Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Mahakamani ingekuwa sahihi Kama ni Ubunge wa kuchaguliwa na sio wa viti maalum. Halafu mahakamani Mambo yatawekwa wazi ni jinsi gani walivyopata Ubunge ambapo itakuwa mbaya zaidi.
Mbaya zaidi kwa nani??
 
Mkuu, unaweza kunieleza kufukuzwa kwa hao wanachama kuna faida gani kwa chadema?
Kutatoa nafasi kwa CHADEMA kuteua wake, waume, watoto, na ndugu za viongozi kupewa ubunge nao wanuyfaike.
 
Zitto mwenyewe amekiri katika makosa makubwa aliyofanya katika Maisha yake ni kuondoka Chadema. Kwa huu mwaka mmoja akina Halima wamekuwa na impact gani?. Dr Slaa, Masinji etc wameshindwa kukivunja chama sembuse Hawa akina Halima Mdee waliochuja?. Waende CCM au ACT .

Umesahau wale wanawake ambao 2020 walihma chama kwa visingizio vingi, Leo wapo wapi?. Alfred Rwakatale aliyehama chadema kwa mikwara yupo wapi leo?. Chadema ilishindwa kuvunjwa na jiwe sidhani Kuna wakuivunja zaidi ya Mungu mwenyewe.
Baambie baambie Chadema ni Taasisi kubwa sana
 
Ndugai alikataa ila mwisho kaondoka yeye kwenye uspika. Sometimes tuangalie utaruhusuje mbunge asiyetakiwa na chama awe mbunge?. Maana kikatiba chama ndio kinadhamini wabunge sio spika. Tulia alishasema wazi anasubiri maelekezo kutoka kwenye chama Cha Chadema.


Ndugai alitumia njia kutoka kwenye uspika, na mpango wa haraka ukawa ni huo. Mwache apumzike ajilie maisha huku anavuta pesa ndefu bado.
 
Ndugai alitumia njia kutoka kwenye uspika, na mpango wa haraka ukawa ni huo. Mwache apumzike ajilie maisha huku anavuta pesa ndefu bado.

Usisahau aliomba msamaha kuwa asamehewe lakini msamaaha ukakataliwa. Karma ndio ilimuondoa ndugai kwenye uspika.
 
Samia anaendelea kusafisha masalia yote ya mwenda...
 
Back
Top Bottom