Barua ya Julius Nyerere ya kujiuzulu ualimu St. Francis College Pugu 1955

Unazo, Sheikh wangu, kama sikosei umekinukuu hicho kitabu ndani ya kitabu chako cha Abdulwahid Sykes cc: Joka Kuu

Mohamed Said,

..bahati mbaya nimesahau title ya kitabu ambacho inasemekana kina barua ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa Kanisa Katoliki.

..lakini kwa kumbukumbu zangu kitabu hicho kimekuwa kikinukuliwa na wanazuoni mbalimbali wa Kiislamu hapa nchini akiwemo Ustaadh Ilunga Kapungu. Aliyeandika kitabu hicho ana jina la Kidachi au Kijerumani.

.. Companero unaweza kutusaidia title ya kitabu pamoja na jina la mwandishi?
 
JK,


Jan P van Bergen​
 

..asante sana Sheikh.

.. Companero ndiyo alinidokeza kuhusu kuwepo kwa barua ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa Kanisa Katoliki.

..Na aliahidi kuileta barua hiyo hapa JF lakini hajatimiza ahadi yake mpaka leo.

..Na kama sijakosea nadhani alisema barua hiyo ipo ktk kitabu cha Van Bergen.

..naomba utusaidie kuangalia kama barua tunayoifuta ipo ktk kitabu hicho hapo juu.
 

Sio kwel,i Abdulwahid Sykes hakuwahi kwenda UNO kwa niaba ya WATANGANYIKA kudai uhuru acheni kupotosha historia!!! Kulikuwa na wasoni wengi wakati tuo kama wakina John Keto ,kwanini ikawa Nyerere pekee ndio akubalike kwenda kujenga hoja ya Tanganyika UNO ili nchi ipate uhuru? Sababu ni moja tu nayo ni kukubalika kwake na wale aliokuwa anawaongoza!!! Hao wakina Fuundikira hawakuwa na karama hiyo na ilikuja kudhihilika hata baada ya UHURU kwa Said Fundikira kupatikani na hatia ya kupokea RUSHWA akiwa Waziri wa sheria!!!
 

Mwombe aangalie kule mwisho kwenye maambato/viambatanisho, kama kumbukumbu zangu bado siko sahihi, ipo huko
 
je Nyerere ndio wa kwanza kwenda UNO?
 
je Nyerere ndio wa kwanza kwenda UNO?

Nyerere alikuwa wa kwanza kuwawakilisha WATANGANYIKA wote!!! Chief Thomas Marealle wakati huo Mangi Mkuu wa wachaga aliwahi kupelekwa na wazungu katika mbinu zao za kuigawa nchi!!!
 
Mohamed Said,

.. hebu angalia kwenye viambatanisho vya kitabu cha Van Bergen kama kuna barua ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa Kanisa Katoliki. I am told it is a very interesting letter, tutafurahi kama utaweza ku-share na sisi.

cc Companero
 
Nyerere alikuwa wa kwanza kuwawakilisha WATANGANYIKA wote!!! Chief Thomas Marealle wakati huo Mangi Mkuu wa wachaga aliwahi kupelekwa na wazungu katika mbinu zao za kuigawa nchi!!!
WATU WA CHAMA ndio namaanisha achana na makabila
 

Vitabu vyako nanunua Masjidi manyema
 
H
Hawa mama zetu walikuwa na ushujaa usio na kifani cha kuweza kumsindikiza mwalimu bila ya kumuogopa mwingereza ila ninasikitika sana haya hayaongelewi sana.
 
H
Hawa mama zetu walikuwa na ushujaa usio na kifani cha kuweza kumsindikiza mwalimu bila ya kumuogopa mwingereza ila ninasikitika kuwa haya hayaongelewi sana.
 
Sasa chama cha kiisilamu alafu mkatoliki ndo wamempa mpini,,mkatoliki kabisaa,akubakize
 
Sasa chama cha kiisilamu alafu mkatoliki ndo wamempa mpini,,mkatoliki kabisaa,akubakize
B...
TANU ilikuwa nationalist-secularist party ila ilikuwa imetawaliwa na wanachama na viongozi Waislam hadi kufikia Kura Tatu mwaka wa 1958.

Wazee wetu wakiongozwa na Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa mufti wa Tanganyika walijitahidi sana kuijenga TANU katika msingi wa kuwaunganisha wananchi wote wa Tanganyika kudai uhuru kwa umoja wao.
 
Historia yetu imepotoshwa mno.
Baba yangu mkubwa ambaye alikua, na kulelewa na kanisa tangu akiwa mdogo tangu mwaka 1941.
Miaka ya 1995 alipendamulia historia ya Tanganyika na kutueleza kuwa ina uongo kwa 86% na ukweli baada ya kujifunza na kupitia sehemu mbalimbali kuna uongo mwingi.
Leo hii. Mohamed Said. Umenisaidia kufanya hitimisho kuupata ukweli dhahiri.
Tegemea utapata upinzani kwa wale wavivu wa fikra lakini jitahidi kutupa ukweli tujifunze zaidi huenda siku moja taifa hili kitaandika historia ya kweli na kuacha urithi wa historia isiyotia shaka.
Mungu akubariki.
 
Kwa hiyo kura tatu ya tabora ndo iliwaweka kando waasisi wa tanu akina muft Ameir na wenziwe.

Lkn pia la ziada baada ya mwalimu kupata uhuru wa tanganyika na kua rais ulitaka mwalimu awape nini wale waanzilishi na waasisi wa tanu,,?
 
Kwa hiyo kura tatu ya tabora ndo iliwaweka kando waasisi wa tanu akina muft Ameir na wenziwe.

Lkn pia la ziada baada ya mwalimu kupata uhuru wa tanganyika na kua rais ulitaka mwalimu awape nini wale waanzilishi na waasisi wa tanu,,?
B...
Umekosea kumtaja Sheikh Hassan bin Ameir.
Sheikh Hassan hakuwa ameshika nafasi yoyote katika chama.

Wala Sheikh Hassan hakuwa na mwenzie katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mwenzie kama alikuwepo ni Nyerere.

Sheikh Hassan alikuwa kiongozi bila ya kushika nafasi ya uongozi.

Wengi wenu hamjui nafasi ya Sheikh Hassan bin Ameir katika siasa za Tanganyika hadi Tanzania.

Sheikh Hassan bin Ameir alikuwapo katika mpango wa kuunda TANU toka mwaka wa 1950 akiwa mjumbe wa TAA Political Subcommitee.

Nakuwekea hapo chini mada niliyotoa Zanzibar University kuhusu Sheikh Hassan bin Ameir mpate kumjua.

Swali la pili kuwa Mwalimu awape nini waasisi wa TANU sijui kwa nini unauliza swali hili sidhani kama waasisi walikuwa wanataka kupewa kitu.

Hapa nawasemea waasisi ambao mimi nawajua vyema toka wako hai hadi walipofariki.
Sikupata kuwasikia wakisema kuwa hawakupewa kitu.

Nilichokisikia mara nyingi wakisema ni kuwa historia ya TANU inavurugwa na kupotoshwa.
Nakumbuka maneno ya Mzee Germano Pacha aliyoniambia katika mahojiano yetu wakati wa utafiti wa kitabu.

Mzee Pacha alisema kama si kuwapo ile picha ya waasisi wa TANU kungekuwa na waasisi wengi hivi sasa.

 
Impongo,
Ahsante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…