Baraza la Maaskofu nao ni wanadamu wa kawaida, wanakosea katika mengi hata hili la waraka ni Moja ya makosa.Maswali ninayojiuliza ambayo natamani TEC waje wayajibu:
1. Ni kweli ni wanadamu, "wanaweza" kukosea. Waliofanya maamuzi ya kugawa bandari zetu Watanganyika Kwa kuuandaa huo uchafu unaitwa mkataba, wao ni miungu au malaika kiasi kuwa hawawezi kukosea?
2. TEC imetumia reference ya vipengere vya mkataba wenyewe kuja na hitimisho kuwa mkataba huu haufai na hawauungi mkono..
3. Wewe mbona sasa unaokuja na "
sweeping statements" tu za "
wamekosea" bila kuonesha makosa yao kwa kutumia vipengere vya mkataba huohuo vilivyoanishwa? Au unafanya propaganda hapa???
Sema sasa wamekosea nini au wapi na usahihi wake ni upi?
Je, ikitokea kutokana na tafsiri na uelewa ,wanachopinga kikawa sio kweli watakuja kuupinga waraka wao?
Wewe unaishi wapi?
Itokee wapi wakati mkataba uko wazi na karibu kila mtu mwenye akili ameshausoma na kujiridhisha pasipo kuwa na shaka kuwa, hiyo kitu ni takataka sio mkataba?
Mkataba huwa ni lazima uoneshe manufaa na wajibu wa Kila upande unsosaini mkataba huo. Huu pamoja mapungufu mengine meeeengi unampa Dubai Ports World manufaa yote kwa kutumia mali na rasrimali yetu wenyewe!!!
Je, licha ya yote kukiwa na faida katika uwekezaji huo watapinga waraka wao?
Ziko wapi?
Acha maneno matupu ya "
kukiwa na faida....". Ziwe wapi wakati mkataba wenyewe unajieleza na kujisemea??
Yote haya yanapaswa kuainishwa kwenye mkataba lakini hakuna popote tunapooneshwa kuwa tutapata faida hizi au zile zaidi ya maneno ya midomoni tu huku kilichosainiwa na kupitishwa ni kingine kabisa!
Sasa kama wewe unaziona hizo faida, waambie TEC kwa kuwaonesha kipengere hata kimoja kwenye mkataba kinachoainisha hizo faida.!!
Je, ikiitishwa kura ya maoni Leo, kujua wanaopinga na wanaokubali uwekezaji wapi wengi, na ikaonekana wanaokubali ni wengi watapinga waraka wao?
Thubutu..!
CCM si wajinga wajichome moto weyewe eti kwa kuitisha kura ya maoni kwa jambo ambalo wanajua fika kuwa halikubaliki na limekataliwa wananchi..!!
Ukitaka kuthibitisha hili hata kwa macho tu, fuatilia
reaction ya umati mkubwa wa wananchi uliokuwa unajitokeza ktk mikutano ya CHADEMA moja ya agenda ikiwa ni hii ya mkataba wa bandari za Tanganyika...
Watu wameshalikataa hili ndugu
KARLO MWILAPWA hata kama TEC isingetoa tamko lolote. Wenye macho na akili wameshaliona hili long time
Baraza la Maaskofu nao ni wanadamu wa kawaida, wanakosea katika mengi hata hili la waraka ni Moja ya makosa.
Kama wamekosea, basi shida yenu ni nini? Si wapuuzeni tu na muendelee na mission yenu?
Maaskofu wetu kupitia chombo chao cha TEC hajawajtoa
order kwa serikali bali kilichotolewa ni
ushauri tu ambao ndani yake una msimamo wao kuwa,
HAWAKUBALIANI MKATABA HUO wa kugawa rasrimali za Tanganyika Kwa waarabu wa Dubai kupitia kampuni yao ya DP World..
Serikali inaweza kuchukua ushauri huo au ikaendelea na mission yake halafu tutaonana mbele kwa mbele..!!