Barua ya wazi kwa members wenye chuki zisizo na msingi kuhusuya Id yangu!

Barua ya wazi kwa members wenye chuki zisizo na msingi kuhusuya Id yangu!

Hello members,

Kwanza kabisa, mimi sio mwanaume! kuna watu wananifahamu na ninaongea nao mambo mbalimbali ya kiimani na kibiashara! mimi sio malaya wala shoga! kukaa kwangu jf muda mwingi au kila siku sidhani kama inamuhusu mtu yoyote humu! mnaotaka kuni-babysit please sihitaji! yamekuja maparody na ids kibao kunijazia kunguni kila mahala, sitaki na ninaomba mniaiche! mara mtu akusalimie leo, kesho kajinunisha upumbavu, please!

Na kama kuna member yoyote ambaye nimewahi kuchat naye mambo ya pesa sijui umalaya ajitokeze na ushahidi! sijawahi kuomba pesa humu na wala sina hizo tabu ndogo ndogo kama mnavyonikadiria. Naona tuhuma zimekuwa nyingi si wame wala wake! mnanivamia sana kwenye comments na kukicha mnaongezeka! Hizo chuki zidi yangu zinawasaidia nini?

Inashangaza kuona jinsi baadhi ya watu wanavyotumia muda wao mwingi kutengeneza simulizi, tuhuma na hitimisho kuhusu kitu ambacho hawakifahamu kikamilifu. Wengine wamejigeuza wachunguzi, waendesha mashtaka na majaji kwa wakati mmoja, ilhali hawana ushahidi wala uelewa wa jambo lenyewe.

Kwa wale vijana mnaojitafuta na kunianzishia nyuzi zisizo na kichwa mimi huwa nahesabu kama utani na wengi wenu ni wadogo kwangu! nikisema niwe serious sana hapo tutazinguana sana halafu mimi ndio nitabaki kuonekana mjinga! Nyuzi nyingi haziko serious ila kuna hawa viumbe wenye nyota za mbwa wanaumia sana, mimi sijamtuma mtu kunianzishai nyuzi! kama kuna yoyote nachati naye nje ya uzi wake aje kunianika hapa!

Kuwa na maoni ni haki ya kila mtu, lakini kujenga chuki juu ya dhana, uvumi na hisia binafsi ni upungufu wa fikra, si hoja. Kama mngewekeza nguvu mnazotumia kunichunguza katika maisha yenu binafsi, huenda mngekuwa mbali zaidi kuliko mlipo sasa. Kama humjui mtu kwanini ujifanye unamjua? unapata faida gani kumchafua mtu? ukikaa kimya kuna biashara yako labda inaharibika?

Sina deni la kuwafurahisha wanaonichukia, wala sitabadilisha ukweli ili uendane na simulizi mnazozipenda. Ukweli hubaki kuwa ukweli hata kama hauwapendezi.

Kwa hiyo kabla ya kuhukumu, hakikisheni mnajua mnachokizungumzia. Vinginevyo, mnachobaki nacho si ukweli bali ni kelele za chuki zisizo na msingi.

Naruhusu maoni, chonde chonde leo sukari yangu iko juu!
Nyuzi zako zinafanana na nyuzi za GENTOMICE sijui sikuhi yupo wapi
 
Seran cha kukushauli kutokua serious na ID za humu au watu humu sisi tunatunwa matusi makubwa lakini sijawai kuyachukulia serious wala kuona kama yananihusu ndo life
Hii yangu sio huko, sipo huko kabisa! kuna campain imeanzishwa inasambaza taarifa za uongo muda mrefu humu! so mpaka nimeongea sijakurupuka! na sababu za kipuuzi sana eti naanzishiwa nyuzi! sio kubishana as mabishano basi tu out of air mtu anakuja na chuki!
 
Nadhani humu JF mm ndo hua siko serious ndo mana cjawah kuumizwa kichwa na chcht cha humu JF

Nawashangaa sana watu wanaoichukulia JF kama vile ndio muongozo wa maisha yao kiasi kwamba hadi wanashikiwa akili na watu wa humu na kila kitu kilichomo Humu.

Imagine niliwahi kumpoteza mwanamke niliyewah kukutana nae humu JF kisa ameshikiwa Akili na mambo ya JF akizani upuuzi wa humu kila mtu anao.
 
HU
Tena wangari mathari kabla yake alikua anajiita manengelo, pia kuna yule dada alie letwa kutoka mwanza kuja dar aklipwa mi sita sijui alikuja julikana.
Wapo wengi waliamua kupita mazima na I'd name zao , walio kubali kudhalikika leo hii wapo ila kwa tahadhari sana.

Mleta mada miezi sita mbele hamna aakae jua kama kuliwahibiuwa na mtu kama huyu hapa jf, maybe ajitoe sana ufahamu.
HUYO WA MWANZA ALIKUWA ANAITWA CUTELOVE
 
Nasikitika sana nikiona wanawake kwa wanawake hatupendani, sisi tulipaswa kunyanyuana, kulindana, kuteteana lakini ndio tunakua wa kwanza kusemana na kushushana,
Ifike mahala tujirekebishe, sijapenda
 
wewe sasa unaelewa chanzo na si mara moja wala id moja unazishuhudia zikifanya hivi! mada nyingine tu mtu anakuja kama kakata ringi duh!
Mimi naelewa kinachoendelea yaani kuna watu huwa wakikosa attention kwenye maisha yao watatukana njia nzima. Kwani wasichana wangapi wanaojipodoa na kwenda sokoni ila hawasemeshwi na wala hawaombwi namba? Your on the peak just live it
 
Back
Top Bottom