Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Baraza Kuu la Waislam Tanzania latoa tamko kuhusu Mahakama ya Kadhi na Katiba iliyopendekezwa

Status
Not open for further replies.
...haya ona sasa!CCM wamegawa nchi na hapa naona alshabab,boko haram wanapisha hodi,hii ndio matokeo ya kuendesha nchi kisanii.Ona sasa walikataa sensa lakini eti matokeo yakatangazwa wakati watu kibao hawakuhesabiwa,ile sensa ni feki.......

Hatuna njia ni kuleta tu hiyo mahakama ya kadhi maana kuikataa basi alshabab,boko haram.alqaeda wanakuja....mmetaka wenyewe sasa inyweni....mlidharau misingi ya BABA WA TAIFA......kuna madai ya baraghasia ipo njiani kwa wanaume,wanawake tayari ushungi.....nini sasa!..unafikiri watu hawajui maana ya uniform
 
walislamu waliona jk ni mwenzao wakampa kura 2010 sasa walivyoachwa kwenye mataa hawaamini hadi leo!
_sasa mara hii anapita mkristo sijui itakuweje huko twendako na mahakama yenu


_changeni pesa muanzishe mahakama hizo kwa hela yenu ndio ushauri wangu
Nadhani huna kumbukumbu nzuri pale askofu wa katoliki alipotangaza hadharani kwamba Kikwete ni chaguo la Mungu. Aidha, mwenye akili zake timamu na apendae kuhushughulisha ubongo wake ipasavayo anafahamu pasipo na shaka yoyote ile kwamba endapo angechaguliwa na Waislamu peke yake basi JK asingeingia Ikulu! Acheni huu ujinga wa kuaminishana kwamba jamii fulani ndio tatizo la nchi hii!! Kama Waislamu walimchagua JK kwa kumuona mwenzao, Wakristo ambao walimpigia kura kwanini walifanya hivyo? Ni mkoa, wilaya au kijiji gani Tanzania hii ambako JK hakupigiwa kura? Kote huko kuna Waislamu peke yake? Achana na mawazo mgando ndugu....
 
Heshima kwako Maalim. Swali langu, umeweka kichwa cha habari: "BARAZA KUU LA WAISLAMU TANZANIA LATOA TAMKO..." Lakini tamko lenyewe ni la JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU (T). si kwamba hizo ni taasisi mbili tofauti? Maana kwa uelewa wangu mdogo - nisahihishe tafadhali - Baraza kuu la Waislamu Tanzania ndio BAKWATA, ambayo ni tofauti na hiyo Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu.

Lakini kwa maoni yangu mimi, nadhani kila mtu mwenye akili alitambua kwamba kilichotokea wakati wa mtifuano wa katiba pendekezwa, kiasi kwamba mpaka waliokuwa Hijja Makka walisemekana kupiga kura kwa fax au email, ilhali taarifa zingine rasmi kabisa zikionesha kwamba ilikuwa ni haiwezekani hilo kufanyika; kilichotokea ni gilba. Waislamu walitulizwa ili mambo yaende. nadhani wengi wao walilijua hili, kwamba hapa tunatulizwa tu.

Mapambano mema yenye mafanikio!!
 
Katika hii taarifa kuna hoja za msingi na zingine hapana.

All in all,CCM hiyo katiba pendekezwa itawatokea puani maana mmeharibu karibu kwenye kila eneo/idara.
 
Hata Mohamed Said ungepewa uraisi wa Tanzania, nakuhakikishia hutaweza kuinfluence mahakama ya kadhi igharamikiwe na serikali, ama kwa kupitia katiba, kwa sheria za nchi au hata kwa udikteta... hutaweza...

Mimi ni mpinzani mkubwa wa CCM, lakini nina uhakika kwa hili mnawaonea...
 
Last edited by a moderator:
Astaghafilullah kafiri weye unaongea ufirauni mwanakharam mkubwa weye..Hahahahaha...:glasses-nerdy::biggrin::biggrin:
Hii kitu wangeikomalia Ccm wangeharisha maji..lakini wenyewe kwa wenyewe wanafitiniana. Hapo utamsikia yule Shekh wa mkoa wa daslama,mnafiki yule anakuja kuunga mkono hoja ya "subra" kumlinda kikwete..ptyuuuuu!!!
Halafu kwa kujifanya mko smart nyie watu hamjambo? Hivi huko Ugalatiani hakuna unafiki na kusalitiana? Ikiwa Sheikh wa Mkoa ni mnafiki kwa kigezo kwamba huenda akatoa tamko la kumlinda JK, vipi kuhusu yule Askofu ambae alitangaza hadharani kwamba JK ni chaguo la Mungu? Hivi Wakristo si mnaamini kwamba Uislamu ni Ushetani? Sasa ikiwa ni ushetani, ni unafiki kiasi gani Askofu kusimama hadharani kutangaza shetani ni chaguo la Mungu? Acheni chuki zenu za kijinga... nchi hii Wakristo na Waislamu wote ni tatizo lakini watu walivyo wajinga wanajitia upofu na kuona CCM inakaa madarakani kwa ajili ya Waislamu wakati Bara kote huko ambako kumejaa Wakristo kote huko wanaichagua CCM.
 
Sasa hivi nadhani BAKWATA wamejifungia wanaandaa Tamko kuwapinga hawa jumuiya za kiislam na wataunga mkono hoja,Mapendekezo au mswada unaopendekezwa... Si Mufti amepewa mamlaka ya kuteua hao Makadhi..!!!

THE BIG SHOW FaizaFoxy poleni kwa Dilemma hii!!

