Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Status
Not open for further replies.
Tetere,
Baraza hili si BAKWATA...

Soma tena tamko kwa uangalifu...
Hayo mengine mie sina haja ya kuyasemea labda wengine watakujibu.

Mohammed, wewe waone hivyo hivyo unavyotaka kuwaona. Suala la mahakama ya kadhi ni kitendawili kuliko unavyodhani. Na BAKWATA wana SHUGHULIKIA kuhakikisha kuwa lengo halifikiwi. Tatizo liko hivi:
1. Lengo la mahakama ya kadhi haliko wazi
2. Nia haiko wazi
3. Mkakati na mipango ya kufikia lengo ni vurugu, dhaifu na imejaa rushwa
4. Waislam hawawezi kufikia lengo wakati kuna waislam wanaSHUGHULIKIA lengo lisifanikiwe kwa kula rushwa, kushibishwa matumbo yao na tamaa zao, kwa dhuluma!
 
Kwanini watoe ahadi hewa sasa, kama suala haliwezekani basi watoe elimu kwa wananchi kwamba kwakua hakuna fungu lolote pesa linaloenda kwa wasio waislamu basi vivyo hivyo haitawezekana kwa waislam kutengewa fungu kisha wangetoa mawazo mbadala wa kufanikisha hili.

Wanasiasa husema chochote wanapoomba kura. Ni jukumu letu wapiga kura kuchambua pumba na mchele. Kwa chaguzi za 1995, 2000, 2005, 2010, CCM haijateleza hata 10% ya iliyoyaahidi.
Hilo la mahakama ya kadhi ni moja kati ya mambo elfu moja ambayo hayajatekelezwa kwa wapiga kura.
 
Hiyo Mahakama uishaambiwa ilikuwepo na ilitambulika hata na Serikali ya Kikoloni hadi mwaka 1963.

Suali ni je, nani aliiondosha na kwa malengo gani na kama pana badali ya ile Mahakama /Chombo cha kusimamia mambo /masuala ya Waislaamu ni kipi na kiliekwa na nani....!?

Ahsanta huenda /labuda weye baadaye ukajafahamu kama ukajiepusha na mazogo /ushabiki.

Nipo kipembeni hapa.

Kuna muislamu yeyote aliyekosa haki yake kwa kukosekana kwa mahakama ya kadhi toka 1963 hadi sasa?
 
Kwani kuna dini au madhehebu gani ambayo imeomba mahakama ?!....kwa ajili ya kesi gani !?
Hii ni njia moja wapo ya kukimbia ukweli kuhusu kuanzisha Taasisi hii !
Hawa viumbe wa ajabu wanasumbuliwa na chuki tu, mahakama ya kadhi ni kwa ajili ya Waislam lakini kwao ni shida.
 
Kuna muislamu yeyote aliyekosa haki yake kwa kukosekana kwa mahakama ya kadhi toka 1963 hadi sasa?

Malalamiko ya Waislaamu kutaka wahukumiwe kwa mujibu wa Imani yao hujapatapo sikia ama mekufahamu sivyo....!?

Khasa kunako mas ala ya MIIRAATHI na NDOA....!?

Ndiyo wapo.
 
Malalamiko ya Waislaamu kutaka wahukumiwe kwa mujibu wa Imani yao hujapatapo sikia ama mekufahamu sivyo....!?

Khasa kunako mas ala ya MIIRAATHI na NDOA....!?

Ndiyo wapo.

kiukweli sijawahi kuyasikia... utanisamehe kwa hilo...
na ni kwa nini basi mambo yanahusu mirathi nk yanavyotamkwa kwenye sheria za kiislamu yasiwekwe kwenye sheria za kawaida za nchi. then ikatamkwa kuwa yatakuwa considered kwa waislamu tu?
 
