Tetesi: Barcelona wamepanga kuweka dau kubwa la kutaka kumnunua tena Messi

Tetesi: Barcelona wamepanga kuweka dau kubwa la kutaka kumnunua tena Messi

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,503
Reaction score
15,858
Barcelona wamepanga kuweka dau kubwa la kutaka kumnunua tena Lionel Messi kabla ya msimu wa 2026/27, kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini Argentina.

Messi alihudumu Barcelona kwa zaidi ya miongo miwili huko Catalonia kuanzia mwaka 2000 mpaka msimu wa joto wa 2021, akijiunga na Paris Saint-Germain kwa uhamisho wa huru baada ya miamba hao wa Uhispania kukosa njia ya sahihi ya kumpatia mkataba mpya.

Mshindi huyo mara nane wa tuzo ya Ballon d'Or ametumia mwaka mmoja na nusu akiwa na Inter Miami kwenye Ligi Kuu ya Soka Marekani (MLS), huku kukiwa na tetesi kwamba Messi anaweza kurejea Barcelona, kulingana na TNT Sports Argentina.

Miamba hao wa Kikatalani wanasemekana kuwa na mpango wa kumsajili nyota huyo kwa mkataba ambao utakuwa na "idadi kubwa ya masharti" mara baada ya Kombe la Dunia 2026 akiwa na umri wa miaka 39.
 
Labda wanataka aje asitafie hapo Bacca baada ya kuondoka kwa aibu na fedheha.

Kumbuka Lapulga ndiye mfalme wa muda wote pale Camp Nou ila aliondoka kwa machozi badala ya furaha.
 
Labda wanataka aje asitafie hapo Bacca baada ya kuondoka kwa aibu na fedheha.

Kumbuka Lapulga ndiye mfalme wa muda wote pale Camp Nou ila aliondoka kwa machozi badala ya furaha.
Mmmmh, kwa aibu na fedheha tena? 🤔
 
Halafu huyu Messi si anatajwa kuwa alikanyaga jezi ya Barcelona aliyorushiwa na shabiki mmoja wakati akielekea kwenye vyumba vya Wachezaji wa Inter Miami? Japo hilo si ilisemekana liliwakera Mashabiki wa Barcelona?
 
Ni vizuri kama akaja kumalizia soka lake Barca.

Karibu Messi.
 
Halafu huyu Messi si anatajwa kuwa alikanyaga jezi ya Barcelona aliyorushiwa na shabiki mmoja wakati akielekea kwenye vyumba vya Wachezaji wa Inter Miami? Japo hilo si ilisemekana liliwakera Mashabiki wa Barcelona?
Propaganda tu hizo mkuu
 
Back
Top Bottom