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Pasipo kumumunya maneno, uoga wala kuongea kwa kuogopa au kufarijiana, Tanzania sio nchi ya kidini na haitajuja kuwa kamwe.

Suala la Mahakama ya Kadhi halitakuja kuingia kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano, sasa tuweke Mahakama ya Kadhi ambayo ni ya kidini kwenye Katiba kwani hii nchi ni ya Waislamu peke yao?? Katiba ni mali ya wananchi wote, wa dini zote.

MAHAKAMA YA KADHI MWIKO kuingia kwenye katiba, Isipokua umoja au mamlaka binafsi za kiislamu ziunde mahakama pasipo kuingia kwenye katiba ili kuendelea kufanya shughuki zenu za ibada..

Kuweka kwenye katiba na kusema Mufti ajulikane kikatiba unataka kusema sasa Maaskofu wote wajulikane kikatiba na Wachungaji Viongiozi wa makanisa mengine mengi nchini!!

Hili jambo halitafanyika Tanzania, hii nchi haina dini isiookua watu wake wana dini na katiba iliyopo inaheshimu uhuru wa ibada, sasa uhuru huo umekua mkubwa kiasi kwamba mnavuka mipaka ya kutaka kujiamulia mambo hadi ndani ya katiba.

Jambo hili ni baya, chafu, linanuka na halina sababu njema za amani na utulivu katika Taifa letu.
Acheni ujinga kabisa kabisa na mkome kabisa.
 
....
KUPIGA KURA YA HAPANA katiba inayopendekezwa muda utakapofika wa kuipigia kura.

Ndugu waandishi wa habari,
Ahsanteni sana kwa ushirikiano mliotupa.

Tunawatakia kazi njema katika ujenzi wa taifa letu.

Kaimu Katibu
………………………….

Jumuiya na Taasisi za Kiislam (T)




 
Hata Mohamed Said ungepewa uraisi wa Tanzania, nakuhakikishia hutaweza kuinfluence mahakama ya kadhi igharamikiwe na serikali, ama kwa kupitia katiba, kwa sheria za nchi au hata kwa udikteta... hutaweza...

Mimi ni mpinzani mkubwa wa CCM, lakini nina uhakika kwa hili mnawaonea...


Rejea ahadi za CCM wakati wa chaguzi, kama jambo haliwezekani kwa nini watoe ahadi wa kuanzisha mahakama? Point ya msngi IPO hapo
 
Last edited by a moderator:
Siku za mwongo ni fupi, ni hawa hawa waliokaa kimya wakati wenzao walipopigishwa kura feki kwa njia za kichawi, kura haramu za kwenye mtandao, na nyingine alizooteshwa kwenye ndoto Samweli Sitta, bila kusahau za kupigishwa marehemu, na wale waliohamishwa kimiujiza Zanzibar.

Hawajitambui wanaotoa matamko sasa. Kama walipewa peremende wakakubali katiba feki, sasa matamko ya nini? Waishi katika kweli nayo itawaweka huru...............

Labda waikatae katiba mpya kwa sababu za msingi zaidi, na madhaifu mengi yaliyojaa kwenye hiyo katiba haramu, sio kuitumia kama chambo cha cha kupitishia/kurekebishia sheria iliyotungwa.

Hawa watu hawajui kuwa hiyo sheria hata ikiruhusu pesa za watanzania kuhudumia hizo mahakama, mwisho wake ni Mwezi April, pindi katiba wanayoitumia kama chambo kutishia serikali, endapo itapita???

Kuna tatizo kubwa la uelewa wa hawa wenzetu....., Waonewe huruma tu....
 
Halafu kwa kujifanya mko smart nyie watu hamjambo? Hivi huko Ugalatiani hakuna unafiki na kusalitiana? Ikiwa Sheikh wa Mkoa ni mnafiki kwa kigezo kwamba huenda akatoa tamko la kumlinda JK, vipi kuhusu yule Askofu ambae alitangaza hadharani kwamba JK ni chaguo la Mungu? Hivi Wakristo si mnaamini kwamba Uislamu ni Ushetani? Sasa ikiwa ni ushetani, ni unafiki kiasi gani Askofu kusimama hadharani kutangaza shetani ni chaguo la Mungu? Acheni chuki zenu za kijinga... nchi hii Wakristo na Waislamu wote ni tatizo lakini watu walivyo wajinga wanajitia upofu na kuona CCM inakaa madarakani kwa ajili ya Waislamu wakati Bara kote huko ambako kumejaa Wakristo kote huko wanaichagua CCM.
Institutionally Bakwata ipo upande wa Ccm. Huko kwa wagala ni individual's corrupt mind ndo wanasupport.
Kwa taarifa yako,expect nothing as Kadhi court under this Bs Ccm reign. Hata sasa mtapigwa tobo na mtakubali. wameshawajulia weakness yenu,
 
...

Hata Wapagani tunasema
Hapana kwa Katiba inayopendekezwa ya Warioba tu !!!
 
Ikiwa watapata mahakama ya kadhi,Je? kwa wasio waislamu watahusika katika sharia?/mahakama hizo?
 
Hizi sintofahamu ni kwa faida ya nani kama si ccm na kuendelea na katiba ya zamani? All in all, tupeni tume huru ya uchaguzi hayo mengine mbele ya safari.
 
Safi sana, pigeni kura ya hapana ili tuendelee na katiba iliyopo. Eti mtaipunguzia mzigo serikali, kwani serikali imewaomba msaada. Kimbelembele chenu mnataka kukifanya iwe ni lazima.

Acha kupotosha. kura ya hapana haimaanishi tunarudi kwenye katiba ya 1977. bali tunakwenda kurekebisha iyo katiba ya ccm
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom