Baraza la sasa la Mawaziri halikidhi matarajio ya wananchi chini ya uongozi mpya wa Rais Samia

Baraza la sasa la Mawaziri halikidhi matarajio ya wananchi chini ya uongozi mpya wa Rais Samia

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Tupo kwenye zama mpya na kila zama na style yake.
Kwa hivi sasa wananchi wana matumaini makubwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwamba atakuwa ni rais atakeyekidhi matarajio yao ya maendeleo lakini pia atakuwa rais atakayeondoa mapungufu makubwa yaliyoonekana katika serikali iliyopita ya rais Magufuli yakiwemo, Kutoheshimu katiba, kutotenda haki ipasavyo, uonevu wa dhahiri, kugeuza bunge kuwa kikaragosi cha mtawala, ukopaji mkubwa sana na hivyo kuongezeka kwa deni la Taifa lililokithiri, kujaza Makada wa CCM kwenye nafasi za kitaalamu (rejea uDAS), Viashiria vya udini na Ukabila katika teuzi, kunyima wananchi haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa kupora chaguzi, kauli tata na chafu, kuharibu sekta binafsi, kuharibu maisha ya watu kwa kupora korosho na kuvuruga kilim cha mbaazi na Kahawa, na mambo mengi ya hovyo

Sasa katika mazingira ya aina hii si sahihi hata kidogo kwa raisi mpya kwenda na timu ileile, katika mtindo uleule ambao wananchi walionyesha kutokuwa na matarajio nayo.

Hivyo basi kutokana na sababu zifuatazo, Tunamtarajia Raisi Samia Suluhu Hassan afanye mabadiriko makubwa kwenye timu yake ya Mawaziri na Manaibu waziri ili aweze kupata Imani thabiti ya wananchi kuwa atakidhi matarajio yao.

1. Mosi, hiyo timu ya sasa si ya Rais Samia bali ni ya Rais Magufuli kwa kusaidiana na Kassim Majaliwa (Sijui alishirikishwa kiasi gani).

Katiba haimpi role Makamu wa Raisi kwenye kuunda baraza la mawaziri, bali inampa role hiyo Rais kwa kushirikiana na Waziri Mkuu, Kwa hiyo ni dhahiri hiyo timu siyo ya Rais Samia, bali imeundwa kulingana na vigezo vya kiutawala, haiba na mawazo ya Hayati Magufuli. Ili Samia aweze kuperform kwa kiwango tunachontarajia ni lazima ateue timu yake mwenyewe ambaye yeye anaiamini na sisi wananchi pia kuiamini kuwa kweli hii ni timu itakayoweza kuleta mabadiriko ya msingi lakini pia kubeba ajenda ya maendeleo. Timu ileile ya watu wale ambamo miongoni mwao kuna wababaishaji wengi na watu makini wachache haiwezi kukidhi matarajio yetu wananchi.

2. Baraza hili la sasa ni sura ya "divisiveness" (ukosefu wa mshikamano wa Kitaifa).

Haiwezekani uuende baraza la mawaziri la Tanzania nzima ambalo haliakisi demografia ya kitaifa, baraza ambalo halina Waziri hata mmoja kutoka Zanzibar, Lina waislamu watatu tu kati ya makumi ya mawaziri, lina wanawake wa kuangalizia kwa tochi, baraza ambalo kanda nyingine za nchi hakuna mtu, Hilo siyo baraza la kujenga umoja, mshikamano na Utaifa, hilo ni baraza kama la vikao vya harusi, ambapo hujali nani kaja kikaoni isipokuwa pesa tu zipatikane!. Tunataka baraza lenye sura ya Kitaifa ambalo halina viashiria vya Udini, Ukabila, Ukanda, Utanganyika au Uzanzibari

3. Hili baraza la mawaziri pamoja na manaibu wake liliundwa Strategically kwa sababu za kisiasa za Hayati na siyo kwa dira ya maendeleo ya Taifa

Ukiangalia hili baraza la sasa la mawaziri, limejaa watu waliokuwa vinara wa kujipendekeza kwa hayati, kuna watu humo ndani wameshatoa oda za kukamata wananchi eti kisa wanahoji wapi alipo kiongozi wao Mkuu wa nchi, kuna Manaibu Waziri humo walikimbia vyama vyao vya awali na kuha CCM kwa ahadi ya fedha na vyeo, Watu wa aina hii wa kununuliwanunuliwa siyo aina ya baraza la mawaziri na manaibu waziri tunaowahitaji chini ya Uongozi mpya.

Hapa rais Samia aache huruma kuwaangalia usoni wateule wa hayati kihurumahuruma, hii biashara si yake, hii ni biashara yetu sisi wananchi. Hatutaki viongozi wenye sura za unafiki, wanaonunuliwa nunuliwa na kubadili misimamo yao kwa ajili ya fedha na vyeo. Hawa walionunuliwa ili kuunga mkono juhudi hawa ndiyo aina ya watu ambao wanaweza kuingiza nchi katika mikataba yenye harufu ya ufisadi kwa sababu wana bei.

