Basi Nenda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 20,774
- 47,866
Kinshasa, May 11 1997
Kwa Mheshimiwa Rais,
Bwana Jacques Chirac
Rais wa Jamhuri ya Ufaransa
Mheshimiwa Rais,
Kwanza kabisa ningependa kutanguliza salamu zangu za dhati kwako na kwa mkeo, vile vile kwa jina la urafiki mrefu sana ambao umetuunganisha kwa zaidi ya miaka kumi.
Leo hali ni ya machungu sana kwangu mbele ya mvuto wa muda mfupi kwanza kwenye kiwango cha madaraka yangu ambapo nimepoteza ufanisi katika watu, pili katika kiwango cha kijeshi ambapo ni vigumu mimi kuzuia maendeleo ya wanamgambo kuja Kinshasa ambapo wanaweza kufika muda wowote.
Na kuhusu Kinshasa siwezi kukuza umwagaji wa damu usiohitajika kwa namna yoyote ile wanamgambo wataifikia Kinshasa ni suala la muda tu. Je, nina budi kukukumbusha ninapambana na vita visivyokuwa na usawa? Leo Marekani na Uingereza kupitia Afrika Kusini, Uganda, Rwanda na Angola wanamtumia kiongozi wa genge la waharifu Laurent Kabila kunichoma kisu mgongoni huku wakitumia mwanya wa maradhi yangu.
Zamani Marekani walikuwa ni washirika wangu; kumbuka visa vya Angola ninabakiza haki ya kuchapisha kumbukumbu zangu katika siku chache zijazo ili dunia nzima ipate kujua ukweli uliofichika
Rafiki yangu unafahamu kama mimi ninavofahamu kwamba Laurent Kabila ni mtu wa kutilia shaka, muuaji na mwenye tabia zisizofaa kuiongoza Zaire, kama kiongozi wa nchi nimejaribu kwa kila namna kuzuia hili lakini mabwana zake wa Magharibi, Wamarekani, wanamuunga mkono.
Kutokana na ukaidi wa Marekani na kuzidi kuzorota kwa Afya yangu ninalazimika kutangaza lengo langu la kumpa madaraka Kabila katika kikao chetu kijacho katika meli ya Utenika mnamo May 14.
MOBUTU SESE SEKO KUKUNGBENDU WA ZABANGA
MARECHAL
RAIS WA JAMHURI
Sent using Jamii Forums mobile app