Barua nzito ya kijana Mkatoliki kwa Maaskofu yazua Gumzo

Barua nzito ya kijana Mkatoliki kwa Maaskofu yazua Gumzo

Naona leo kwenye makundi yenu ya WhatsApp ya elf 7, 7 mmekubaliana mje humu kuanzisha nyuzi za kupinga kanisa kwa tamko lake la kuzuia mambuzi kwenye miambali ya kanisa. Kazi mnayo 😄
Wamesha shindwa hawawezi pambana na kabisa wakashinda!!
 
We mjinga n
Kijana mmoja Mkristo Mkatoliki ameandika barua ya wazi kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) akieleza masikitiko yake juu ya kile anachokiona kuwa ni kuingizwa kwa Kanisa katika mijadala ya kisiasa.

Katika barua hiyo iliyojaa maneno makali ya kiimani na rejea nyingi za Maandiko Matakatifu kijana huyo amehoji iwapo kweli viongozi hao wanamfuata Kristo ambaye hakuwahi kushiriki siasa wala kushabikia harakati za madaraka licha ya kuishi chini ya utawala dhalimu wa Kirumi.

Amenukuu maneno ya Mtume Paulo kuhusu mamlaka za serikali kuwekwa na Mungu na kuonya kuwa Maaskofu wanapoteza dira yao ya kiroho kwa kuruhusu Kanisa kujiingiza katika mapambano ya kidunia.

“Je, mnamfuata Kristo yupi? Au mmeona haya kuishi mfano wa Kristo kwa kuwa watu watawacheka?” anauliza kijana huyo kwa uchungu akihoji misimamo ya baadhi ya viongozi wa Kanisa wanaotoa kauli zenye mwelekeo wa kisiasa.

Amehitimisha kwa kuwataka Maaskofu wa TEC warudi katika msingi wa kazi yao kuhubiri kufundisha na kusimamia maadili na waepuke kuwa chombo cha propaganda kinachotumiwa kwa malengo ya muda mfupi ya kisiasa.

Barua hiyo imesambaa kwa kasi mitandaoni na imezua maoni mseto kutoka kwa waumini na wachambuzi wa masuala ya dini na jamii
aona unataka watu waanze kutukuna waislamu na waislamu kwa kuleta mada zako za kijinga humu
 
Naona leo kwenye makundi yenu ya WhatsApp ya elf 7, 7 mmekubaliana mje humu kuanzisha nyuzi za kupinga kanisa kwa tamko lake la kuzuia mambuzi kwenye miambali ya kanisa. Kazi mnayo 😄
Hivi bei haijapanda? Bado ni buku saba fc??
 
Acha fix, hizo propaganda za CCM - Kanisa huwa na msimamo mmoja tu - na msimamo wa Kanisa hadi leo ni kwamba Reforms zifanyike kabla ya Uchaguzi. Sasa huwezi pandikiza mgogoro ndani ya kanisa unajidanganya.
 
Fafanua zaidi tukuelewe!

Back
Top Bottom