Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Baraza la Wazazi la Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga limeishauri Serikali kutoa mwongozo wa namna bora ya matangazo ya biashara za nguo za ndani za wanawake kwa kutumia midoli ambayo imetajwa kuchochea mmonyoko wa maadili katika Jamii.
Ushauri huo umetolewa na Baadhi ya Wajumbe wa Baraza hilo akiwemo John Manyirizu na Mihayo Mdima wamesema ipo haja kwa Serikali kudhibiti biashara ambazo zinakiuka maadili ya Kitanzania kama vile uuzaji wa nguo za ndani za Wanawake kwa kutumia midoli ambayo imekuwa ikiwekwa nje ya maaduka.
Awali akichangia mjadala huo kuhusiana na maadili Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kahama, Charles Lutonja amesema baraza hilo linadhima ya kuishauri Serikali pindi lipoona kuna viashiria vya uvunjifu wa maadili unachangiwa na utandawazi huku Mboni Mhita Mkuu wa wilaya ya Kahama akiwataka Wazazi kuwa mstari wa Mbele katika Malezi.