Mohammed, wewe waone hivyo hivyo unavyotaka kuwaona. Suala la mahakama ya kadhi ni kitendawili kuliko unavyodhani. Na BAKWATA wana SHUGHULIKIA kuhakikisha kuwa lengo halifikiwi. Tatizo liko hivi:
1. Lengo la mahakama ya kadhi haliko wazi
2. Nia haiko wazi
3. Mkakati na mipango ya kufikia lengo ni vurugu, dhaifu na imejaa rushwa
4. Waislam hawawezi kufikia lengo wakati kuna waislam wanaSHUGHULIKIA lengo lisifanikiwe kwa kula rushwa, kushibishwa matumbo yao na tamaa zao, kwa dhuluma!

Tetere,
Uungwana ni mtu kustahi fikra na mawazo ya mtu mwingine.

Ikiwa hizo ni fikra zako sawa na tusubiri tuone.
 
kiukweli sijawahi kuyasikia... utanisamehe kwa hilo...
na ni kwa nini basi mambo yanahusu mirathi nk yanavyotamkwa kwenye sheria za kiislamu yasiwekwe kwenye sheria za kawaida za nchi. then ikatamkwa kuwa yatakuwa considered kwa waislamu tu?

Tuko,
Hayo unayosema mbona yashajadiliwa sana?

Inaelekea wewe ni mgeni katika jambo hili.
Ikiwa hivyo ndivyo soma kwanza kisha ndiyo uingie katika mjadala huu.
 
kiukweli sijawahi kuyasikia... utanisamehe kwa hilo...
na ni kwa nini basi mambo yanahusu mirathi nk yanavyotamkwa kwenye sheria za kiislamu yasiwekwe kwenye sheria za kawaida za nchi. then ikatamkwa kuwa yatakuwa considered kwa waislamu tu?

Hii nchi haina uadilifu na Katiba ndo Msingi mkuu wa Utawala.

Sasa ushauri wako mzuri ila nami nashauri kuwa, wacha tuitie kunako hiyo Katiba ya Nchi kisha tutajaitungia hizo Sharia ndanimwe humo.

Kwani tatizo liwapi khasa kwa upande wa pili/ Wakristo maana yaonekana wao ndo wasoitaka dhaahir shaahir....!?

Kwani kuna nini huko/ humo hadi washupake nalo kiasi hiko....!?
 
Mohamed Saidi ni mtu mstaarabu sana,hana jazba anatoa darsa kwa lugha nzuri hata kwa mtu mkorofi.Tofauti na hawa panya road kina Ritz,THE BIG SHOW na kahtan!Mzee Mudi kwa nini sasa huwa huungani na sisi kwenye topic zingine kutupa busara zako?
 
attachment.php

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM (T)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

17 Mfungo Sita 1436
9 Januari 2015

TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI KWA WATANZANIA WOTE, JUU YA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI NA. 02, WA MWAKA 2014, HUSUSAN KUHUSU SEHEMU YA MAREKEBISHO KWENYE SHERIA YA TAMKO LA SHERIA ZA KIISLAM

Awali ya yote tunapenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu, Ardhi na vilivyomo, na Rehma na Amani zimfikie Kiongozi wa Ummah Mtume Muhammad (SAW).

Ndugu wanahabari,
Assalam Alaykum Warahamatul llah Wabarakatuh.

Tumekuiteni hapa kwa lengo la kueleza kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 02, wa mwaka 2014 haswa kuhusu marekebisho kwenye sheria ya tamko la Sheria za Kiislamu. Tunafahamu kuwa kuanzia tarehe 13 hadi 23 Mwezi huu wadau mbalimbali wataitwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba kwa ajili ya kuwasilisha mapendekezo yao, Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania tukiwa sehemu ya wadau muhimu tunapenda kuwaeleza kuwa mtiririko wa mchakato wa marekebisho ya sheria kwa mujibu wa muswada huu unaokusudia kutambua Mahakama za Kadhi Tanzania bara una kasoro kubwa na kwa dhati unaonesha wazi kuwa serikali haina nia ya kweli ya kuunda Mahakama ya Kadhi yenye hadhi kamili ya kimahakama na uthabiti wa kuwepo kwake na kuwa muswada huu ni hadaa nyingine ya serikali hii ya CCM kwa Waislamu kwa sababu zifuatazo:-

1. Malalamiko juu ya Mahitaji ya Mahakama ya Kadhi yana historia ya kupindishwapindishwa na serikali hii inayoundwa na CCM.
Kwa mfano katika Ilani ya CCM mwaka 2005 iliahidi kuanzisha Mahakama ya Kadhi lakini kwa ghilba nyingi CCM haikutekeleza ahadi hiyo baada ya kuingia madarakani kwa hoja kuwa hili ni jambo la Kikatiba.

