Mangungo II
JF-Expert Member
- Jul 6, 2012
- 18,133
- 26,766
Akili tuKiliwakuta nini hao waislamu waliounda Chama afu nchi akachukua mkristo?
Walipigwa chenga ya akili
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Akili tuKiliwakuta nini hao waislamu waliounda Chama afu nchi akachukua mkristo?
Unazo, Sheikh wangu, kama sikosei umekinukuu hicho kitabu ndani ya kitabu chako cha Abdulwahid Sykes cc: Joka Kuu
JK,Mohamed Said,
..bahati mbaya nimesahau title ya kitabu ambacho inasemekana kina barua ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa Kanisa Katoliki.
..lakini kwa kumbukumbu zangu kitabu hicho kimekuwa kikinukuliwa na wanazuoni mbalimbali wa Kiislamu hapa nchini akiwemo Ustaadh Ilunga Kapungu. Aliyeandika kitabu hicho ana jina la Kidachi au Kijerumani.
.. Companero unaweza kutusaidia title ya kitabu pamoja na jina la mwandishi?
Nyerere sio wa kwanza kwenda UNO kwa taarifa tu, Sykes alishaenda huko na kupewa masharti hayo aliporudi akawajulisha wazee then wakakaa kujadili watampata wapi huyo muRC ndipo Fundikira alipowaambia kuna dogo mmoja nimemuacha kule Makerere nadhani atafaa.
..asante sana Sheikh.
.. Companero ndiyo alinidokeza kuhusu kuwepo kwa barua ya Mwalimu Nyerere kwenda kwa Kanisa Katoliki.
..Na aliahidi kuileta barua hiyo hapa JF lakini hajatimiza ahadi yake mpaka leo.
..Na kama sijakosea nadhani alisema barua hiyo ipo ktk kitabu cha Van Bergen.
..naomba utusaidie kuangalia kama barua tunayoifuta ipo ktk kitabu hicho hapo juu.
je Nyerere ndio wa kwanza kwenda UNO?Sio kwel,i Abdulwahid Sykes hakuwahi kwenda UNO kwa niaba ya WATANGANYIKA kudai uhuru acheni kupotosha historia!!! Kulikuwa na wasoni wengi wakati tuo kama wakina John Keto ,kwanini ikawa Nyerere pekee ndio akubalike kwenda kujenga hoja ya Tanganyika UNO ili nchi ipate uhuru? Sababu ni moja tu nayo ni kukubalika kwake na wale aliokuwa anawaongoza!!! Hao wakina Fuundikira hawakuwa na karama hiyo na ilikuja kudhihilika hata baada ya UHURU kwa Said Fundikira kupatikani na hatia ya kupokea RUSHWA akiwa Waziri wa sheria!!!
je Nyerere ndio wa kwanza kwenda UNO?
WATU WA CHAMA ndio namaanisha achana na makabilaNyerere alikuwa wa kwanza kuwawakilisha WATANGANYIKA wote!!! Chief Thomas Marealle wakati huo Mangi Mkuu wa wachaga aliwahi kupelekwa na wazungu katika mbinu zao za kuigawa nchi!!!
Mkuu wa Kijiji,
Ahsante sana.
Siku zote mimi hujiuliza ingekuwaje laiti kama Kleist Sykes asingeleiandika maisha yake na katika mswada ule asingelieleza historia ya African Association.
Nani leo angelijua historia ya TAA na historia ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika vyama viwili ambavyo vilikuja kutoa uongozi katika TANU na kuingiza wanachama wengi wa mwanzo.
Wazee wetu wametuachia picha nyingi sana za harakati za uhuru na hizi nimeziweka hapa mara nyingi tu kwa faida ya wasomaji.
Salute mzee wangu. Je nikitaka kununua vitabu vyako nitavipata wapi?
Hawa mama zetu walikuwa na ushujaa usio na kifani cha kuweza kumsindikiza mwalimu bila ya kumuogopa mwingereza ila ninasikitika sana haya hayaongelewi sana.
Nimeletewa barua ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kujiuzu kazi ya ualimu, aliyeniletea bila shaka akidhani siijui barua hii.
Nimeamua kumwandikia kumpa fikra zangu na kumweleza historia nzima ya barua hii ambayo inaitwa ''Uamuzi wa Busara.'':
''Hii barua ni maarufu ila kilichopungua ni vipi Mwalimu Nyerere alifikia katika uamuzi mgumu kama huu wa kuacha kazi na kuamua kuwa mtumishi wa TANU chama kichanga cha siasa kilichoasisiwa miezi minane tu iliyopita.
Chama ambacho kilikuwa kikiendeshwa kutoka fedha za wafadhili wake wanne: John Rupia, Waziri Dossa Aziz na ndugu wawili Abdulwahid na Ally Sykes.
Bahati mbaya barua aliyoandikiwa Mwalimu na mwajiri wake hapa haipo lakini nayo pia ni barua maarufu.
Toka alipochaguliwa kuwa Rais wa TAA tarehe 17 April 1953 mkakati uliokuwa umepangwa na Hamza Mwapachu na Abdul Sykes ilikuwa ni kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.
Sasa haikutegemewa kuwa Rais wa TANU atadai uhuru wa Tanganyika akiwa mfanyakazi wa Kanisa.
Huu ulikuwa muhali mkubwa na hili viongozi wa TANU wakilijua na Abdul na Nyerere walishalizungumza kabla na ukweli ni kuwa kabla ya safari ya kwanza ya UNO Februari 1955, Nyerere alitaabika sana na fikra ya kuacha kazi.
Ujasiri wa kuacha kazi Mwalimu hakuupata kwa kule kuzingirwa na watu wenye uwezo hawa viongozi na wahisani wakubwa wa TANU.
Ujasiri wa kuacha kazi aliupata siku aliporudi UNO na akapokewa na umma ambao ulikuwa haujapatapo kuonekana Dar es Salaam.
Siku ile ndiyo Nyerere alitambua kuwa ana watu wanaomuunga mkono na wana mapenzi ya kweli na yeye na TANU na wanataka kuwa huru na wamemkubali yeye kama kiongozi wao.
Kwa upande wa serikali ya Gavana Edward Francis Twining walitanabai ule ukweli kuwa sasa siku zao Tanganyika zilikuwa zinahesabika.
Kwa upande wa mwajiri wa Mwalimu Nyerere, yaani Kanisa iliwadhihirikia kuwa mtumishi wao alikuwa amewasababishia mgongano mkubwa sana wa maslahi kwani Kanisa na Serikali walikuwa na ushirikiano mkubwa katika kuitawala Tanganyika.
Kubwa zaidi lililowashangaza ni kuwa ni ile jamii waliyokuwa wameinyima elimu kwa hila za ukoloni za wagawe uwatawale.
Waislam wameunda chama na kumweka kiongozi Mkatoliki aongoze mapambano ya kuikomboa Tanganyika.
Mkakati huu ulikuwa na maana gani?
Mwalimu alikuwa alama ya umoja na alama ya kuwaita walio mfano wa yeye kuingia TANU na kuunga mkono juhudi za kudai uhuru wa Waafrika wa Tanganyika.
Barua ile aliyoandikiwa Nyerere na mwajiri wake ilisomwa na Abdul Sykes mtu aliyekuwa karibu sana na Nyerere na Abdul alisisitiza kuwa Nyerere aache kazi lakini barua ile akapendekeza ijadiliwe na Halmashauri Kuu ya TANU chini ya Mwenyekiti Clement Mohamed Mtamila na ilikuwa nyumbani kwake Mtamila ndipo barua ile ilipojadiliwa na uamuzi ukawa Nyerere aandike barua ya kujiuzulu kazi.
Nyerere aliandika barua ya kujiuzulu na akaja mjini Dar es Salaam sio mwalimu wa shule tena na kwa muda akaishi nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey na Sikukuu.
Katika Halmashauri Kuu ya TANU mmoja kati ya wajumbe wale alikuwa Tatu bint Mzee.
Yapo mengi sana katika historia ya TANU na historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo wengi hawayajui.
Picha ya kwanza juu ni barua ya Mwalimu Nyerere na picha ya pili hapo chini ni wa kwanza kulia ni Bi. Tatu bint Mzee akifuatiwa na Bi. Titi Mohamed na wa kwanza kushoto ni Bi. Chiku bint Said Kisusa wakimsindikiza Julius Nyerere Uwanja wa Ndege safari ya kwanza UNO.
Hawa mama zetu walikuwa na ushujaa usio na kifani cha kuweza kumsindikiza mwalimu bila ya kumuogopa mwingereza ila ninasikitika kuwa haya hayaongelewi sana.

B...Sasa chama cha kiisilamu alafu mkatoliki ndo wamempa mpini,,mkatoliki kabisaa,akubakize
Historia yetu imepotoshwa mno.May Day,
Kitabu leo kipo miaka 20 kimechapwa mara nne na hajatokea mtu yeyote kusema kuwa mimi ni muongo.
Kilichofanyika ni kuundwa jopo linaloongozwa na Prof. Issa Shivji akiwa na Prof. Saida Yahya na Dr. Kamatha ambao sasa wanaandika historia ya Mwalimu Nyerere ili angalau wapate kufahamu nafasi yake katika kuasisi harakati za kujikomboa kutoka ukoloni.
Jopo hili wamefanya mazungumzo na mimi nyumbani kwangu mara mbili na nimewapa picha na nakala za nyaraka kutoka Nyaraka za Sykes ambazo baadhi wamepata kuzionyesha katika Kavazi la Mwalimu Nyerere ambalo Prof. Shivji ni Mwenyekiti wake.
Marehemu Prof. Haroub Othman kaonana uso kwa macho na Mwalimu Nyerere kuhusu kitabu cha Ali Muhsin Barwani, ''Conflict and Harmony in Zanzibar,' Dubai (1997) na ''The Life and Times of Abdulwahis Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' London (1998), vitabu viwili ambavyo Mwalimu katajika sana.
Kama ilivyokuwa kwako wewe Prof. Haroub alichomwa sana na historia hii niliyoandika akili yake ilikuwa inakataa kama yale anayosoma ni kweli.
Mimi nilizungumza na Prof. Haroub ambae ni mwalimu wangu na yeye ndiye aliyeniambia kuwa ameonana na Mwalimu na akamuomba na yeye aandike ili yapatikane majibu kwangu na kwa Sheikh Ali Muhsin.
Napenda kukufahamisha kuwa baada ya kuzungumza na mimi hakutosheka Prof. Haroub alikwenda kufanya mazungumzo na Ahmed Rashad Ali mtu aliyekuwa rafiki kipenzi na Abdul Sykes kutaka ukweli wa yale yeye alikuwa na mashaka.
Prof. Haroub aliondoka katika mazungumzo yake na Mzee Rashad akiwa kichwa kainamisha.
Mimi sina sababu ya kuzua uongo.
View attachment 1221898May Day,
Kulia: Prof. Haroub Othman, Ahmed Rashad Ali na Ahmed Islam 1997
View attachment 1221902
Kulia: Prof. Issa Shivji, Prof. Saida Othman na Dr. Kamatha siku walipokuja kufanya mazungumzo na Mwandishi kuhusu kitabu cha Abdul Sykes 2013
Unaweza kutaka kumjua Ahmed Rashad Ali ni nani katika historia ya Tanzania.
Tafadhali ingia hapo chini:
![]()
AHMED RASHAD ALI BINGWA WA PROPAGANDA ZA UKOMBOZI WA AFRIKA SEHEMU YA KWANZA
1931 Cup Central Government School Mnazimmoja Waliosimama kuanzia kulia: 1. Amour Muhammed Al Barwani 2. Muhammed Abdulla Al Gh...mohamedsaidsalum.blogspot.com
![]()
KUTOKA JF: HISTORIA YA TANZANIA ITAKAVYO WAHUKUMU AHMED RASHAD ALI, ALI MUHSIN BARWANI, ABDUL SYKES NA JULIUS NYERERE
dangadunguri said: ↑ Na yeytu anayekuja mbio bila kupepesa na kuanza kutoa kejeli na matusi ujue UJUMBE AMEUPATA sasa ni aibu ujumb...mohamedsaidsalum.blogspot.com
Kwa hiyo kura tatu ya tabora ndo iliwaweka kando waasisi wa tanu akina muft Ameir na wenziwe.B...
TANU ilikuwa nationalist-secularist party ila ilikuwa imetawaliwa na wanachama na viongozi Waislam hadi kufikia Kura Tatu mwaka wa 1958.
Wazee wetu wakiongozwa na Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa mufti wa Tanganyika walijitahidi sana kuijenga TANU katika msingi wa kuwaunganisha wananchi wote wa Tanganyika kudai uhuru kwa umoja wao.
B...Kwa hiyo kura tatu ya tabora ndo iliwaweka kando waasisi wa tanu akina muft Ameir na wenziwe.
Lkn pia la ziada baada ya mwalimu kupata uhuru wa tanganyika na kua rais ulitaka mwalimu awape nini wale waanzilishi na waasisi wa tanu,,?
Impongo,Historia yetu imepotoshwa mno.
Baba yangu mkubwa ambaye alikua, na kulelewa na kanisa tangu akiwa mdogo tangu mwaka 1941.
Miaka ya 1995 alipendamulia historia ya Tanganyika na kutueleza kuwa ina uongo kwa 86% na ukweli baada ya kujifunza na kupitia sehemu mbalimbali kuna uongo mwingi.
Leo hii. Mohamed Said. Umenisaidia kufanya hitimisho kuupata ukweli dhahiri.
Tegemea utapata upinzani kwa wale wavivu wa fikra lakini jitahidi kutupa ukweli tujifunze zaidi huenda siku moja taifa hili kitaandika historia ya kweli na kuacha urithi wa historia isiyotia shaka.
Mungu akubariki.