Barua ya wazi kwa members wenye chuki zisizo na msingi kuhusuya Id yangu!

Barua ya wazi kwa members wenye chuki zisizo na msingi kuhusuya Id yangu!

Nimetoka kuhakiki nssf yangu mwezi March, aside na wasiwasi wazee tupo!
Hapo wajukuu washindwe wao tu, uzuri wa sisi Wazee hatuna shoo za kukamia kama walivyo vijana 🤪
 
Kumbe mko sokoni🤔🤔🤔
Ile umaarufu, sijui watu kukutaka kukujua au sokoni sijui vinatokana na nini! Nimegundua hata yale masihara tu watu wanayahesabu wanahisi mtu yuko serious incase uki click na baadhi ya watu mka-vibe inaumiza wengine. Tujifunze kutofautisha! Hakuna comment yangu inayoonesha kutafuta soko wala umaarufu! Ni shobo zao waja wenyewe sikuita mtu na siko katika hiyo age ya upumbavu! So watatafuta namna ya kuheal.. mimi niko ambaye niko😎
 
Hello members,

Kwanza kabisa, mimi sio mwanaume! kuna watu wananifahamu na ninaongea nao mambo mbalimbali ya kiimani na kibiashara! mimi sio malaya wala shoga! kukaa kwangu jf muda mwingi au kila siku sidhani kama inamuhusu mtu yoyote humu! mnaotaka kuni-babysit please sihitaji! yamekuja maparody na ids kibao kunijazia kunguni kila mahala, sitaki na ninaomba mniaiche! mara mtu akusalimie leo, kesho kajinunisha upumbavu, please!

Na kama kuna member yoyote ambaye nimewahi kuchat naye mambo ya pesa sijui umalaya ajitokeze na ushahidi! sijawahi kuomba pesa humu na wala sina hizo tabu ndogo ndogo kama mnavyonikadiria. Naona tuhuma zimekuwa nyingi si wame wala wake! mnanivamia sana kwenye comments na kukicha mnaongezeka! Hizo chuki zidi yangu zinawasaidia nini?

Inashangaza kuona jinsi baadhi ya watu wanavyotumia muda wao mwingi kutengeneza simulizi, tuhuma na hitimisho kuhusu kitu ambacho hawakifahamu kikamilifu. Wengine wamejigeuza wachunguzi, waendesha mashtaka na majaji kwa wakati mmoja, ilhali hawana ushahidi wala uelewa wa jambo lenyewe.

Kwa wale vijana mnaojitafuta na kunianzishia nyuzi zisizo na kichwa mimi huwa nahesabu kama utani na wengi wenu ni wadogo kwangu! nikisema niwe serious sana hapo tutazinguana sana halafu mimi ndio nitabaki kuonekana mjinga! Nyuzi nyingi haziko serious ila kuna hawa viumbe wenye nyota za mbwa wanaumia sana, mimi sijamtuma mtu kunianzishai nyuzi! kama kuna yoyote nachati naye nje ya uzi wake aje kunianika hapa!

Kuwa na maoni ni haki ya kila mtu, lakini kujenga chuki juu ya dhana, uvumi na hisia binafsi ni upungufu wa fikra, si hoja. Kama mngewekeza nguvu mnazotumia kunichunguza katika maisha yenu binafsi, huenda mngekuwa mbali zaidi kuliko mlipo sasa. Kama humjui mtu kwanini ujifanye unamjua? unapata faida gani kumchafua mtu? ukikaa kimya kuna biashara yako labda inaharibika?

Sina deni la kuwafurahisha wanaonichukia, wala sitabadilisha ukweli ili uendane na simulizi mnazozipenda. Ukweli hubaki kuwa ukweli hata kama hauwapendezi.

Kwa hiyo kabla ya kuhukumu, hakikisheni mnajua mnachokizungumzia. Vinginevyo, mnachobaki nacho si ukweli bali ni kelele za chuki zisizo na msingi.

Naruhusu maoni, chonde chonde leo sukari yangu iko juu!
Unajipa umuhimu sana kwenye jukwaa.
Una matatizo ya akili 🚮
 
Acha tu kipande dawa zipo kitashushwa! Hata changu kilishashuka😅
Nimeshauriwa nitembee na dawa zangu za kisukari, maana sio kunikaripia huku babu yako 😢

Kuna haja uniletee kiko pengine hiki kisukari ulichonipandisha kikashuka
 
Nimeshauriwa nitembee na dawa zangu za kisukari, maana sio kunikaripia huku babu yako 😢

Kuna haja uniletee kiko pengine hiki kisukari ulichonipandisha kikashuka
Unatakiwa uwe na mixed feelings babu, wengine wanakubembeleza wengine tunakuchemsha sukari ipande😆
 
Unatakiwa uwe na mixed feelings babu, wengine wanakubembeleza wengine tunakuchemsha sukari ipande😆
Kwahiyo ndiyo uanze kunifundisha hizo mixed feelings uzeeni lakini

Bora uniletee tu kiko pengine nitapata nafuu babu yenu 😉
 
Back
Top Bottom