Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Status
Not open for further replies.
Rejea ahadi za CCM wakati wa chaguzi, kama jambo haliwezekani kwa nini watoe ahadi wa kuanzisha mahakama? Point ya msngi IPO hapo

Kwani kuna ahadi ngapi haxijatekelezwa?? na aliyekuambia siasa za afrika ahadi zote zinatekelezeka nan???
 
Hata akaja nani. Mahakama.ya kadhi haiwezekan kugharimia na kodi zetu. Kaomben misaada oman huko.......
 
Ukana...
Hayo yote uliyouliza yalishatolewa majibu siku nyingi tena serikalini...

Inaelekea huna ujuzi na unachotaka kukujadili.
Fanya utafiti utakuwa katika hali nzuri ya kufanya mjadala wenye maana.

Wewe ndo una lolote,Jibu hoja,umefiwa wewe alie mwingine,serikari si ndo ileile mnayoilalamikia.Mi mukianzisha wenyewe nipo tayari kufanya project ya kuchangia,lakini si serikari.Shame on you,shame up on teachers who taught you,it seems education has made you to be more ignorant than those who did not attend ah! ah ! ah !...................UKANA SHILUNGO.
 
Mpaka baraza la waislamu kusema hivyo serikali ishakosa leverage, ikose leverage mara ngapi?

My question was based on principle, not Machiavellian politicking.

Religious institutions derive their tax exempt status from being religious institutions, once they politicize their wherewithal, why shouldn't they be taxed like everyone else?

cc EMT

Sijui hii issue iliishia wapi. Ilikuwa implemented and, if so, how?

Viongozi wa dini wazidi kumkalia kooni Mkulo

VIONGOZI wa dini za Kiislamu na Kikristo jana waliendelea kumkalia kooni Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, licha ya kueleza kuwa ufisadi katika baadhi ya taasisi hizo ndio uliofanya serikali itangaze katika bajeti yake kuwa inazifutia msamaha wa kodi.

Akijaribu kutuliza viongozi wa dini waliokasirishwa na kitendo cha serikali kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi za dini na mashirika yasiyo ya kiserikali, Waziri Mkulo alisema baadhi ya vyombo hivyo vimekuwa vikitumia vibaya misamaha hiyo na kwamba ameiagiza Mamlaka ya Mapato (TRA) kutoa orodha ya vitu ambavyo vitasamehewa kodi.

Aidha alisema vitu vyote vya huduma, ikiwa ni pamoja na vya hospitali na shule havitatozwa kodi na kwamba tayari ameiagiza TRA, kuandaa orodha ya vitu vyote vitakavyotozwa na vitakavyosamehewa ushuru. Katika hotuba yake ya Alhamisi, Mkulo alisema vitu ambavyo havitatozwa kodi ni vile vya huduma za kiroho tu.

Lakini viongozi wa dini walielezea kauli hiyo ya Mkulo kuwa haina msingi na kwamba angekutana kwanza na wadau kabla ya kutangaza kufuta misamaha hiyo kwenye bajeti yake ya mwaka 2009/10 aliyoisoma bungeni mjini Dodoma Alhamisi iliyopita.

Wakizungumza na gazeti hili jana, viongozi hao wa dini walisema uchafu na ukosefu wa maadili upo takriban katika kila sekta, lakini wakasema hiyo haifanyi wahusika wote wastahili kuadhibiwa na kufafanua kuwa Mkulo anaweza kutangaza taasisi za dini ambazo zimedanganya katika kupata misamaha ya kodi.

Askofu Msaidizi wa Kanisa Katokili Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Method Kilaini aliiambia Mwananchi jana kuwa kitu ambacho Mkulo na serikali yake walitakiwa kufanya ni kukutana na wadau na kuwaeleza uamuzi wao; mapungufu waliyoyaona pia kusikia maoni ya taasisi za dini. "Kama kutangazwa majina ya wanaotumia vibaya misamaha, sisi hatuna shida atangaze tu," alisema.

