Mleta mada nahisi utakuwa mwalimu wa madrassa, napenda Rais awateue waislamu wote kwenye nafasi za mawaziri uridhike wewe na kundi lako ili taifa letu lipige hatua ya kweli kuelekea maendeleo, ni vigumu sana sisi kuendelea kama bado kuna watu wenye mawazo mgando kama yako.
Halafu unazungumzia Rais abadilishe watu, sioni kuna maana gani kubadilisha hao watu kama wale watakaokuja nao watatekeleza ilani ya chama chao ile ile, au labda hamu yako uone waislamu wenzio wakitekeleza hiyo ilani.
Mawazo yenu bado sana, mko nyuma ya wakati, badala mpiganie Katiba Mpya mnapigania waislamu wengi waingie kwenye baraza la mawaziri, kwani hao wakristu waliopo huko wananisaidia nini mimi ninaepambana na hali yangu kila siku mtaani?