Barmaid amenisimulia 'take home' yake kwa mwezi na maisha anayoishi mpaka nimejiona fala na degree yangu Halmashauri

Barmaid amenisimulia 'take home' yake kwa mwezi na maisha anayoishi mpaka nimejiona fala na degree yangu Halmashauri

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Ajira za kuajiliwa za hovyo sana wakati mwingine.
Serikali mishahara midogo sana.

Unaenda benki mara 1 umeshakatika kabla hata ya tarehe 30.
Moshi mjini kuna kijiwe kinaitwa 'Red Stone'. Kipo njia ya Arusha mkabala na ukumbi mmoja maarufu sana uitwao Kuringe social hall.

Mdada analipwa mshahara wake safi wa kawaida halafu kila units za vinywaji anazohudumia kuna commission yake. Nauli ya kwenda na kurudi home wanapewa na msosi wanapewa.

Walevi wakishalewa huwa wana kautaratibu ka kukeep chenchi sana na kusahau masalia ya pesa. Kwakuwa yeye yupo strategic unakuta hela anayokusanya kwa mwezi ni nyingi kuliko wewe mwajiriwa wa Halmashauri idara ya kilimo na uhandisi wako wa hovyo.

Ana gheto safi. Mtoto anaenda shule na anavaa na kula vizuri bila mawazo ya buku 7. Mabar maid ambao wako strategic na wako vijiwe vizuri wanapiga sana hela. Siyo lazima awe malaya.

Fuatilia mabar mad mijini wanaishi maisha gani. Hamna mwenye hali ngumu.
 
Ukitaka kujua vipato vya watu vitakuhangaisha mkuu mie nna mchepuko wangu una biashara juzi kaniambia anamiliki sio chini ya milion 50 ambazo mie kuzifikia naona kama ndoto, nlisomaga nae akaishia la saba mie nkapiga mpaka mlimani yaani natamani kukimbia kazi
 
Mkuu ukitaka pia ujione fara na maandazi nenda stend yoyote ya daladala Dar jamaa huwa wana chukua 200 kila gari akipakia sasa jiulize kwa siku ana toka na shilingi ngapi?
 
Ukitaka kujua vipato vya watu vitakuhangaisha mkuu mie nna mchepuko wangu una biashara juzi kaniambia anamiliki sio chini ya milion 50 ambazo mie kuzifikia naona kama ndoto, nlisomaga nae akaishia la saba mie nkapiga mpaka mlimani yaani natamani kukimbia kazi

Mkuu umenena vema kabisa. Ukifuatilia kipato cha mtu unaweza kufa kabla ya muda wako. Mimi mwenyewe pamoja na MSc yangu laikini wapo jamaa zangu wengi tu niliowaacha darasa la saba wameniacha mbali tu lakini sikati tamaa naendelea kukomaa.
 
Back
Top Bottom