Kilaini alisema: "Mkulo anapaswa kukutana na wadau na kuwafafanulia kuhusu hatua hiyo kabla ya TRA haijataja wale anaodai Mkulo wanaotumia vibaya misamaha hiyo. Kama wabunge wamemwelewa kama sisi tulivyoelewa anategemea sisi tumwelewe vipi? Awaite wadau awafafanulie. Bado nasisitiza kuwa hatua hiyo si sahihi. Wabaya wapo kila mahali, lakini huwezi kutupa mtoto kwa sababu mkono wake umeingia maji machafu.

"Wanaovunja sheria wapo kila mahali huwezi kuhukumu wote kwa kosa la wachache. Katika taasisi za dini wapo wanaovunja sheria. Zipo taasisi hata makanisa yanayoanzishwa kwa lengo la kupata msamaha wa kodi na ilitakiwa serikali idhibiti hilo si kufuta kodi kwa wote."

Aliongeza kuwa ndani ya mfumo wa serikali kuna mapungufu na matatatizo mengi, akiyataja baadhi kuwa ni wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), majina ya walimu hewa na mengineyo. "Ikiwa kasoro ya wachache, inahusisha wote basi walimu wangefutwa wote na pia serikali isingerudisha ruzuku kwa wafanyabiashara," alisema.

Kaimu mufti wa Tanzania, Sheikh Suleiman Gorogosi alisema kwa sasa hawawezi kuzungumza lolote hadi hapo waziri huyo atakapotoa orodha hiyo na baada ya wao kuichambua, ili kuona ni kwa kiasi gani imetoa nafuu kwa taasisi hizo au imezidi kuzikandamiza.

"Haya unauliza wakati orodha yenyewe haijatolewa; yeye si kafafanua; si kasema ameiagiza TRA kuandaa orodha hiyo na kuichapisha magazetini? Sisi tunaisubiri kwa hamu hiyo orodha yake," alisema Sheikh Gorogosi. Alifafanua kuwa iwapo orodha hiyo itatoa unafuu kwa taasisi za dini, wao hawana tatizo. Lakini akaongeza kuwa ikiwa itazidi kuwakandamiza kwa kulazimisha ushuru hata kwa vitu vya huduma katika taasisi na mashirika ya dini, hawataikubali.

Naye Mchungaji John Magafu wa idara ya habari ya Jumuia ya Makanisa Tanzania (CCT) alisema kuwa taasisi za dini zinafanya kazi kwa uwazi, hivyo ni bora Mkulo akaweka wazi taasisi zinazotumia vibaya msamaha wa kodi kwa majina. "Sisi tunafanya mambo kwa uwazi. Ili kuondoa utata unaotumika kuzikandamiza taasisi zote za dini, ataje wahusika wala si jambo la kututia hofu," alisema Mchungaji Magafu.

Alisema kimsingi kama Waziri Mkulo ana ushahidi, yupo huru kutangaza wale wanaotumia vibaya misamaha hiyo. Serikali isifanye kiini macho na kuaminisha wananchi kuwa mapato yake yanategemea zaidi taasisi na mashirika ya dini. Katibu mkuu wa Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda alisema hawataikubali orodha yoyote ambayo itataka vitu vya kutolea huduma katika taasisi na mashirika ya dini kutozwa ushuru.

Alisema Waislamu wanasikitika kuona hata misikiti inatozwa kodi wakati hakuna biashara yoyote inayofanyika ndani zaidi ya watu kuingia kufanya ibada na kusoma na baadaye kutoka. Alisema suala la kutotozwa kodi kwa bidhaa na vitu vya huduma hususan vya kiroho, kiibada, hospitali na hata mashuleni ni haki ya waumini kwa sababu serikali imeshindwa kuwatosheleza katika huduma hizo.

"Kwa miaka mingi serikali imekuwa ikitunyanyasa kwa kututoza kodi katika vitu vya kiibada, kiroho na huduma, lakini kwa sasa hatutakubali kwa sababu ni haki yetu na tutaidai," alisema Sheikh Ponda.

Kauli za viongozi hao wa dini ni mwendelezo wa mjadala mkali ulioibuka hata kabla ya hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2009/10 iliyotolewa bungeni Alhamisi iliyopita baada ya kubainika kuwa taasisi za dini na zile zisizo za kiserikali zinafutiwa kodi.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alisema: "Serikali imeonyesha udhaifu mkubwa katika msamaha wa kodi ya mafuta kwa kampuni za madini, kwani inataka kushauriana nao kwanza. Sasa ni kwanini haikushauriana na vingozi wa dini kabla ya uamuzi huo kama inavyotaka kwa makampuni ya madini?

"Ina maana kuwa serikali inathamini uwekezaji kuliko dini na shughuli za dini? Natambua kuna taasisi za dini zinatumia vibaya misamaha hii, lakini kwa nini serikali itoe adhabu kwa taasisi zote? Ni jukumu la serikali kudhibiti abuse (matumizi mabaya) hiyo."

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, alielezea msamaha wa kodi ya mafuta ya petroli kwa kampuni za madini nchini umelikosesha taifa Sh181 bilioni toka uanze mwaka 2005.

"Msamaha huo ulitolewa wakati kampuni zote zikiwa tayari zina mikataba, hivyo kimsingi msamaha huo haupo kwenye mikataba ya madini ambayo serikali imeingia nayo," alisema Zitto.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-dini-wazidi-kumkalia-kooni-mkulo-print.html
 
Mkuu EMT kama uko court una argue case law kwa ku cite vitu namna hii lazima ushinde.

Kumbe huku ninakofikiria mimi Mkulo alishapita?

Bora nikachukue jimbo na mimi mwaka huu, sera zangu zinafaa naona 🙂
 
Last edited by a moderator:
Mkuu EMT kama uko court una argue case law kwa ku cite vitu namna hii lazima ushinde.

Kumbe huku ninakofikiria mimi Mkulo alishapita?

Bora nikachukue jimbo na mimi mwaka huu, sera zangu zinafaa naona 🙂

Hata JK alilisemea hili: MICHUZI BLOG: JK azungumzia misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini

Kuna uzi mmoja nilianzisha miaka hiyo juu ya hili suala nimeutafuta siupati.

Hata hivyo, kuna mwandishi mmoja anadai kuwa "wanaoneemeka sana na misamaha hii ni makampuni makubwa na si mashirika ya kidini kama ambavyo miaka michache iliyoaminishwa kama njia ya propaganda kuendelea kutetea uwepo wa misamaha."

Ame-quote uchambuzi wa Twaweza wa mwaka 2010: "Misamaha ya Kodi Tanzania: Ipo juu sana na kutufanya kwa kiasi kikubwa kutegemea misaada ya nje" uliosema kuwa kwa mwaka 2010 misamaha ya kodi kwa taasisi za kidini ilikuwa ni asilimia 0.05 tuu na mashirika yasiyo ya kiserikali asilimia 4.06.
 
Mimi si muislamu na sitaki kuamini kua uanzishaji wa mahakama ya kadhi hapa Tanganyika utakua na athari kwa taifa.Mi nadhani ianzishwe tu mbona nchi nyingine wana mfumo huo na hakuna shida?.Mwaka huu msikubali ahadi.

Hata huko Nigeria, Somalia, nk walianza kutokuona tatizo hivi hivi, lakini sasa hivi wanayaona machungu ya hii dini ya Kiislamu!
 
Wewe umepotoka au pombe zinakusumbua, hakuna nchi ulimwenguni ambayo ina waislamu hata kwa asilimia 40% kusiwe na Mahkama ya kadhi ambayo inatambuliwa kikatiba ili kuweza kikidhi matatizo na waislamu kupata haki zao. Tanzania Bara peke yake waislamu hawawezi kupungua asilimia 60% si kwambii Zanzibar ambao ni 99% waislamu.

