Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Hata hivyo walisha kula sana; mwaka mzima? Naona kama ama watahamia ama ACT Wazalendo au CCM. Kokote watakokokwenda nadhani watakuwa na nyota inayong'ara kwani ndio watakaoutumika kukibomoa CHADEMA. Labbda washawishiwe wasiondoke ndani ya Chama.
Yani kina Slaa na Zitto washindwe kuibomoa CHADEMA ndo hizo Covid kumi na tisa ziweze? Duh! Think again. Maana hizo ni “wishful thinking”.
 
1. Mkuu charge sheet si utasema umevuliwa "ubunge" kimakosa. Sasa mawakili wa upinzani wanaweka zuio kwamba kesi ya msingi isisikilizwe kwa sababu hao wanaoleta madai hawakuwa "wabunge Viti Maalum" wa CHADEMA kwa definition Ile ya kisheria (Uteuzi wa Kamati kuu, barua ya Katibu Mkuu n.k)

2. Otherwise hata wakishinda kesi hiyo haina impact sababu Kamati kuu imewavua uanachama sio ubunge. So wakienda bungeni wakiulizwa wanadhaminiwa na chama Gani ndio mchezo umekwisha hapo.

3. Wakina mama Gani wananyanyasika CHADEMA?? Unafahamu kwamba CHADEMA ndio ilipitisha wagombea wengi zaidi wanawake 2020? Zaidi ya majimbo 70 waliachiwa wanawake!!! In fact ndio chama pekee chenye sera ya Jinsia/wanawake!!

4. Wanaume Gani wanaamua?? Sheria za nchi lazima zifuatwe otherwise katiba itambue women wings za vyama ndio vipitishe viti maalum ila kusema eti wanaume mpaka waamue unakosea!! Issue pale ni katiba za vyama sio kelele zingine za feminism hapa!!

Mkiambiwa katiba mpya hamtaki afu mkibanwa ndio mnalialia kuwa Sheria ni kandamizi!!!
1. Point yako ya pili ndio ya msingi kwa hakina mama, CDM awawezi wavua ubunge wanachoweza washafanya kuwavua uanachama na kukosa sifa za kuwa wabunge.

Maana yake hakina mama awawezi kwenda mahakamani kutetea kuvuliwa ubunge wanachoweza kutetea uanachama wao ili wabaki na sifa za kuwa wabunge.

So kesi yao ni unfair dismissal ya kuvuliwa uanachama na mfumo dume kwa njia za uonevu.

2. Iwapo kesi ya wamama ya kufukuzwa uanachama itachukua muda na kufanya waendelee kubaki na sifa za kuwa wabunge. CDM nao wanaweza fungua kesi tofauti ya kutaka kufutwa ubunge wao kwa kufoji sign. Hiyo sasa inakuwa ni kesi nyingine aina uhusiano na kesi ya wamama ya unfair dismissal kwenye uanachama wao.

In their defence kwenye kesi ya kufoji sign hakina mama wanaweza kubali kosa na kujitetea iliwalizimu kufanya hivyo kwa sababu wapiga sign ni wanaume ambao wanawapangia cha kufanya katika nafasi za wanawake bungeni zilizotolewa kisheria.

Ukiitazama kwa kina ni kesi ya ukandamizaji kwa sababu wengi ya hawa wabunge wa viti maalum walikuwa viongozi wa BAWACHA so ni maamuzi yao kuchukua hizo nafasi, especially CDM wakijichuza kupeleka majina mapya inawajengea hoja ya ukandamizaji zaidi hizo nafasi mpaka mwenyekiti na kundi lake waamue lakini sio Democratic decision za viongozi wa BAWACHA.

3. Lakini uwezi kuingiza mambo ya kufoji sign na shenanigans zingine za kupata nafasi za ubunge katika kesi number moja ya unfair dismissal ni vitu viwili tofauti.
 
HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAFUKUZWA RASMI CHADEMA

Baraza Kuu la #CHADEMA limezitupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 wakipinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge wa Viti Maalumu bila baraka za chama
======
UPDATE:

Halima Mdee: Kilichofanyika ni Uhuni, hata Mbowe (Freeman) mwenyewe anajua

John Mrema: Baada ya uamuzi wa Baraza Kuu, Katibu Mkuu ataandika barua kumuarifu Spika kuwa suala lao limehitimishwa; tutamwachia spika afanye uamuzi kama alivyosema anasubiri Rufaa zao
=======

Matokeo ni kama ifuatavyo;

Kanda ya Victoria (Wajumbe 44)
-Wanaokubalia wavuliwe uwanachama 42
-Wasiokubali 1
-Wasiofungamana na Upande wowote 1
Jumla kura 44

