Barua ya mwaliko ili kupata passport

Barua ya mwaliko ili kupata passport

Na passport huwa inaukomo wa muda(Expiration)? Au inakuwaje? Na je, kama inaukomo, kurenew ni lazima?

Niliwahi kwenda nje ila nilitumia emergency documents.

Sasa wakati narudi Tz pale boda nikaona jamaa mmoja wamemhold kwamba passport yake ishaexpire kitambo anahitajika kulipa terms 5.

Sasa sikuelewa hiyo imekaaje.
 
Tatizo lako uliwaambia unaenda yuropu au amerika
Ungewaambia unaenda Malawi hapo kwenda kuloga walaaa wasingekuomba mwaliko au sababu ya safari.
Sasa katafute mwaliko.
Mkiambiwa muwe mnapitia kwa vishoka muwe waelewa kwani utaepuka kadhia kubwa kubwa kama hizi
Inasikitisha sana
 
Passport ni hati ya kusafiria...

Kama huna sababu ya safari tarajia kukutana na mkwamo kwenye kuipata...

Sababu ni kupunguza gharama za uchapaji, kuzuia passport kutumiwa na maharamia n.k...
Passport inanunuliwa, sio bure.
Vipi kama sababu za kusafiri ni kwenda kutembea tu au kufanya utalii nchi nyingine??
 
Logically ni kitu ki moja. Mfano unapojibu nimealikwa na mtu then toa mwaliko, kama utajibu unaenda masomoni utaombwa admission letter. Ilinitokea nlikuwa naenda exchange then waliomba ile barua ya kunialika kwenda kubadilishana uzoefu
Kama naenda kutembea tu au kufanya utalii??
 
Invitation letter anaandika mwenyeji wako huko unakoenda. Just kuthibitisha kuwa yeye ndiye anakupokea, usije zamia nchi za watu kama mhamiaji haramu😀😀
Kama naenda kufanya utalii au kula bata tu??
 
Katika vitu navyoumia ni pamoja na hiki Watanzania kushindwa kupewa passport zao kwa wakati na bila kutoa rushwa unakuta bwana mdogo ana safari ya muhimu sana ila muhuni anamkazia kwa maswali ya kijinga jinga tu ili mradi amkwamishe ili atoe rushwa..
 
Rudi tena waambie unakwenda nchi ambazo hazihitaji mwaliko wala visa. Zipo nyingi tu.
Akiwaambia anaenda Mecca kufanya hija na kumpiga shetani mawe bado watataka mwaliko??
 
Passport si haki ya kila mtanzania??
Kwann kuna vikwazo??
Ukurasa wa 48 wa Pasipoti, kuna "Tahadhari" inayosema "Pasipoti hii ni mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na inaweza kuchukuliwa na Serikali wakati wo wote. Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri, Serikali inawaomba na kuwasihi wote watakaohusika kukuruhusu wewe unayekuwa nayo kupita bila kizuizi cho chote na kukupa msaada wo wote utakaohitajika". Pasipoti za mataifa yote ulimwenguni zinasema hivyo hivyo. Kama unataka kusafiri kivyako tu, nenda bila pasipoti ya nchi ukajijue kivyako kukitokea matatizo.
 
Passport inanunuliwa, sio bure.
Vipi kama sababu za kusafiri ni kwenda kutembea tu au kufanya utalii nchi nyingine??1

Mkuu kama ushawahi safiri kwenda nje utakubaliana nami kwamba lazima uoneshe uthibitisho wa sababu ya kusafiri iwe ukiomba passport au visa...Sasa sijajua maswali yako yanalenga kutaka kujua kitu gani?
 
Vipi kama mtu anataka kwenda kufanya utalii tu nchi nyingine??
Ukiwa na evidence kwamba mpunga unao af mkono wako usiwe mfupi Sana unatoboa fasta. 3 days ya nne kitabu unapokea
 
Siku ya jana nimepeleka document zangu kwa ajili ya kupata passport lakini nimeambiwa inahitajika barua ya mualiko pamoja na copy ya passport ya mtu ninae kwenda kumtembelea.

Kama kuna mtu yuko na sample ya barua ya mualiko anisaidie nipate niweze kuedit kwa ajili ya kuitumia.
Ili upate passport uwe na :-
Barua ya utambulisho toka serikali za mtaa.
Ceti chako cha kuzaliwa (copy)
Cheti cha kuzaliwa mzazi mmoja/affidavit
Barua ya maombi ya passport kwenda kwa kamishna uhamiaji.
Kitambulisho cha NIDA/NAMBA
picha moja ya passport
Hakuna wqlipoandika barua ya mwaliko. Wanataka rushwa tu hao
 
Siku ya jana nimepeleka document zangu kwa ajili ya kupata passport lakini nimeambiwa inahitajika barua ya mualiko pamoja na copy ya passport ya mtu ninae kwenda kumtembelea.

Kama kuna mtu yuko na sample ya barua ya mualiko anisaidie nipate niweze kuedit kwa ajili ya kuitumia.
Kama unakwenda kumtembelea mtu, huyo mtu aandike barua inayosema "Fulani ni ndugu/rafiki yangu anakuja huku kwa madhumuni ya kunitembelea. Anatarajia kufika hapa nchini (itaje nchi inayohusika) tarehe (itaje) na atakuwa hapa kwa muda fulani (utaje). Anwani yangu ya makazi ni (taja) na kimawasiliano ninapatikana kwenye simu namba ..., barua pepe..., nk. Mhusika atakaa kwangu wakati wa ziara yake na mimi nitahusika kwa gharama zote za ugeni huo, zikiwemo malazi, chakula, nk. (au taja vinginevyo kadiri ya makubaliano yenu)".
Mimi ninaishi nje ya Tanzania. Nimewahi kuandika barua ya aina hiyo kwa ndugu Watanzania watatu, rafiki Watanzania wawili, na familia rafiki moja ya Kiganda. (Hapo ujuwe kwamba si Tanzania tu wanaotaja hitaji hilo). Hakukuwa na tatizo lo lote katika mifano yote niliyoitaja. Wahusika waliweza kuja bila bughudha yo yote.
 
Back
Top Bottom