Hata hivyo mchakato wa Katiba mpya ulipokuja asilimia kubwa ya maoni ya Waislamu yalihitaji Mahakama ya Kadhi kuingizwa ndani ya Katiba, mapendekezo hayo yalikataliwa na Tume ya Jaji Warioba kwa hoja kuwa katiba inayotengenezwa ni ya Muungano na suala la Mahakama ya Kadhi si la Muungano hivyo lisubiri wakati wa kuandaa Katiba ya Tanganyika. Waislamu tukavumilia kuisubiri Katiba ya Tanganyika.

Lakini Bunge Maalum la Katiba likaikataa Katiba ya Warioba na kutunga Katiba Mpya Pendekezwa yenye mambo yote ya Muungano na yasiyo ya Muungano bila ya kuingiza Mahakama ya Kadhi kama ilivyoahidiwa na Tume ya Jaji Warioba. Bunge la Katiba lililokuwa linaundwa na wajumbe wengi wa CCM hawakuona umuhimu wa kutimiza ahadi yao ya kuweka Mahakama ya Kadhi katika katiba pendekezwa na kwa makusudi Mahakama ya Kadhi ikakataliwa na wajumbe wengi wa CCM walishangilia jambo hili ili hali wanajua dhahiri kuwa Waislamu hawakufurahishwa na uamuzi wao na pia kukiuka Ilani yao na ahadi kwa Waislamu.

Muswada huu ni sehemu nyingine ya hadaa kwa Waislamu kwani badala ya sheria kuanzisha Mahakama ya Kadhi kama ilivyo kawaida ya uanzishwaji wa mahakama zote duniani muswada huu umeliacha jukumu hilo kwa taasisi binafsi ili hali Mahakama ya Kadhi kama zilivyo mahakama zingine ni sehemu ya chombo cha dola katika mfumo wa Mahakama yaani “the Judiciary”, hili limefanywa makusudi kutokana na kutokuwepo na nia ya dhati ya Serikali ya CCM kuanzisha na kuona Tanzania Bara kunakuwa na Mahakama ya Kadhi madhubuti na ya ukweli.

2. MUSWADA umempa mamlaka “Mufti” kuteua makadhi na kutengeneza kanuni za Uendeshaji wa Mahakama ya Kadhi ili hali Mufti sio chombo cha kisheria.
Hakuna sheria inayounda ofisi ya Mufti isipokuwa uwepo wake unategemea katiba ya BAKWATA. Maana yake ni kwamba Mahakama ya Kadhi uwepo wake utategemea uwepo wa Katiba ya Bakwata inayounda ofisi ya Mufti. Kukiwa na mgogoro wa kikatiba Bakwata athari yake itaikumba na Mahakama ya Kadhi. Hakuna duniani mtu ambaye ofisi yake haiundwi na sheria kisha sheria ikampa mtu huyo madaraka ya kuunda chombo chenye mamlaka ya kisheria kama mahakama. Serikali ya CCM inalijua hili lakini imefanya makusudi kwa kusukumwa na nia yake ya kutopenda kuona Waislamu wanakuwa na Mahakama ya Kadhi ya ukweli iliyo madhubuti.

3. Kama tulivyoeleza hapo juu MUSWADA umempa Mufti mamlaka ya kutengeneza kanuni za uendeshaji wa Mahakama za Kadhi hili ni jambo la ajabu sana kwa ofisi ambayo haiundwi na sheria kuwa na mamlaka ya kutengeneza kanuni za kuendesha chombo cha kisheria ambacho ni Mahakama ya Kadhi. Hili ni jambo ambalo haliwezekani.

