Baraza la Chuo Kikuu Huria Tanzania lamtaka Prof. Bisanda aombe radhi kuhusu waraka wa Corona alioutoa

Baraza la Chuo Kikuu Huria Tanzania lamtaka Prof. Bisanda aombe radhi kuhusu waraka wa Corona alioutoa

kwa nini aombe radhi mbona ukweli wa jambo hili liko wazi.
 
Baraza la Chuo Kikuu Huria, limekaa kikao cha dharura na kuagiza Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Elifas Tozo Bisanda aombe radhi kwa Wizara ya Elimu, Chuo Kikuu Huria na Umma kwa waraka wa tahadhari ya #CORONAVIRUS alioutoa Februari 8, 2021.

Prof. Bisanda alitoa waraka kuwatahadharisha wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho kuhusu ugonjwa wa Corona. Baraza limebaini kuwa yalikuwa maoni binafsi na alikosea kutumia nembo za Serikali.

Aidha imedaiwa taarifa ya Prof. Bisanda imeonekana kukinzana na Sera ya Serikali juu ya tahadhari dhidi ya #COVID19 pia haikuwa na takwimu za kuthibitisha uhalali wa baadhi ya taarifa hizo.

Baraza limeagiza wanafunzi na wafanyakazi wa chuo waendelee na kazi na masomo kama kawaida. Pia limeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Pia soma

- Chuo Kikuu Huria cha Tanzania(OUT) Chatahadharisha wanafunzi na wafanyakazi wake dhidi ya COVID19 NA COVID21

- Corona: Wizara ya Elimu yaukana waraka wa Prof. Elifas Tozo Bisanda Makamu wa Chuo Kikuu Huria (OUT)
Watalaam wanapokuwa waganga wa kienyeji!!
 
Ujumbe wangu kwa taifa
"Kama unajua kaa kimya"
 
cc Kichuguu mbona umeadimika sana? Njoo uone ''the Bold Magufuli wako asivyojali.

Haa haa haa MTAZAMO yamekufika. Mwana kulitaka, mwana kulipata! Hata wenzako kina Kichuguu na Mwanakijiji sasa hivi Magufuli ameangusha sana. Ni kwa sababu tu watu wanataka kufa na tai shingoni.
Huenda ni kwa sababu unapenda kusoma na kuandika mambo ya namna fulani, hivyo unadhahi wote tuko hivyo. Uliisoma thread hii niliyoanzisha mwezi uliopita, na watu wa aina yako wakanishambulia tena?

Au ulisoma post yangu hii? Tunanadika mambo objective huwa hatuangalii yanamhusu nani; Magufuli akifanya vizuri tutamsifia, na akifanya vibaya tutamkosoa pia. Sio kama wewe unaoyeonekana kupenda kukososa tu hata pale pasipohusika.

Wamekuwa watumwa wa mtu kwa tamaa ya fedha!
Sio tu tamaa ya Fedha Bali Kwa uoga wa kujiajiri. Hao ndio think tanks wa Taifa. Nonsense kabisa.

Wanataka kuaminisha umma kuwa hakuna Tatizo la Covid 19?? Wao wamepata wapi takwimu za kumpinga mwenzao aliyetoa takwimu hata kama sio accurate kivile?

Hawa ndio Mzee Mkapa alikuwa anawaita Wapumbavu-Malofa.
 
Na ATUMBULIWE KABSA yeye nan wa kutoa waraka mzto kama ule wakat hana mamlaka ya kufanya ivo
Huyo ni Kiongozi wa Taasisi Hana Mamlaka kivipi?? Ni moja ya majukumu yake ya Kila Siku kuhakikisha usalama wa wanafunzi unapatikana.
 
Mnavyopiga kelele mtasema huwa hamuendi makazini shubamiti zenu! Huna ata uweze wakujilockdown lakini unashadadia kama hela yakuishi ata mwezi unayo..!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama kuna changamoto kubwa Nchini basi ni kuwa na watu wengi wasiojielewa.

Unataka kusema tufiche ukweli Ili kusiwe na lockdown? Au Ili twende makazini??

Ndugu unajiona mfanyakazi Bora Kwa vile Corona virus hajakutight. Akikutight vizuri hiyo kazi hutoikumbuka na wala hutokumbuka kama umeajiriwa.
 
Back
Top Bottom