Barua ya wazi kwa dada Halima Mdee

Wabunge watae Wabunge wataenda, na wewe utaendelea kuwashabikia tu huna namna, huna maamuzi kwenye chama na ukichoka hama uende kwa dovutwa.
Pesa mnapewa za bando mnadhani zinatoka wapi kama sio ruzuku ya hao wabunge.?
 

Sio kwa Tanzania hii ambayo mnasusa kila siku
 
Nasikia kuna wapenda amani wamechoma nyumba ya mtu mmoja kwa kusisitiza suala la amani ya kusafisha wavurugaji wasiopenda amani ya nchi kule Katikati ya Afrika na kuweka matumbo yao Mbele.
Yana mtu ana sheria inayomwongoza namna ya kuendesha zoezi zima la Uchaguzi wa Timu bora duniani halafu anakiuka na kuchagua timu anayoona inampa pesa na maisha mazuri tu huku akipuuza mawazo na kura za wanasoka.

Sijawahi kusikia kama kweli Wapenda amani wamekwenda mahakamani kudai kuwa wamenyima amani . Nasikia tu wapenda haki wakipinga amani na wapenda amani wakipinda tu haki huku wanufaika wa amani wakitumia vitisho ,kuua, kutesa na nguvu kama ngao ya amani ya nafsi zao na amani ya Mali zao.

Khaaaa ,kumbe matajiri siku zote adui yao ni Haki. Na maskini adui yao ni dhulma.
Tangu lini maskini akaweza kumdhulumu Tajiri.?
Tangu lini maskini akakosa amani kwa sababu ya ugumu wa maisha wakati kwake ugumu wa maisha ndiyo maisha yake . Woga wa maskini ni kukosa haki yake mbele ya sheria.
Hayo.

Hofu ya wapenda amani kote duniani ni kukosa nafasi ya kutumia Mali zile walizodhulumu. Kumbe basi amani kwao ni kutoa haki.
Light wangejua kuwa siku zitafika ambapo kuishi kwa Mwovu kutakua ni gharama kubwa sana mana itabidi ajenge nyumba yenye Fensi kubwa sana ,makamera kila kona, mbwa wengi,walinzi nyumbani na ofisini na barabarani, na kila aina ya tahadhari . Je, si bora zaidi kwa mtu kuwa na Mali za kadiri na halali bila kuzipata kwa kudhulumu wengine na kutoa machozi ya haki kwa wengine?
Hivi walioua watu kule kwenye mashamba ya Visiwa vya Karafuu nchini Komoro wanajisikiaje wakiona vilio vya watoto wa marehemu na wajane kwa sababu tu kuna watu wanataka kunufaika na amani ya dhulma ya miayo yao wenyewe?

Je, Afrika neno Haki limekua limepigwa marufuku kutajwa na viongozi wa serikali au ni kwa sababu Haki itawanyima Waovu wengi utajiri wa dhulma na hivyo watapoteza amani yao?

Mtu yupo Bungeni miaka 30 lakini anatumia jeshi ,polisi ,usalama wa chama kutesa ,kuua na kunajisi watu ili arudi bungeni mwaka wa 35 ? Khaaa. Hata shetani ana nafuu mana hamlazimishi mtu amkubali bali anatumia maneno matamu na vishawishi.
 
Mwenyewe namushauri halima apelrke majina na yeye mwenyewe aende bungeni wanaume ni wabinafsi Sana, ni bawacha tu imebaki na nguvu na udhubutu wanaume waoga wamebaki suruali tu
 
Sasa kwenye mtihani wakifeli wengi na wewe ukifaulu hautaendelea kisa wengine wamefeli?
Hii hoja yenu ya kitoto na kiubinafsi na penda kuwaona wakienda bungeni ni wachache Ila SAUTi yao itasikika
 
Nilifikiri barua ya uchumba
 
Hivi kweli unaona ni sawa kuwanyima wabunge wa upinzani ushindi wao kule majimboni kwa hila za kila namna ikiwemo Fursa ya kutangaza Sera zao kupitia TV na Radio halafu serikali hiyo hiyo iliyotumia nguvu kuwazuia wananchi kuchagua wapinzani kwa sanduku la kura sasa inasema iko tayari kutoa nafasi 19 za bure kwa chama cha upinzani kwa sababu ni matakwa ya sheria !?
Je, sheria haikuwa inafanya kazi wakati wa zoezi zima la kura lakini sasa ndio imekua rafiki?

Je, huoni kuwa bado kuna hila kubwa inayoandaliwa ili hao wabunge wa viti maalumu wakifika Bungeni wadhalilishwe I wakijibu hoja kwa jaziba iwe sababu ya kuwapiga na kuwatoa nje kwa nguvu na kusema kuwa wapinzani wanafanya vurugu bungeni hivyo maeneo wanayotoka watanyimwa maendeleo kwa sababu ya kupinga maendeleo?

Huoni kuna watu kama Kibajaji , Juliana, Gwajima ,Musukuma wameandaliwa kwa ajili ya kutumia kugha chafu za kuwadhalilisha Wakina Mdee na Bulaya na wengineo watakaopewa nafasi maalumu za Ubunge kuwa Wamehongwa hizo nafasi kingono ?

Je, Ni spika yupi au Naibu spika yupi au nje ya Bunge ,serikali ipi au mahakama ipi itawasikiliza na kupinga udhalilishaji na matusi watakayotukana miaka mitano huku Jamii ikiaminishwa kupitia TBCCM na Chanel Ten CCM kuwa Chadema imepeleka Wabunge wa viti maalumu kwa upendeleo na Rushwa ya ngono?

Kama Binti Mzuri kama Upendo Peneza amenyimwa ushindi wake akapewa Mwanaume asiye na mvuto kwa sababu tu ya kuvuruga Demokrasia kuna haja gani ya kwenda kumtukana na kumdhalilisha bungeni.
Kwanza bado ni binti mdogo atafika Mbali sana wakati huo akina Ndugai watakua hawapo tena huku juu ya ardhi.


Chadema isikubali kudumisha udikiteta kwani Demokrasia halali ilikua ni sanduku la Kura na CCM na serikali yake ikavuruga uchaguzi mzima kwa maana ya kutaka wapite wenyewe na kwenda kujenga maisha yao kama wakivyopania kuwa mabilionea kupitia Ubunge na Uwaziri.
 
Mkuu acha kumpotosha Dada Halima, ubunge ndo kazi yake, mwache akafanye kazi yake ya ubunge. Wewe kama ulishashindwa usimshauri mwenzako kufanya maamuzi mabovu ili mshindwe wote.
Acha ujinga, Mdee sio wa kusubiri fadhila. Kwa vipindi vyote Kawe kawagaragaza magwiji wa siasa hivyo acha kumfanya legelege kama unavyodhani
 
Sasa kwenye mtihani wakifeli wengi na wewe ukifaulu hautaendelea kisa wengine wamefeli?
Hii hoja yenu ya kitoto na kiubinafsi na penda kuwaona wakienda bungeni ni wachache Ila SAUTi yao itasikika
Tumia akili kabla ya kuandika. Mdee ameshinda Kawe, kwa nini kumnyang'anya ushindi ili kumpa viti vya hisani?
 
Mlisema hafai kurudi bungeni......
 

Ndio ndio ndio mkuu agiza beer [emoji481] kwa mangi nakuja kulipa
 
Pumbavu. Uzi wa kijinga kabisa, pengine umeandikwa Lumumba. Vicha upumbavu wako. CHADEMA ikafanye nini kwenye bunge ambalo ni NEC B ya CCM? CHADEMA, yenye akili mno, haiwezi kuhalalisha uchaguzi haramu kwa kupokea viti maalumu.
 
As long as Aida Khenani yupo bungeni na chama kipo kimya ni suala la muda ila majina yatapelekwa na akina mama hao wataingia bungeni hata kabla ya hiyo deadline ya April 2021

Tuwe tu na akiba ya maneno.
 
Pumbavu. Uzi wa kijinga kabisa, pengine umeandikwa Lumumba. Vicha upumbavu wako. CHADEMA ikafanye nini kwenye bunge ambalo ni NEC B ya CCM? CHADEMA, yenye akili mno, haiwezi kuhalalisha uchaguzi haramu kwa kupokea viti maalumu.

Ww ndio mpumbavu
Hivyo viti maalum vingekuwa wanaume wanaenda basi chadema wangeenda wasingejali utopolo wako

Unajua gharama za kuongoza chama ww?

Au unaongea tu kwa vile una MB
 
As long as Aida Khenani yupo bungeni na chama kipo kimya ni suala la muda ila majina yatapelekwa na akina mama hao wataingia bungeni hata kabla ya hiyo deadline ya April 2021

Tuwe tu na akiba ya maneno.

Yes kabisa
Na mchango wake chama imechukua
 
Majina yako tayari
Ila sasa changamoto iko kwa wabunge waliokosa majimbo ndio hawataki na wanashawishi majina yasipelekwe
Thibitisha! Au wewe ndiye halima Mdee? Una uhakika gani kuwa majina yapo tayari?
Jambo moja mnalisahau ya kuwa bawacha siyo cdm Bali ni idara ndani ya cdm ambayo haiwezi kuwa na maamuzi yake bila kuyawakisha kwenye chama!
Kwasasa sahauni habari ya viti maalum kwani bawacha nao no binadamu, Wana uchungu wa wapigakura wenzao waliopoteza Maisha na au kupata ulemavu kwa sababu ya ccm kupora ushindi!
 
Nimekumbuka lile andiko la kusema:

“Akupigae shavu moja mgeuzie na lingine”

“Akunyang’anyaye joho mpe na kanzu pia”

Inahitaji tafakari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…