Kanda ya Nyasa (Wajumbe 57)

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 57
-Wasiokubalina 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 57

Kanda ya Unguja (Wajumbe 22)

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 19
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 1
Jumla ya Kura 22

Kanda ya Pemba 15
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 12
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 2
Jumla ya Kura 15

Kanda ya Kusini 32

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 32
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 32

Kanda ya Pwani 47

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 45
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 2
Jumla ya Kura 47

Kanda ya Kati 44

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 44
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 44

Kanda ya Serengeti Wajumbe 41

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 41
-Wasiokubalina 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 41

Kanda ya Magharib Wajumbe 37

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 37
Wasiokubali 0
Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 37

Kanda ya Kaskazini Wajumbe 61

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 61
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 61

MATOKEO YA JUMLA

Idadi ya wajumbe 423

Waliokubalina na maamuzi ya Kamati ya kuwafukuza Uanachama ni 413 sawa 97.6%

Wasiokubaliana na uamuzi wa Kamati kuu ni 5 sawa na 1.2%

Wasiofungamana na upande wowote ni 5 sawa na 1.2%

Pia, soma;

1). BAVICHA: Tumesikitishwa sana na walioenda kuapa, ni kitendo cha usaliti, hujuma na hakiwezi kuvumilika. Wataka hatua kali zichukuliwe

2. Uchaguzi 2020 - CHADEMA yaitaka Tume ya Uchaguzi NEC kutoa Ufafanuzi kuhusu Majina ya Wabunge wa Viti Maalum Wanaodaiwa wamepelekwa Bungeni

3). Mnyika: Ni miezi 5 sasa NEC hawajajibu barua yangu kuhusu walikopata majina ya Wabunge 19 na nani amesaini fomu zao

4). Uchaguzi 2020 - Hatimaye Wabunge wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

5. Uchaguzi 2020 - Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

6. Spika Ndugai: Wabunge waliofukuzwa CHADEMA wapo kwenye mikono salama

7. Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni UHUNI!
Sasa Uhuni wa Chama Uko wapi Hapo??
 
Wakina mama Gani wananyanyasika CHADEMA?? Unafahamu kwamba CHADEMA ndio ilipitisha wagombea wengi zaidi wanawake 2020? Zaidi ya majimbo 70 waliachiwa wanawake!!! In fact ndio chama pekee chenye sera ya Jinsia/wanawake!!
Hawa wanawake waliipigania mno Cdm kwenye nyakati ngumu, maadamu kila binadamu kuna wakati hufanya makosa hawakustahili adhabu ya kikatili kiasi hiki.

Kuna ambao angalau wangefikiriwa kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo wakati huo (rejea sakata la Nusrat Hanje)

Chama kinachoshindwa kuwasamehe makada wake wanapokengeuka/kukosea kwa bahati mbaya ni hatari kikishika dola (huenda kikageuka chama dola).

Anyway wenye chama wameshaamua ni vyema wakajiunge na vyama vingine kama Ccm au Act.
JokaKuu Nguruvi3 Tindo Pascal Mayalla jmushi1
lwaitama1
 
Remmy Ongala Song ,Tititinti tiriri,,,,Kifoooo kifo ,kifo hakina hurumaaaaa tititinti tiririri.....X 2.
Kifooo kifo ,tulikuwa na baba yetu tulikuwa tunamtegemea,kifo umechukua baba yetu leo tunakwenda tunahangaika,hatuna mahali pa kulala........[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
[emoji23][emoji23]dah
 
hali bado ni tete.wabunge hao wataendelea kuwa bungeni kwa sababu naamini wataenda mahakamni kudai haki yao na ninavyojua mahakama itachukua muda mrefu kufanya maamuzi ya jambo hili sababu linahitaji vielelezo ya kutosha ili kufikia maamuzi.kuna technicality kwa pande zote mbili hivyo busara itabidi utumike ili kufikia hitimisho la jambo hilo.nina amini spika kwa kuwa pia ni mtalaamu wa mambo ya sheria hatakurupuka katika maamuzi yake.Tusubiri time will tell.
# I contemplate conteplatinng#
Mahakama ya nini sheria ipo wazi mtu akikoma kua mwanachama wa chama cha siasa ubunge wake una koma immediately?!
 
Hiyo ndiyo maana ya CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO uwazi na ukweli.
 
Hawa wanawake waliipigania mno Cdm kwenye nyakati ngumu, maadamu kila binadamu kuna wakati hufanya makosa hawakustahili adhabu ya kikatili kiasi hiki.

Kuna ambao angalau wangefikiriwa kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo wakati huo (rejea sakata la Nusrat Hanje)

Chama kinachoshindwa kuwasamehe makada wake wanapokengeuka/kukosea kwa bahati mbaya ni hatari kikishika dola (huenda kikageuka chama dola).

Anyway wenye chama wameshaamua ni vyema wakajiunge na vyama vingine kama Ccm au Act.
JokaKuu Nguruvi3 Tindo Pascal Mayalla jmushi1
lwaitama1
Adhabu ya msaliti popote pale duniani ni kuangamizwa. Covid 19 wanapaswa kuangamizwa milele kisiasa.
 
Kuna watu humu JF wana upeo mdogo sana. Mtu anajenga hoja eti wakina mdee walipaswa wasamehewe au wasipewe hiyo adhabu, wakati ukweli ni huu.

1. Kikao cha jana kilikuwa ni kusikiliza rufaa zao walizozikata kupinga maamuzi ya kamati kuu ya kuwavua uanachama. Agenda ya kuwasamehe inatokea wapi?

2. Mpaka kikao cha jana kinafanyika, Covid 19 walikuwa wanajiona wako sahihi na wamekuja kupambana na CHADEMA. Hawakuwahi kuomba msamaha na hawakuona umuhimu huo. Msamaha unawezaje kutokea katika mazingira hayo?

3. CHADEMA ni chama kinachongozwa kwa misingi ya katiba, na uhuni uliofanywa na akina mdee na genge lake hauwezi kuvumilika hata kidogo chini ya Katiba ya CHADEMA. Unawezaje kutoa msamaha kwa wahuni?
 
Hawa wanawake waliipigania mno Cdm kwenye nyakati ngumu, maadamu kila binadamu kuna wakati hufanya makosa hawakustahili adhabu ya kikatili kiasi hiki.

Kuna ambao angalau wangefikiriwa kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo wakati huo (rejea sakata la Nusrat Hanje)

Chama kinachoshindwa kuwasamehe makada wake wanapokengeuka/kukosea kwa bahati mbaya ni hatari kikishika dola (huenda kikageuka chama dola).

Anyway wenye chama wameshaamua ni vyema wakajiunge na vyama vingine kama Ccm au Act.
JokaKuu Nguruvi3 Tindo Pascal Mayalla jmushi1
lwaitama1
Wanabodi.

hili ni bandiko la swali "Je Wabunge 19 wa Chadema Walijiteau?. Je CC-ya Chadema ni Kangaroo Court?. Je Baraza Kuu Litabariki Ukangaroo Ule?. Likibariki, Karma Itawatafuna!"
Nawatakia wana Chadema, kikao chema cha Baraza Kuu.

Paskali
Kikao cha Baraza Kuu Chadema, kimemalizika, limebariki ule Ukangaroo uliofanywa na CC ya Chadema, uamuzi wa Baraza Kuu Chadema ni uamuzi wa mwisho, final and conclusive. Sijasikia popote juhudi zozote za kumtafuta aliyesaini barua ya uteuzi, sijasikia popote Chadema wakisema kuna forgery au kuripoti popote forgery ile, hivyo hoja za bandiko hili zinasimama, wabunge hao 19 wa Chadema, hawakujiteua wenyewe, waliteuliwa na kiongozi wa Chadema aliyesaini barua yao ya uteuzi!. Hakuna forgery yoyote iliyofanywa kwenye uteuzi wao ndio maana Chadema hawajaripoti forgery popote!.

Tena kiukweli, Halima Mdee ni mwanamke wa shoka kweli kweli nilidhani mbele vya kikao cha Baraza Kuu Chadema angesimama na kuyasema ukweli wa barua yao ya uteuzi, wajumbe wangebaki midomo wazi!.

Kama it's a battle, kina Halima have lost the battle, they have nothing more to loose au ni kukubali kufa kikondoo kwa kuisubiria karma iwalipie, au to keep on fighting hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike kwa kuhamishia mpambano kwenye wiwanja vingine vya Kisheria!.

Halima anamjua aliowasainia barua ya uteuzi, ili kumlinda, waliamua kunyamaza kwa imani kuwa atawaombea msamaha, kumbe... kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.

Life goes on
P
 
hali bado ni tete.wabunge hao wataendelea kuwa bungeni kwa sababu naamini wataenda mahakamni kudai haki yao na ninavyojua mahakama itachukua muda mrefu kufanya maamuzi ya jambo hili sababu linahitaji vielelezo ya kutosha ili kufikia maamuzi.kuna technicality kwa pande zote mbili hivyo busara itabidi utumike ili kufikia hitimisho la jambo hilo.nina amini spika kwa kuwa pia ni mtalaamu wa mambo ya sheria hatakurupuka katika maamuzi yake.Tusubiri time will tell.
# I contemplate conteplatinng#
Hakuna hali tete. CHADEMA wameshamaliza kazi. Mambo ya ubunge hayawahusu wala hawana hoja huko. Ni juu ya wananchi wote kukereka na jinsi katiba na rasilimali zao zinavyochezewa na watawala kwa maslahi binafsi. Bunge linaweza kufanya linavyotaka au kama linavyoagizwa na wenye mamlaka.

Kuhusu mahakama, mambo yako wazi. Ushahidi wote wa shauri hili uko kwenye taasisi husika. Kama mahakama ina nia ya kutenda haki ni suala la kumalizwa kwa muda usiozidi mwezi. Tatizo experience imedhihirisha kuwa mahakama na bunge wanafanya kazi kwa maagizo ya serikali (executive, specifically, Rais). Hapo sasa inategemea integrity ya Rais: anataka katiba na uhuru wa mahakama na bunge viheshimiwe au la?
 
Ni sawa na mimi kusema naenda kukufungulia kesi ya uonevu.

Halafu unitishie tukifika mahakamani utawaambia nilienda kuchukua mkopo bank kwa kufoji saini yako.

Ni vitu viwili tofauti, kesi yako ni nyingine uzuiwi kwenda kunifungulia mashtaka ya kufoji signature yako; lakini accusation zako hazina uhusiano na kesi yangu ya msingi hadi mahakama wazipe maanani.

Hakina mama nchi hii wananyanyasika sana yaani awaruhusiwi kuchukua fursa mpaka wanaume waamue ata kama walipigania chama sawa kwa muda wote; huu mwenendo wa ukandamizaji wa haki za hakina mama aukabaliki dunia ya leo.

Haki ipatikane kwa wadada na wamama 19 wa CHADEMA.
Hakina mama ×
Akina mama✓

Awaruhusiwi×
Hawaruhusiwi✓

Aikubaliki×
Haikubaliki✓

Ata×
Hata✓

Ulisoma ile ilikuwa inaitwa EWW?
 
Kikao cha Baraza Kuu Chadema, kimelazika, limebariki ule Ukangaroo uliofanywa na CC ya Chadema, uamuzi wa Baraza Kuu Chadema ni uamuzi wa mwisho, final and conclusive. Sijasikia popote juhudi zozote za kumtafuta aliyesaini barua ya uteuzi, sijasikia popote Chadema wakisema kuna forgery au kuripoti popote forgery ile, hivyo hoja za bandiko hili zinasimama, wabunge hao 19 wa Chadema, hawakujiteua wenyewe, waliteuliwa na kiongozi wa Chadema aliyesaini barua yao ya uteuzi!. Hakuna forgery yoyote iliyofanywa kwenye uteuzi wao ndio maana Chadema hawajaripoti forgery popote!.

Tena kiukweli, Halima Mdee ni mwanamke wa shoka kweli kweli nilidhani mbele vya kikao cha Baraza Kuu Chadema angesimama na kuyasema ukweli wa barua yao ya uteuzi, wajumbe wangebaki midomo wazi!.

Kama it's a battle, kina Halima have lost the battle, they have nothing more to loose au ni kukubali kufa kikondoo kwa kuisubiria karma iwalipie, au to keep on fighting hadi risasi ya mwisho na tone la mwisho la damu limwagike kwa kuhamishia mpambano kwenye wiwanja vingine vya Kisheria!.

Halima anamjua aliowasainia barua ya uteuzi, ili kumlinda, waliamua kunyamaza kwa imani kuwa atawaombea msamaha, kumbe... kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.

Life goes on
P
Yoote uliyo eleza sawa vp huyo binti aliekua gerezani alitolewa na nani?
 
Hawa wanawake waliipigania mno Cdm kwenye nyakati ngumu, maadamu kila binadamu kuna wakati hufanya makosa hawakustahili adhabu ya kikatili kiasi hiki.

Kuna ambao angalau wangefikiriwa kwa kuangalia mazingira yaliyokuwepo wakati huo (rejea sakata la Nusrat Hanje)

Chama kinachoshindwa kuwasamehe makada wake wanapokengeuka/kukosea kwa bahati mbaya ni hatari kikishika dola (huenda kikageuka chama dola).

Anyway wenye chama wameshaamua ni vyema wakajiunge na vyama vingine kama Ccm au Act.
JokaKuu Nguruvi3 Tindo Pascal Mayalla jmushi1
lwaitama1

Unasamehewa kwa kukiri kosa na kuomba msamaha. Sio unajua umekosea kisha unashupaza shingo.
 
Back
Top Bottom