Kwa hiyo utaona kuwa Hayati aliunda baraza la ma "yesmen", watu atakaoweza kuwaburuza tu na ambao hawana guts za kusimamia misimamo yao tofauti. Sasa sisi hatuhitaji timu ya wanafiki wanaojali matumbo yao badala ya maslahi ya Taifa

4. Kuna mawaziri ambao kutokana na haiba yao na matendo yao ni heri wakawekwa benchi au wabadirishiwe wizara, hawaakisi Taifa la watu wanaojitambua au hawajatimiza wajibu wao ipasavyo

a) Yule waziri Comedian anayelisha viapo wafanyakazi wa ofisi yake, anayeuliza "wanaume mpo, sioni mwanaume hata mmoja hapa)

b) Yule waziri aliyetoa agizo la kukamata wananchi na kuwaweka ndani kisa eti wananchi wanahoji afya ya rais wao na kwamba yuko wapi? —Huyu pia ana rekodi ya kuwa na msimamo alioutoa bungeni kuwa watoto wenye mimba hawafai kuendelea na masomo kwenye shule za serikali

c) Yule Waziri ambaye Ulisema kama Kashindwa kazi basi asaidiwe, haiwezekani wizara yake ina underperform halafu abaki katika wizara hiyohiyo

Hata hivyo, kwenye kubadili mawaziri hakuna haja ya kumbadili Waziri Mkuu, licha ya kauli zake tata za hivi karibuni ambazo zina uongo mwingi ikiwemo, kudanganya umma juu ya hali ya afya ya rais na pia kuandaa maziko ya hayati ambayo aliyaendesha katika mrengo wa KiCCM bila kutambua uwepo wa viongozi wakuu wa chama kikuu cha upinzani nchini, na kuongopea Watanzania kuwa eti watu bilion 3.9 wamefuatilia msiba wa hayati kitu ambacho ni uongo dhahiri na mtu wa calibre yake hapaswi kuongopaongopa, Kiapo chake cha uwaziri mkuu kinamtaka kujiconduct kwa namba ambayo hatadhalilisha heshima ya kiti chake, Sasa uongo unadhalilisha heshima ya nafasi ya waziri mkuu.

Hata hivyo huyu tunaweza kuendelea naye kutokana kwanza, na gharama za kutunza mawaziri wakuu wastaafu na pili ni dhahiri anajitahidi kuchapa kazi. Ila kwa mawaziri na manaibu waziri, Bila mabadiriko katika timu hiyo sioni ni kwa namna wananchi wanaweza kuwa na matarajio na serikali hii ya Rais Samia Suluhu Hassan
 
Hilo suala la udini naona umelivalia njuga lakini nikuambie tu kuwa unachokitafuta utakipata.
Usiogope! kwenye mapungufu ni muhimu tuseme

Nimetaja mengi ikiwemo ukanda, ujinsia, ukabila ila wewe umeona hilo la udini tu, au wewe ni mnufaika wa teuzi za Magufuli zilizojaa udini na hivyo hutaki dhulma ya hivyo iondoke?

Mbona basi wale waliokuwa wakiona ukabila kwenye teuzi za hayati walikuwa wanazungumza na kukemea openly na hukuwasema ila inapokuja kwenye ishu ya udini unakuwa mbogo tukiukemea?
 
Wacheni raisi afanye atakacho kama katiba inavyomuelekeza majungu yenu na fitna yabaki huku mitandaoni!
 
Mtoa mada ulianza vzr sana lkn hapo kwenye udini ndo ukalikoroga.

Kuvuruga uongozi sasa ktk level yoyote sababu ya udini tu ni hatari sana !

Mimi nafikiri sehemu kubwa ya kuangalia ni ktk level ya wilaya na deputy ministers kwanza... what I call field officers wanao deal na issues za wananchi directly.. at times kabla ya kuwafikia ma DC na Ministers.

Nimependa mfano wako wa ma DAS...sijui wote lkn inaonekana sehemu nyingi hii nafasi imekuwa ya kuchomeka vidosho wa watu flan.... mfano check Ilala, Kinondoni au kigamboni to mention a few !!

Pia nakubaliana na wewe juu ya viherehere km DC wa Hai...dc yeye, ocd yy, dso yy, yaani kila kitu... na kutwa ktk media yy tu..kutafuta sifa !

RC mbeya pia, mbona mtu kama RC wa Simiyu yy kutwa utasikia yupo busy na issues za maendeleo ya watu sio ubabe wa kijinga jinga !
 
Maelezo marefu lakini msingi wa hoja yako ni udini!

Haya mengine ni viungo tu vya kukoleza udini!
Huna macho, jaribu kurudia kusoma tena
Humo yameandikwa mengi na nimekemea udini, ukabila, ukanda etc

Hivi kwa nini udini unapokemewa mnakuwa kwenye denial na kuwa wakali? au mnapenda teuzi zilalie watu wa dini moja?

Mbona watu wakikemea ukabila huwa hamuwashambulii kuwa ni wakabila?

Au mnanunufaika na upendeleo wa kidini kwa hiyo hamtaki huo mfumo wa kibaguzi ufutwe?
 
