Bariadi: Wanafunzi wavunja masomo na kuzuia Msafara wa Mbowe, wampigia Saluti

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Tulishasema tangu awali kwamba kwenye harakati za kisiasa, yapo mambo madogo madogo ama tuvitu vitu fulani twa kusisimua sana lakini hatupewi Airtime.

Sasa kwenye maandamano yanayoendelea watoto wa shule baada ya kusikia Mbowe anavurumisha maandamano kwenye eneo lao wakaamua kuvunja masomo na kuingilia msafara wake wakamzuia ili awape neno kuhusu Madawati na baadaye wakampigia Saluti Kabambe na kuahidi kuunga mkono Maandamano hayo.

Ushahidi huu hapa.

 
Kumbe Kuna maandamano? 😁😁
 
Siasa bana,

Ingekuwa wamefanya CCM, mngesema watoto wamelazimishwa,

Mkifanya nyie, CDM inapendwa,

Anyway, in short, watoto wameonekana kufurahia zaidi kuonana na kamanda Mbowe kuliko wale waigizaji wa CCM!!

Ukisimamia HAKI, una kibali Toka juu,

Mbarikiwe🙏
 
Mwalimu mkuu wa hiyo shule ameyakanyaga ajiandae kwa lolote
Ccm wana watoto wa chipukizi kama hao nchi nzima , mwalimu hana kosa na wanamabadiliko huanzia utotoni, sera za ccm kupiga marufuku siasa mashuleni na vyuoni wakati wao wanafanya siasa huko ni ushamba wao wenyewe kama walivo miaka yote
 
Ni kweli kwamba ccm inaandaa waraka wiki nzima wa kusitisha masomo ili wanafunzi wakampokee Nchimbi Lakini Chadema inakimbiliwa
 
Mmeanza kutumia wanafunzi kuwapotezea muda wa masomo hilo ni kosa wizara ya elimu iliangalie hilo na ikemee vikali!
 
Kwahiyo Mbowe kaagiza wakuu wa Shule wafunge shule waje kuandamana?
 

Hiki kweli chama cha mioyoni mwa waTanzania, angalia wananchi wanavyoonesha upendo na matumaini ya kweli kwa chama CHADEMA kinachosimamia Maendeleo ya Watu ili kuondoa umasikini, sera za kupambana na ugumu wa maisha, kupigania bima ya afya kwa wote n.k

Sera za CHADEMA maendeleo ya Watu zinazogusa maisha ya raia badala zile za magari ya kifahari ya viongozi wa chama dola kongwe CCM ambayo ni Maendeleo ya Vitu yanayogusa maisha ya wachache watumbua nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…