4. Kwa madaraka makubwa aliyopewa Mufti sheria haielezi ni nani mwenye mamlaka ya kumuondoa kadhi na wala haiweki sifa za kadhi na wala haiweki vigezo vinavyoweza kumuondoa kadhi yote hii inadhihirisha nia ya serikali ya CCM kuunda Mahakama ya Kadhi legelege na kiini macho.

5. MUSWADA unaeleza Waziri anayehusika na mambo ya sheria kupewa mamlaka ya kutunga taratibu za kutekeleza hukumu za Mahakama za Kadhi bila ya kushauriana na wanazuoni wa Kiislamu.
Japo katika sehemu ya maelezo ya muswada Mwanasheria wa Serikali ameeleza kuwa Waziri atashauriana na wanazuoni maelezo hayo ni hewa kwani si sehemu ya sheria.

6. MUSWADA umetoa hiyari kwa mtu kufungua shauri katika Mahakama ya Kadhi.
Jambo hili limekusudiwa kuifanya Mahakama ya Kadhi iwe butu na kutoa mwanya wa kutokea mgongano baina ya Mahakama ya Kadhi na mahakama za kawaida ikiwa kila upande katika mgogoro utaamua kufungua shauri katika mahakama tofauti. Hili lisingewezekana kama serikali ingekuwa na nia ya kweli ya kuunda Mahakama ya Kadhi madhubuti.

7. MUSWADA kuitaka Mahakama ya Kadhi ijiendeshe yenyewe:

MUSWAAD huu unaitaka Mahakama ya Kadhi ijiendeshe yenyewe badala ya kuendeshwa na serikali jambo ambalo halijawahi kutokea sehemu yeyote duniani chombo kama mahakama kujiendesha chenyewe.

Mahakama ya Kadhi itafanya jukumu la serikali katika kutafsiri sheria za Kiislamu ambazo ni sheria halali kutumika Tanzania hakuna mantiki yoyote kwa chombo hicho kujiendesha chenyewe kama ambavyo serikali ya CCM inataka kufanya.

Isitoshe uwepo wa hii Mahakama ya Kadhi kutaipunguzia serikali mzigo na msongamano wa kesi katika mahakama za kawaida jambo ambalo serikali inapaswa kugharamia uwendeshwaji wake. Serikali kukataa kuigharamia hii Mahakama ya Kadhi ilihali katika nchi hii upande wa Zanzibar serikali inaiendesha Mahakama ya Kadhi kunadhihirisha kuwa kuna nia ya kuidhoofisha mahakama hii ishindwe kujiendesha na kuwa na mahakama isiyokuwa na maana yoyote.

Zipo mahakama za makundi ya watu maalumu ambazo zinaendeshwa kwa pesa za serikali ambazo ni kodi za Watanzania wote. Mfano ni kama vile Mahakama ya Kazi, Ardhi, Biashara n.k. ni kwanini mahakama itakayotafsiri sheria za Kiislamu iwe nongwa?

8. UTAFITI unaonyesha kuwa suala la Mahakama ya Kadhi huletwa kila unapokaribia Uchaguzi Mkuu bila ya utekelezaji linazidi kutupa wasiwasi kwani inaonesha serikali ya CCM imeshazowea kuwacheza shere na kuwalaghai Waislamu na Watanzania kwa ujumla kwa maslahi yao ya kisiasa.
Tabia hii ni hatari sana kwa mustakabali na ustawi wa taifa letu.

Hitimisho
Ndugu wanahabari, kwa maelezo yaliyobainishwa katika taarifa hii, tunahitimisha kwa kusema:

a) Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) zimeukataa na kupinga mapendekezo ya marekebisho kwenye sheria ya tamko la Sheria ya Kiislam kama lilivyo katika MUSWADA wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali na. 02 wa mwaka 2014, mpaka utakapo andaliwa upya kwa kuhusishwa wanazuoni wa Kiislamu, wanasheria wa Kiislamu waliobobea na kwa kuzingatia maslahi ya Waislamu na taifa kwa ujumla na pia Mahakama ya Kadhi ni lazima iingizwe katika Katiba ili kuipa uthabiti.

b) Kwa kuwa katiba inayopendekezwa haitambui Mahakama ya Kadhi na inapinga sheria yoyote inayokwenda kinyume na katiba hiyo ikiwemo Sheria za Kiislamu kwa kauli moja na kwa nguvu kubwa Jumuia na Taasisi za Kiislamu (T) zitawahamasisha Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuikataa kwa KUPIGA KURA YA HAPANA katiba inayopendekezwa muda utakapofika wa kuipigia kura.

Ndugu waandishi wa habari,
Ahsanteni sana kwa ushirikiano mliotupa.

Tunawatakia kazi njema katika ujenzi wa taifa letu.

Kaimu Katibu
………………………….

Jumuiya na Taasisi za Kiislam (T)



Ajira za watu hizo, zitengenezeni hizo fursa wakuu
 
Hii nchi haina uadilifu na Katiba ndo Msingi mkuu wa Utawala.

Sasa ushauri wako mzuri ila nami nashauri kuwa, wacha tuitie kunako hiyo Katiba ya Nchi kisha tutajaitungia hizo Sharia ndanimwe humo.

Kwani tatizo liwapi khasa kwa upande wa pili/ Wakristo maana yaonekana wao ndo wasoitaka dhaahir shaahir....!?

Kwani kuna nini huko/ humo hadi washupake nalo kiasi hiko....!?

Wakristo tunataka fair play. ..
Mambo yetu hayapo kwenye gharama za serikali, kwa nini ya waislamu?
 
Mi nawakubalia muunde ila sitaki kabisa kodi yangu ihudumie mahakama hii, muwe mnawalipisha wanaofungua kesi. Huwezi tumia kodi ya mkristo kwa hili. Kamwe
 
sielewi hapa

Bora usielewe tu ni kuimizani kichwa tuu, nchi aina dini, watu wanalazimisha limahakama lao tuliendeshe sisi tusio wasilamu (taxes) ni upopo.

Endesheni wenyewe, tokeni vijiweni tafuteni mapoli jengeni misikiti huko, tafuteni vyanzo vingi vywa mapato, then anzeni.

Zanzibar ni nchi ya kisilamu kuendesha mahakama hiyo ni sawa.

Sipendi kusikia tena u.ji.nga huu hapa. tumechoka.
 
Wakristo tunataka fair play. ..
Mambo yetu hayapo kwenye gharama za serikali, kwa nini ya waislamu?

Hiyo Mahakama ilikuwepo tangu,
Suali ni je, nani aliiondosha....!?

Tuanze na hapo ndo penye KIINI, mangine yatatufika kirakhisi mno.

Ahsanta na tuendelee na Darsa.
 
Wakristo tunataka fair play. ..
Mambo yetu hayapo kwenye gharama za serikali, kwa nini ya waislamu?

Wakiona vipi waende zanzibar huku Tanganyika haiwezekani, walipa kodi wakuu Tanganyika ni wakristo ndio wengi kila sehemu za uzalishaji utawakuta wao.

Mbona roman Catholic wanayo wao ulna uendesha wao kwa kutumia canon law, na hawajawai kulialia.

Sipendi udini kweli kwenye utanganyika wangu, wote ni sawa.
 
Hiyo Mahakama ilikuwepo tangu,
Suali ni je, nani aliiondosha....!?

Tuanze na hapo ndo penye KIINI, mangine yatatufika kirakhisi mno.

Ahsanta na tuendelee na Darsa.

Wabara
Kama ilikuwepo kwenye sheria ni wazi kuwa iliwekwa na watunga sheria na iliondolewa na watunga sheria. Labda tujiulize sababu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom