KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Kuna aina mbili za mitazamo ya watu juu ya viongozi wa dini:
Aina ya kwanza wanawatazama viongozi wa dini kama wanadamu kamili na wenye ukamilifu wote, kunena mpaka kutenda kwao ni kwa ukamilifu. Hawakosei lolote
Aina ya pili wanawatazama viongozi wa dini kama wanadamu wa kawaida, wanatenda makosa kama wengine ila ukubwa wa makosa unatofautiana na wengine.
Mitazamo ya makundi yote mamili ndio imechangia pakubwa kuwaamini viongozi wa dini na sauti zao kutumika kwenye mengi lakini sio mara zote SAUTI ZAO ni ujumbe wa kinabii.
Baada ya utangulizi huo, niseme machache yafuatayo:
Tunawaamini viongozi wa dini katika mengi ila sio katika yote Kwa sababu nao ni wanadamu wa kawaida.
Kama wanadamu wanakosea katika mengi hivyo kuna hati hati wenye mtazamo wa kundi la kwanza juu ya viongozi wa dini wakaingizwa kwenye makosa ya kuwaamini.
Juu ya suala la uwekezaji bandari, mtazamo na maoni ya baraza la Maaskofu unaweza kuwa ni Moja ya makosa maana nao ni binadamu.
Sipingani na viongozi wa dini Kwa Imani zao bali napingana nao Kwa ubinadamu wao. Kabla ya kuwa kiongozi wa dini alikuwa ni binadamu wa kawaida, hawezi kuacha kuwa binadamu wa kawaida baada ya kuwa kiongozi wa dini.
Maswali ninayojiuliza ambayo natamani TEC waje wayajibu:
Je, ikitokea kutokana na tafsiri na uelewa ,wanachopinga kikawa sio kweli watakuja kuupinga waraka wao?
Je, licha ya yote kukiwa na faida katika uwekezaji huo watapinga waraka wao?
Je, ikiitishwa kura ya maoni Leo, kujua wanaopinga na wanaokubali uwekezaji wapi wengi, na ikaonekana wanaokubali ni wengi watapinga waraka wao?
Ndio maana nimesema Baraza la Maaskofu nao ni wanadamu wa kawaida, wanakosea katika mengi hata hili la waraka ni Moja ya makosa.