Hawamalizi, wanaendelea hadi form IV, yaani huo Mtihani wa darasa la sita utakuwa kama uli mtihani wa darasa la 4 au wa form 2.Miaka kumi au kumi na moja mtoto kamaliza
Na serikali hili hailioni kabisa kama wanaendelea kuzalisha tatizoBaada ya hapo wanaenda form one wakiwa watoto possibly watamaliza form four wakiwa bado wadogo.
Elimu za kujitegemea ni muhimu sana kwa mfumo wetu wa sasa.
Hao watoto watakuja kumaliza vyuo mapema waanze kusota kutafuta ajira mpaka wazeeke.
Kazi kweli kweli, halafu Form Four wanaofaulu vibaya kumbuka ndio wanakuja kuwa walinzi wa Raia na Mali zao.πππ Utakutana na mwajiriwa anamdekea boss wake
Elimu ya msingi ilitakiwa kuwa miaka 8 na iwe sawa na kumaliza form 2 ..... form 5 na 6 ni kupoteza muda na mali bure ..zifutwe .....BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA: DARASA LA TANO MWAKA HUU KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2027View attachment 3673224
Kwa mujibu wa taarifa ya Baraza la Mitihani la Tanzania, wanafunzi waliopo Darasa la Tano mwaka huu (2026) watamaliza elimu ya msingi mwaka 2027 wakiwa Darasa la Sita, wakati wanafunzi waliopo Darasa la Sita mwaka huu watakuwa kundi la mwisho kusoma hadi Darasa la Saba.
Taarif hii inanifanya mimi kama mzazi au mlezi nijiulize jambo muhimu sana kuhusu watoto wetu.
Kama mtoto wa Darasa la Tano leo atamaliza elimu ya msingi mwaka 2027 akiwa Darasa la Sita, atakuwa na umri gani wakati huo? atakuwa kashakwiva kucope mazingira na vishawishi mbalimbali sekondari, na je, atakuwa tayari kuingia sekondari?
Miaka yetu hii watoto wanawahi kuanza shule mapema sana unakuta kitoto kitoto kidogo kweli hata ubongo hujatanuka nacho kinamalkza form four sasa sipati picha wakianza kuletwa hawa wa la sita itakaje π
Kuna muda pia nakaa nawaza hivi serikali yetu imeshaweka mipango ya kuwapokea double cohort ya kundi ya darasa la 6 na la 7 kwa pamoja maana mwakani watafanya mtihani wa kumaliza pamoja
Kwani jamani watoto wetu wanawahishwa wapi?
Acha watu wamalize shule mapema mkuu. Unataka mtu amalize shule na miaka 27 then hajui Nini cha kufanyaWadogo mno ndo maana hata hili la la kuishia la sita linanishangaza kiukweli ,uzuri kila mtu kasoma sekondari anaelewa maisha na mazingira yalivyo
Na inapaswa kuwa hivi ,advance level ilinharibia ndoto yangu siwezi kusahau ππElimu ya msingi ilitakiwa kuwa miaka 8 na iwe sawa na kumaliza form 2 ..... form 5 na 6 ni kupoteza muda na mali bure ..zifutwe .....
MFUMO WA 8 + 4 +CHUO .ndiyo mfumo sahihi..
PRIMARY MIAKA 5....NA ADVANCE PRIMARY MIAKA 3
Dira ipo tatizo Dereva.Hatari sana hii nchi sijui haina DIRA