Barua ya mwaliko ili kupata passport

Barua ya mwaliko ili kupata passport

Ni check mimi pm tuyajenge. Wewe utakaa home tu mpaka siku ya kuja kuweka finger print. Muhimu sana NIDA au Namba yako ya NIDA. Hizo docs nyingine zinapatikana steshenary na pale pale uhamiaji
Nimefika pm mkuu
 
Wape ya pili
 

Attachments

  • Screenshot_20241127_074522_Chrome.jpg
    Screenshot_20241127_074522_Chrome.jpg
    325.2 KB · Views: 12
Mtoto wa mtazania aliyezaliwa kwenye nchi inayotoa uraia wa kuzaliwa mara mmoja (bila kujali asili ya wazazi, mfano Marekani), mtoto anakuwa na uraia pacha, mpaka atakapofikisha miaka 18. Baada ya hapo, atachagua uraia mmoja.
Wewe Sasa ndio umenipa elimu jinsi inavyopaswa Asante mkuu..

Hilo jamaa la kuitwa Bufa hakuna Cha maana lilichofanya hapa zaidi ya kuleta ujuaji na kebehi za kipuuzi tu.
 
Ila kama unaenda South Sudan, fast unapewa uende ukafe huko
Sawa tu kama wananipa passport kubwa... Heri kufua nchi kama sudani kuliko kufia hapa tunapodanganyana eti Kuna Maziwa na asali
 
Siku ya jana nimepeleka document zangu kwa ajili ya kupata passport lakini nimeambiwa inahitajika barua ya mualiko pamoja na copy ya passport ya mtu ninae kwenda kumtembelea.

Kama kuna mtu yuko na sample ya barua ya mualiko anisaidie nipate niweze kuedit kwa ajili ya kuitumia.
Passaport ni haki ya kila mtanzania rudi tena huko huko bila ya hiyo barua!
 
Nakumbuka niliambiwa nilete bank statement nikafoka sana habari ya statement ikajifia. Two weeks later passport tayari
 
Sawa na kitambulisho cha NIDA
wageni wanapata kiurahisi ila watz sasa
Kuna jamaa mmoja msomali hata sio mzaliwa wa hapa, amezaliwa Mombasa huko Kenya na mpaka kuishi anaishi huko huko Mombasa, ila ana kitambulisho Cha NIDA na kinaonesha amezaliwa ILALA🥺🤨...

Mara nyingi nchi yoyote ambayo imetafunwa sana na Rushwa, huduma mbovu huwa zinakuwaga kwa wazawa tu Tena wa Hali ya chini... Mara nyingi wahanga wa bureaucracies na maudhi yote ni wazawa.

Kuna Uzi uliwahi kuletewa humu ulikuwa unamuhusu jamaa mmoja mGhana alikamatwa na madawa ya kulevya huko Malaysia akiwa na Passport inayomuonesha yeye ni raia wa Tanzania... Miaka ya 2017.
 
Ujinga umeandika.

Kusafiri ni hitaji la misingi kwa binadamu.

Huo unaoita ujinga ni sababu ambazo serikali yako huwa inataja, ni nukuu (inaonesha huna information)...

Sasa kama una sababu ya kusafiri peleka maombi watakupa passport...
 
Siku ya jana nimepeleka document zangu kwa ajili ya kupata passport lakini nimeambiwa inahitajika barua ya mualiko pamoja na copy ya passport ya mtu ninae kwenda kumtembelea.

Kama kuna mtu yuko na sample ya barua ya mualiko anisaidie nipate niweze kuedit kwa ajili ya kuitumia.
wewe mwandikie anayekualika akutumie barua,hiyo kopi ya passport ya mtu aliyekualika haina haja ni usumbufuntu wa hao watu wa uhamiaji
 
Ni check mimi pm tuyajenge. Wewe utakaa home tu mpaka siku ya kuja kuweka finger print. Muhimu sana NIDA au Namba yako ya NIDA. Hizo docs nyingine zinapatikana steshenary na pale pale uhamiaji
Na wewe acha kuharibu kazi za watu
 
Sababu zipo nyingi mkuu, lakini hiyo ni mojawapo kuondoa hofu ya uhamiaji haramu. Kuna sababu nyingine kama kuthibitisha safari yako kama ni ishu ya kutembelea familia, charity nk, lakini pia kuthibitisha muda wa kukaa, kuonyesha uhusiano wako na mwenyeji wako kama ni shirika, mtu binafsi nk, kwa kifupi hayo ndio baadhi ninayayafahamu mimi.
Mimi kuwa na barua ya mwaliko wa safari haiwezi kunizuia kuwa muhamiaji haramu huko niendako kama lengo langu ndio Hilo, kwani baada ya Mimi kuondoka hapa nchini watakuwa Wana ni monitor huko nilipo au?

Kimsingi tu hizo sababu ulizoziweka hapo hazina uzito wa kimantiki hata kidogo... Mbona mataifa mengine hapa Afrika hayana huu ujinga?

Hivi unajua kwamba unavyotoa easy Access ya watu kuondoka inchini hata serikali Inakuwa imepunguza mzigo kwa namna Fulani hivi?? Kuna inchi kama Nigeria Moja ya njia ya kupunguza mzigo mzito walionao kutokana na population yao serikali inawapa urahisi wa kuondoka inchini raia wake wakatufute fursa sehemu nyingine... Na ndio maana wanaijeria wametapakaa duniani kote Wana msemo wao wanasema "if you visit any part of this world and you don't find Nigerian, oga the place you visited is not meant for human being.

Leo hii ukienda nchi kama USA hili ukutane na mtanzania basi lazima kwanza uwe umeshakutana na wanaijeria kama 200 na wakenya kama 50 kisha ndio unakuta na mbongo Sasa... Yaani watanzania hawapo kabisa huko duniani na sababu Moja wapo ni Mambo kama haya ya ugumu wa kupata kwanzia passport.

Mwaka Jana Kuna report niliiona ikielezea idadi ya wanafunzi wanaotoka afrika waliko kwenye vyuo vikuu vya Canada.

Wanaijeria walikuwa 20,000, Waghana 11,000 wakenya wako 8,000 halafu wanafunzi wa kitanzania wako sijui 1,200.

Unaweza ukaona jinsi gani sisi Bado tumejifungia humu ndani tukidanganyana eti nchi yetu ni ya Maziwa na asali huku fursa mbali mbali za kielimu na kiuchumi zikitupita sababu ya kuendekeza mambo ya kijima.

Ndio maana Kuna muda huwa naamini taifa hili limelaaniwa na Mungu maana Kuna mambo mengi sana ya ovyo
 
wewe mwandikie anayekualika akutumie barua,hiyo kopi ya passport ya mtu aliyekualika haina haja ni usumbufuntu wa hao watu wa uhamiaji
Kwa hiyo asipomuandikia hiyo barua basi ndio imekula kwake hapati hiyo passport???
 
Naona hapa kuna wataalam wa mambo.

Naomba kujua tofauti ya Passport ya kusafiria na VISA.

Na ipi ni bora zaidi? 🙏🏾

Na utaratibu/mahitaji ili kifanikiwa kuwa na hivyo.
 
Kwa ufahamu mfupi nilionao Visa ni kama entry permission ya kuingia nchi Fulani wakati Passport ni kama utambulisho tu kuonesha unatoka wapi...

Kuhusu kipi Cha muhimu kati ya hivyo viwili, Cha muhimu zaidi hapo ni passport
 
Kwa ufahamu mfupi nilionao Visa ni kama entry permission ya kuingia nchi Fulani wakati Passport ni kama utambulisho tu kuonesha unatoka wapi...

Kuhusu kipi Cha muhimu kati ya hivyo viwili, Cha muhimu zaidi hapo ni passport
De Opera
 
Back
Top Bottom