Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Yaani mwenyekiti atoke kuongea na mkuu wa muhimili uliojichimbia zaidi then eti mahakama?
Kwahyo maaamuzi yamefanyika kwa kufuata matakwa ya huyo mkuu wa mhimili na wala sikwa mjibu wa katiba na kanuni za chadema?? Ebu nitajie huyo mkuu wa mhimili anaweza amua mambo na kuisigina katiba na kanuni za chama
 
HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAFUKUZWA RASMI CHADEMA

Baraza Kuu la #CHADEMA limezitupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 wakipinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge wa Viti Maalumu bila baraka za chama
======
UPDATE:

View attachment 2221145

Halima Mdee: Kilichofanyika ni Uhuni, hata Mbowe (Freeman) mwenyewe anajua

John Mrema: Baada ya uamuzi wa Baraza Kuu, Katibu Mkuu ataandika barua kumuarifu Spika kuwa suala lao limehitimishwa; tutamwachia spika afanye uamuzi kama alivyosema anasubiri Rufaa zao
=======

Matokeo ni kama ifuatavyo;

Kanda ya Victoria (Wajumbe 44)
-Wanaokubalia wavuliwe uwanachama 42
-Wasiokubali 1
-Wasiofungamana na Upande wowote 1
Jumla kura 44

Kanda ya Nyasa (Wajumbe 57)

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 57
-Wasiokubalina 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 57

Kanda ya Unguja (Wajumbe 22)

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 19
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 1
Jumla ya Kura 22

Kanda ya Pemba 15
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 12
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 2
Jumla ya Kura 15

Kanda ya Kusini 32

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 32
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 32

Kanda ya Pwani 47

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 45
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 2
Jumla ya Kura 47

Kanda ya Kati 44

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 44
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 44

Kanda ya Serengeti Wajumbe 41

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 41
-Wasiokubalina 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 41

Kanda ya Magharib Wajumbe 37

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 37
Wasiokubali 0
Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 37

Kanda ya Kaskazini Wajumbe 61

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 61
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 61

Jumla ya Kura 423 zimekubaliana na Kamati Kuu na kura 5 ndo zimepingana na maamuzi ya Kamati Kuu
safi sana jambo jema lenye furaha.Chama si mtu au jina bali maamuzi ya kitaasisi.Waende wakajenge maisha mapya ktk chama kingine.Au waachane na siasa.
 
Kwani katiba ya chadema inasema rufaa ya MTU inapaswa kusikilizwa baada ya mda ganii?? Maana ni zaidi ya mwaka sasa toka rufaa hiyo imepelekwaa?? Maana isijeikaonekana kikao hicho kisijeonekana ni batiriii.
Ingekuwa kikao ni batili huyo halima na wenzie 18 wasengeshiriki
 
Acheni kuwakandamiza kwa kuwatishia wanasheria wenu kandamizi dhidi ya akinamama. Kwenda mahakamani ni haki yao. Acheni kuwatisha, etiwatulie mbeleni mtawasamehe kwa kosa lipi mpaka waombe msamahaa. Tunataka sheria ichunguze na itoe hakiii
Mbona unateseka sana dogo? Muulize Sophia Simba na Membe watakuelimisha vizuri kuhusu hili.
 
Bunge ndo litaamua....sheria za Tanzania zina gaps nyingi. Hapo Tulia Mwansasu ashapata kipengele cha kuwalinda kabla hata ya hilo Baraza lao kukaa
 
Acheni kuwakandamiza kwa kuwatishia wanasheria wenu kandamizi dhidi ya akinamama. Kwenda mahakamani ni haki yao. Acheni kuwatisha, etiwatulie mbeleni mtawasamehe kwa kosa lipi mpaka waombe msamahaa. Tunataka sheria ichunguze na itoe hakiii
Uanachama hauganganiwi kama mpira wa kona,kwenye medani ya vyama vya siasa.Wakikukataa ina maana hawakuitaji,unasepa au unaomba msamaha.
Pammoja na hayo zipo sifa za kuwa mwanachama na pia zipo kanuni za kuvuliwa uanachama.
 
Kwa kifupi tu ni kwamba adhabu za wasaliti kwenye vyama ni laini mno, kosa la usaliti jeshini adhabu yake ni kifo tu
 
Bado wajumbe wanapiga kura mdaa huu taarifa ya kwamba wamefukuzwa ni batili. Ikitokea wamefukuzwa basi spika atapelekewa barua kutoka kwa katibu mkuu mh John mnyika kuwa hawa sio wanachama hivyo sio wa bunge tena. Spika asipowafukuza au wasipojifukuza wenyewe basi mamlaka tunarudisha kwa wananchi ndowenye maamuzi ya mwisho ya kulinda na kuitekeleza Katiba.
Lazima mchanganyikiwe paka shume nyie. Magodifaza wao na mabwana zenu hawapo tena. Mama anaupiga mwingi, hawezi kukaa upande wa dhalimu. Ngoja Betina (Tulia) wenu naye ajichanganye muone kitakachomtokea.
 
Ingekuwa kikao ni batili huyo halima na wenzie 18 wasengeshiriki
Waaaataachaje nawakati wameitwaa na kiongozi wao wa chamaa?? Wangegoma kuja siingekuwa sokomoko kama kipindi kilee?? Ngoja wanasheria watatudadafulia
 
Nadhani uamuzi ni sahihi ukiwa na kikundi au mtu hana nidhamu katika chama huwezi kumuachia sababu takuwa sumu katika chama hata kwenye vilabu vya mpira tu ukikosa nidhamu nje. Hawa walivuka hali ya kukosa nidhamu walikuwa na kiburi na kujiweka juu ya wengine kwa bahati mbaya JPM marehemu na Ndungai alikosa nidhamu kidogo tu akaomba na msamaha na msamaha ukipigwa teke kwenye media yuko nje. Na hivi serikali hawana pesa nadhani posho yao itakuwa sehemu ile ya June-1 100 billion matumizi ya serikali😀. Hawa kundi la Mdee wameonesha utovu wa nidhamu wa kiwango cha juu kupitiliza maelezo. Imagine wanatokea watu kama hawa CCM? waliitwa kina Kinana na mzee Makamba sembuse hawa.
 
Aliyewahi kufukuzwa uanachama akaenda mahakamani wakamrudishia uanachama wake ni nani??. Katiba ya chadema ni kama ya FIFA mambo ya chama/mpira hayatapelekwa mahakamani.
C20D61A9-E5A5-4803-8BC1-2FE41E45AA38.jpeg



Kuna na kesi nyingine iliyofunguliwa N.Y

Katiba ya chama cha siasa au taasisi yoyote ndani Tanzania hazipo juu ya sheria za kazi na katiba ya nchi.

Chama cha siasa ni public property, ukishachukua kadi tu unakuwa equal shareholder hivi sio vikundi vya watu wachache wenye kutaka kulazimisha agenda zao tena zisio consitent.
 
Back
Top Bottom