Waislamu tunaelewa ukishakuwa mkiristo basi ata haki unaweza kuikataa na kupinga kupinga tu mana ndivyo ukiristo. Ivi wewe ulitegemea waislamu haki zao zikatatuliwe na mahakama zenu za ki-mission ambazo hawana taaluma juu uislamu?.

Ivi nyinyi Nyerere munamchukuliaje kama nabii ama mtu aliyekuwa na sifa ya kipekee tofauti na mwanadamu wa kawaida kwamba amesema Tanzania haina dini na nyinyi munatii tu.

Dunia inakuwa wakati wa Julius Nyerere sio wakati wa sasa, sasaivi kuna mambo mbali mbali yanahitaji ufumbuzi waislamu wameona kuna haja ya kuwa na Mahkama ya kadhi tena itambuliwe kikatiba ili matatizo yao yaweze kuwa solved kwa mujibu wa dini yao ilivyotaka, Kama ukiristo haukufundisha nyinyi kuwa na mahkama, Uislamu kwa mujibu wa Quran inafahamisha ivyo kwanini munaleta porojo porojo ambazo hamna elimu nazo?.

Waislamu walio Tanzania nao ni Watanzania hawana sehemu nyengine ya kwao ila Tanzania kwanini wanyanyaswe?

Naomba aya kwenye Quran inayosema kuwa Mahakama za Kadhi LAZIMA ziingizwe kwenye Katiba au zigharamiwe na Serikali!
 
Nyie mmedata sana. Haki za wakristo nani atatetea??
 
kama kweli tamko limetolewa na bakwata. BASI BAKWATA HAINA VIONGOZI BALI INAVIONGOZI HEWA!! Angalia Utetezi Wao "mbona Taasisi Zingine Zinamahakama Zake Mfano Mahakama Ya Ardhi....Kwanini Mahakama Ya Waislam Iwe Nongwa"? Hivi Mahakama Ya Ardhi Raia Wa Dini Zote Wanaishi Angani?Ardhi Haiwahusu?Ardhi Inamanufaa Kwa Wote Bila Kujali Itikadi Yao Na Mahakama Ya Ardhi Itamfaa Peter Na Juma Anaweza Kwenda Kudai Haki Ya Umiliki Wa Ardhi Katika Mahakama Ya Ardhi! Je Mahakama Ya Kadhi Inasifa Hiyo? Kwamba Peter Nae Anaweza Kudai Haki Yake? Peter Hawezi Kwa Sababu Siyo Sehemu Ya Imani Yake!! Je Mahakama Za Kikristo Hazipo? Jibu, Zipo.Je Zinaendeshwa Na Serikali? Jibu Hapana. Kwanini? Kwa Sababu Serikali Ni Ya Wote Na Inapokea Kodi Kwa Wakristo Na Wasio Wakristo Hvy Kodi Za Wasio Wakristo Kutumika Kuendeshea Mambo Ya Wakristo Ni Kuwanyima Haki Wasio Wakristo!! Hvy WAISLAM ANZISHENI MAHAKAMA ZENU,TAFUTENI MAJENGO YENU KAMA MTATUMIA MSIKITINI SAWA TU, LAKINI SIYO KUTUMIA PESA ZA UMMA KWA JAMBO LENYE MANUFAA KWENU.
 
MAHAKAMA YA KADHI INAFAIDA KWENU WAISLAM SISI WAKRISTO HATUNAFAIDA NAYO NA WALA SI IMANI YETU,HVY ANZISHENI KWA KODI ZENU LAKINI SIYO KWA PESA ZETU.Mahakama Ya Ardhi Inafaida Kwa Wote Bila Kujali Dini Ya Mtu.Lakini Ya Kadhi Ni Kwa Mwislam Peke Yake!! Mbona Mnakuwa Si Waelewa?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom