa za kuwa wabunge. CDM nao wanaweza fungua kesi tofauti ya kutaka kufutwa ubunge wao kwa kufoji sign. Hiyo sasa inakuwa ni kesi nyingine aina uhusiano na kesi ya wamama ya unfair dismissal kwenye uanachama wao.

In their defence kwenye kesi ya kufoji sign hakina mama wanaweza kubali kosa na kujitetea iliwalizimu kufanya hivyo kwa sababu wapiga sign ni wanaume ambao wanawapangia cha kufanya katika nafasi za wanawake bungeni zilizotolewa kisheria.

Ukiitazama kwa kina ni kesi ya ukandamizaji kwa sababu wengi ya hawa wabunge wa viti maalum walikuwa viongozi wa BAWACHA so ni maamuzi yao kuchukua hizo nafasi, especially CDM wakijichuza kupeleka majina mapya inawajengea hoja ya ukandamizaji zaidi hizo nafasi mpaka mwenyekiti na kundi lake waamue lakini sio Democratic decision za viongozi wa BAWACHA.

3. Lakini uwezi kuingiza mambo ya kufoji sign na shenanigans zingine za kupata nafasi za ubunge katika kesi number moja ya unfair dismissal ni vitu viwili tofauti.
 
Sasa Uhuni wa Chama Uko wapi Hapo??
 
Wakina mama Gani wananyanyasika CHADEMA?? Unafahamu kwamba CHADEMA ndio ilipitisha wagombea wengi zaidi wanawake 2020? Zaidi ya majimbo 70 waliachiwa wanawake!!! In fact ndio chama pekee chenye sera ya Jinsia/wanawake!!
Hawa wanawake waliipigania mno Cdm kwenye nyakati ngumu, maadamu kila binadamu kuna wakati hufanya makosa hawakustahili adhabu ya kikatili kiasi hiki.

Kuna ambao angalau wangefikiriwa kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo wakati huo (rejea sakata la Nusrat Hanje)

Chama kinachoshindwa kuwasamehe makada wake wanapokengeuka/kukosea kwa bahati mbaya ni hatari kikishika dola (huenda kikageuka chama dola).

Anyway wenye chama wameshaamua ni vyema wakajiunge na vyama vingine kama Ccm au Act.
JokaKuu Nguruvi3 Tindo Pascal Mayalla jmushi1
lwaitama1
 
[emoji23][emoji23]dah
 
Mahakama ya nini sheria ipo wazi mtu akikoma kua mwanachama wa chama cha siasa ubunge wake una koma immediately?!
 
Hiyo ndiyo maana ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO uwazi na ukweli.
 
Adhabu ya msaliti popote pale duniani ni kuangamizwa. Covid 19 wanapaswa kuangamizwa milele kisiasa.
 
Kuna watu humu JF wana upeo mdogo sana. Mtu anajenga hoja eti wakina mdee walipaswa wasamehewe au wasipewe hiyo adhabu, wakati ukweli ni huu.

1. Kikao cha jana kilikuwa ni kusikiliza rufaa zao walizozikata kupinga maamuzi ya kamati kuu ya kuwavua uanachama. Agenda ya kuwasamehe inatokea wapi?

2. Mpaka kikao cha jana kinafanyika, Covid 19 walikuwa wanajiona wako sahihi na wamekuja kupambana na CHADEMA. Hawakuwahi kuomba msamaha na hawakuona umuhimu huo. Msamaha unawezaje kutokea katika mazingira hayo?

3. CHADEMA ni chama kinachongozwa kwa misingi ya katiba, na uhuni uliofanywa na akina mdee na genge lake hauwezi kuvumilika hata kidogo chini ya Katiba ya CHADEMA. Unawezaje kutoa msamaha kwa wahuni?
 
Wanabodi.

hili ni bandiko la swali "Je Wabunge 19 wa Chadema Walijiteau?. Je CC-ya Chadema ni Kangaroo Court?. Je Baraza Kuu Litabariki Ukangaroo Ule?. Likibariki, Karma Itawatafuna!"
Nawatakia wana Chadema, kikao chema cha Baraza Kuu.

Paskali
Kikao cha Baraza Kuu Chadema, kimemalizika, limebariki ule Ukangaroo uliofanywa na CC ya Chadema, uamuzi wa Baraza Kuu Chadema ni uamuzi wa mwisho, final and conclusive. Sijasikia popote juhudi zozote za kumtafuta aliyesaini barua ya uteuzi, sijasikia popote Chadema wakisema kuna forgery au kuripoti popote forgery ile, hivyo hoja za bandiko hili zinasimama, wabunge hao 19 wa Chadema, hawakujiteua wenyewe, waliteuliwa na kiongozi wa Chadema aliyesaini barua yao ya uteuzi!. Hakuna forgery yoyote iliyofanywa kwenye uteuzi wao ndio maana Chadema hawajaripoti forgery popote!.

Tena kiukweli, Halima Mdee ni mwanamke wa shoka kweli kweli nilidhani mbele vya kikao cha Baraza Kuu Chadema angesimama na kuyasema ukweli wa barua yao ya uteuzi, wajumbe wangebaki midomo wazi!.

Kama it's a battle, kina Halima have lost the battle, they have nothing more to loose au ni kukubali kufa kikondoo kwa kuisubiria karma iwalipie, au to keep on fighting hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike kwa kuhamishia mpambano kwenye wiwanja vingine vya Kisheria!.

Halima anamjua aliowasainia barua ya uteuzi, ili kumlinda, waliamua kunyamaza kwa imani kuwa atawaombea msamaha, kumbe... kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.

Life goes on
P
 
Hakuna hali tete. CHADEMA wameshamaliza kazi. Mambo ya ubunge hayawahusu wala hawana hoja huko. Ni juu ya wananchi wote kukereka na jinsi katiba na rasilimali zao zinavyochezewa na watawala kwa maslahi binafsi. Bunge linaweza kufanya linavyotaka au kama linavyoagizwa na wenye mamlaka.

Kuhusu mahakama, mambo yako wazi. Ushahidi wote wa shauri hili uko kwenye taasisi husika. Kama mahakama ina nia ya kutenda haki ni suala la kumalizwa kwa muda usiozidi mwezi. Tatizo experience imedhihirisha kuwa mahakama na bunge wanafanya kazi kwa maagizo ya serikali (executive, specifically, Rais). Hapo sasa inategemea integrity ya Rais: anataka katiba na uhuru wa mahakama na bunge viheshimiwe au la?
 
Hakina mama ×
Akina mama✓

Awaruhusiwi×
Hawaruhusiwi✓

Aikubaliki×
Haikubaliki✓

Ata×
Hata✓

Ulisoma ile ilikuwa inaitwa EWW?
 
Yoote uliyo eleza sawa vp huyo binti aliekua gerezani alitolewa na nani?
 

Unasamehewa kwa kukiri kosa na kuomba msamaha. Sio unajua umekosea kisha unashupaza shingo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…