Mleta mada nahisi utakuwa mwalimu wa madrassa, napenda Rais awateue waislamu wote kwenye nafasi za mawaziri uridhike wewe na kundi lako ili taifa letu lipige hatua ya kweli kuelekea maendeleo, ni vigumu sana sisi kuendelea kama bado kuna watu wenye mawazo mgando kama yako.

Halafu unazungumzia Rais abadilishe watu, sioni kuna maana gani kubadilisha hao watu kama wale watakaokuja nao watatekeleza ilani ya chama chao ile ile, au labda hamu yako uone waislamu wenzio wakitekeleza hiyo ilani?

Mawazo yenu bado sana, mko nyuma ya wakati, badala mpiganie Katiba Mpya mnapigania waislamu wengi waingie kwenye baraza la mawaziri, kwani hao wakristu waliopo huko wananisaidia nini mimi ninaepambana na hali yangu kila siku mtaani?
 
Wananchi wanayo Matarajio ya JPM kupitia Mh Rais Samai SH hakuna mbadala wa hilo. Kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri ni chambo kilicho tiwa katika ndoana kinacho subiria kumnasa mtu kooni.
 
Mwanzo mlisema Wasukuma hawajosoma ndio maana teuzi nyingi waliachwa.

Ilikuwa kila teuzi Wachaga na Wahaya...kumbe ilikuwa ni ka mfumo.

Magufuli amekuja na kuwainua Wasukuma na Waha sasa mnalalamika...endeleeni tu huo Mlalamiko,,,zama hizo zilishaisha
 
Mleta mada nahisi utakuwa mwalimu wa madrassa, napenda Rais awateue waislamu wote kwenye nafasi za mawaziri uridhike wewe na kundi lako ili taifa letu lipige hatua ya kweli kuelekea maendeleo, ni vigumu sana sis kuendelea kama bado kuna watu wenye mawazo kama yako...
Hata akiteua Samia kwani watatoka mbinguni? mfumo ni mbovu na siyo watu
 
Huna macho, jaribu kurudia kusoma tena
Humo yameandikwa mengi na nimekemea udini, ukabila, ukanda etc

Hivi kwa nini udini unapokemewa mnakuwa kwenye denial na kuwa wakali? au mnapenda teuzi zilalie watu wa dini moja?

Mbona watu wakikemea ukabila huwa hamuwashambulii kuwa ni wakabila?

Au mnanunufaika na upendeleo wa kidini kwa hiyo hamtaki huo mfumo wa kibaguzi ufutwe?

Hoja hii umeonyesha rangi halisi ya udini ambao nimebainisha pale juu!

Ni wapi uliniona ninashabikia hoja ya ukabila?

Unasema tunanufaika na upendeleo wa kidini? Unajua mimi dini gani?
 
Mleta mada nahisi utakuwa mwalimu wa madrassa, napenda Rais awateue waislamu wote kwenye nafasi za mawaziri uridhike wewe na kundi lako ili taifa letu lipige hatua ya kweli kuelekea maendeleo, ni vigumu sana sis kuendelea kama bado kuna watu wenye mawazo kama yako.
Hata akifanya hivyo nitakuwa wa kwanza kuja hapa na kulaani kitendo hicho.

Hata hivyo hili Taifa bado lipo katika phase ya kusimika misingi yake, halijakomaa kama mnavyodhani. Kwa hiyo ili kujenga nchi imara lazima makundi yote makubwa kwa madogo yashirikishwe ipasavyo, kusiwepo Hali ya kulalia upande mmoja kwa kiwango kikubwa na cha kutisha. Kufanya hivyo ni kuweka precedence mbaya itakayobomoa misingi ya Taifa husika.

Haiwezekani kundi moja kubwa tu katika society liwe underrepresented, Yaani kila teuzi wao wa kuhesabu kwa manati, hii siyo sawa haikubaliki.

Leo nakuhakikishia Samia akiunda baraza kama alivyoliunda Magufuli humu ndani hapatakalika

kuweka watu 80% wa dini moja na only 20% wa dini nyingine katika almost nafasi zoooote za uteuzj huu ni Udini wa wazi na Namuomba Rais Samia asifanye hivyo kwenye teuzi zake na Alirekrbidhe hilo!
 
Hoja hii umeonyesha rangi halisi ya udini ambao nimebainisha pale juu!

Ni wapi uliniona ninashabikia hoja ya ukabila?

Unasema tunanufaika na upendeleo wa kidini? Unajua mimi dini gani?
Mimi sina tatizo hata wakiteuliwa dini moja sijui waislam au kabila moja, mi nachotaka ni maendeleo ya kweli na siyo haya maigizo ya miaka yote.
 
Nimeona Lissu leo amejipanga kuchafua nchi .

Yani Mkenya PLO Lumumba amejipanga kuitetea Tanzania lakini mzaliwa wa Singida Tundu Lisu anajipanga kuchafua.

Ni aibu kubwa kwa taifa letu

Lisu ni makamu mwenyekiti hewa wa Chadema mnalipa mshahara wa bure
 
Back
Top Bottom