Barua ya Dani Alves baada ya kutengana kwa Joana Sanz

Barua ya Dani Alves baada ya kutengana kwa Joana Sanz

Ni mkewe kumbe?? Maskini afu atataka apewe talaka wagawane mali[emoji22][emoji22][emoji22]
Three quarters of footballers/athletes get divorced after retirement.

Possibly mkewe ndio kacheza dili kamchomekea mwanamke nae kaingia laini kumbe mke keshachungulia mbali kisha aanzishiwe kesi ya ubakaji ili iwe scapegoat ya kuombea talaka wagawane mali kwisha habari si kaingia kwenye 18 na career yake imeisha, wachezaji wa nje career yao ikiisha hata mikataba inapungua na umaarufu unashuka,hapo sasa kama mwanamke alifuata mali na umaarufu ili afanye nae dili zake kama biashara au apate mikataba ya mitindo vikishuka anaona hapa sasa biashara hakuna bora liwalo na liwe atokomee mbali mgawane kilichopo aende kwa ampendae.

Ref case study: Francisco Totti once alipo staafu tu mke akaanza mapicha picha ndoa chali, Thierry Henry, kuna yule Wanda Nara kwa mumewe wa kwanza na wa pili kaona career zinaelekea mwisho anazingua, bado mke wa Ebue pia,Tiger Wood,Tyson, Rafael van der vaart, Lineker nk

Ndio maana baadhi ya athletes kama hawataki kuoa wanajua wamezungukwa na wanawake ambao sio wakweli.
Ukiwa na pesa kumpata mwanamke mwenye upendo wa kweli kabisa ni ngumu sana sijui kwanini [emoji26]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Barua ya beki, Dani Alves aliyomwandikia aliyekuwa mke wake Joana Sanz imefuchuliwa lakini beki huyo akiendelea kusota jela kufuatia kesi ya ubakaji inayomkabili.

Beki huyo wa zamani wa Barcelona, aliandika barua hiyo akiwa jela ya ‘Brian 2’ iliyopo Hispania akishikiliwa kwa mashtaka ya unyanyasaji wa kijinsia. Imeelezwa Alves aligoma kula baada ya mwanamitindo huyo kutangaza rasmi ameachana na mwanasoka huyo kutokana na madai yanayomkabili.

Alves anakabiliwa na kesi ya kumshambulia mwanamke bafuni kabla ya kumbaka, baadaye mwanamke huyo ambaye hakufahamika jina alimripoti polisi na kukamatwa, tukio hilo lilitokea Desemba 31 mwaka jana.

Nyota huyo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Brazil, alichanganyakiwa baada ya ndoa yake kuvunjika kwa
mujibu wa ripoti. Spanish TV ilisema barua hiyo imefichuliwa baada ya Joana kutangaza rasmi ndoa yake na beki huyo imevunjika rasmi kupitia akaunti yake ya Instagram.
.
Hii hapa barua ya Alves aliyomwandikia aliyekuwa mke wake

“Kipenzi changu Joan, imepita miaka minane sasa ya upendo wetu na heshima. Miaka ya nyuma mambo yetu yalikuwa mazuri na yenye furaha, wewe na watoto wangu (Dani Filho na Victoria), Tumekua pamoja tangu siku tulionana, tumeongozana pamoja kwa jambo lolote, tulipitia magumu mimi na wewe, nasikitika umeivunja ndoa yetu, nitaomba kila siku unipe nafasi nyingine ya kukupenda tena, naelewa maumivu unayopitia, nitaendelea kupambana kwa ushirikiano wa familia yangu, ukweli utagundilika na dunia itafahamu.”

View attachment 2565247
Mwanamke akishakuzidi urefu tayari ni tatizo kubwa
 
Visca Barca, chama langu dah....! Alikuwa dependable player wetu kwa muda mrefu.
Kesi za sexual abuse, sexual harassment, rape na nyinginezo za aina hiyo huwa zinagubikwa na utata mwingi hata ushahidi wake huwa una utata. Mnaweza kukubaliana ile umekojoa tu demu anatoka na ushahidi wake(sperms) anenda kukugeuza dili.
Wanawake watu wabaya sana basi tu tunaishi nao
 
Ninyi mnaover look hili jambo. Kama ni issue ya mali angeweza kuomba talaka hata kabla ya mumewe kuwa na hiyo kesi na angepata migao yake vizuri tu, sote tunajua suala la talaka kwa wenzetu sio nongwa kama huku.

Kwa wenzetu mtu Maarufu akiwa na kesi ya unyanyasaji wa watoto, unyanyasaji wa wanawake, ubakaji, unanyanyasaji wa wanyama, Ugaidi na human trafficking, ubaguzi wa rangi, na kwasasa hivi ubaguzi dhidi ya hawa LGBTQ huwa anakuwa cancel na kila, hakuna mtu/taasisi inayotaka kuhusishwa na mtuhumiwa wa hivyo au a convict.

Hakuna mtu ambaye ana jina atataka kuhusishwa na wewe au kukutetea hadharani na yeye akiogopa kucanceliwa kwa kuonekana anayeyemtetea au kuside naye pengine na yeye ana tabia iko hivyo hivyo.

Kama huyo mke ana career yake jua hawezi kurisk career kwa kuonekana anaside na mumewe ambaye ni mtuhumiwa (sifahamu hii kesi vizuri nazungumzia uzioefu) Kuna madhara ya huyo mkewe kuside na mumewe wakati kama huu, to make the matter worse he cheated on her! 😅

Msimlaumu sana huyo dada, system za kidunia hazifanyi kazi hivyo, Watu maarufu wakipatwa na kesi za hivi chunguzeni vizuri wanaowatetea ni watu wa kawaida (common wananchi) ambao hawana chakupoteza, ambao wana vya kupoteza hujitenga nao kabisa. Vyakupoteza namaanisha Gigs, shows, endorsements, mikataba etc.

Atleast hivi ndivyo mimi ninavyofikiri, naomba kukosolewa.
 
Back
Top Bottom