Barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Dkt. John Pombe Magufuli.

Kwako Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Natumai unaendelea vizuri na shughuri zako za kila siku.

Mimi ni kijana wako mtanzania halisi mpenda maendeleo na mchapa kazi wa kweli.
Nakupongeza kwa kuendelea kuishikilia vyema sera ya kujenga viwanda Tanzania ili kuweza kuinua uchumi wa nchi yetu.

Mh. Rais ni kweli ili nchi yeyote iweze kuendelea inahitaji, moja miundo mbinu bora na imara, viwanda, bila kuisahau elimu n. k.

Katika swala la viwanda mh Rais ni kweli nchi inahitaji viwanda mh Rais, vikubwa kwa vidogo. Viwanda vikubwa vipo vya aina nyingi, kuna viwanda vya magari, viwanda vya kemikali n.k.

Ndugu Mh. Rais Mimi naomba niegemee kwenye viwanda vikubwa vya kemikali mfano viwanda vya mbolea za ammonia, urea, CAN, DAP n. k. Ni wazi kwamba asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania ni wakulima wadogo kwa wakubwa. Lakini hata waajiriwa katika makampuni mbalimbali huutumia muda wao unaobaki baada ya kazi kujishughurisha na kilimo. Na hili ndilo linafanya kilimo kionekane kuwa uti wa mgongo wa maisha ya Watanzania.

Hivyo basi kama tukiweza kutengeneza mbolea bora kupitia viwanda vyetu tutakuwa tumelinuafaisha taifa hili kwa kiasi kikubwa sana. Kuhusiana na soko, soko la mbolea Tanzania ni la uhakika japo tunahitaji kuwaelimisha wananchi kutotegemea kilimo cha msimu mmoja. Tukifanya hivyo biashara ya mbolea itakuwa ni ya uhakika.

Ndugu Mh. Rais nchi yetu imebarikiwa kuwa na gesi asilia (methane) ambayo ndio malighafi kuu katika utengenezaji wa mbolea. Ambapo katika utengenezaji huo methane hubadirishwa ili kupata carbon monoxide na hydrogen gesi. Baada ya hapo Nitrogen huchukuliwa angani na kuunganishwa na hydrogen kikemikali kwa kutumia Haber process na kupata ammonia.

Ammonia kama ammonia yenyewe tu ni mbolea ikiwa katika mfumo wa hewa au inaweza kubadirishwa kuwa katika mfumo wa, majimaji au yabisi. Lakini pia ile carbon monoxide nayo pia inaweza kubadirishwa kuwa carbon dioxide kisha kuunganishwa na ammonia na kutupatia mbolea ya urea. Kutokea kwenye urea hapo tunaweza kupata mbolea nyingi tu.

Mbolea ambazo tunaweza kuzipata kwa kuunganisha kemikali zingine na Ammonia ni
1. Carbamide (urea)
2.Monoammonium phosphate (MAP)
3.Diammonium phosphate(DAP)
4.Ammonium nitrate (AN)
5.Sodium nitrate
6.Calcium Ammonium Nitrate
7.Ammonium sulphate (SA)
8.Calcium Nitrate
9.Urea ammonium nitrate (UAN)

Ndugu Mh. Rais kutokana na maelezo yangu hapo juu nilikua napendekeza gesi yetu asilia itumike zaidi kutengenezea, mbolea ili tukiinue kilimo chetu. Kilimo kitawezesha nchi yetu kupanda zaidi kiuchumi pia.

Ndugu Mh Rais ili kutengeneza mbolea tunahitaji kiwanda kikubwa (Fertilizer Petrohemical Plant). Ni kweli kabisa kwamba ili kuwekeza na kujenga kiwanda inahitaji pesa nyingi kwa makadirio ni dola billion 3 ($3B) ambazo ni sawa na Sh Trillion 7.

Mimi nilikuwa napendekeza tujenge kiwanda kikubwa cha mbolea kupitia michango ya wananchi. Kwamba wakuu wetu wa wilaya waanzishe michango ya kujenga kiwanda cha mbolea, nadhani tukifanya hivyo hiyo trillion 7 ni ndogo sana. Badala ya kusubiria mabeberu waje wawekeze ni bora tutumie fedha zetu za ndani. Ndugu Mh. Rais Kama shule tulijenga viwanda hatuwezi shindwa.

Ni wazi kwamba tukiendelea kuwategemea mababeru waje na mitaji yao kuwekeza kwenye miradi yetu, tutachelewa sana kupata maendeleo yale tunayo yahitaji. Maana wahenga walisema mtegemea cha nduguye hufa maskini. Hivyo mimi naungana nawewe katika kutumia fedha zetu za ndani kujenga miradi yetu.

Ndugu Mh. Rais Mimi sina mengi
Nashukuru kwa kuipata barua yangu.

Jina: Meneja wa Makampuni
Elimu: BSc. Oil and Gas Chemistry (Aberdeen University)
 
Mkuu, mtumie huu ujumbe kwa address hiyo hapo chini
Screenshot_2020-07-14-15-23-03-84.jpg
 
Hilo wazo lako si geni miaka ya sabini ilipogunduliwa gesi asilia huko Songo Songo nia ilikuwa kujenga kiwanda cha Mbolea pale Kilwa kilichoitwa KILAMCO.
Kilamko ingekuwa mji wa watu 50,000. Nje kidogo ya Kilwa.
Nchi zenye gesi kama Qatar,Thailand ,Malaysia wameitumia kuzalisha:
Perfume
Plastic
Mafuta ya magari aina ya platinum
Gesi ya kuendeshea magari kama mabasi na daladala.
Urea
Tindikali
Umeme kama mitambo ya Ubungo na Kinyerezi.
Na kwa kuwa ina mazao mengi baadhi ya nchi wamekuwa hawataki kuuza gesi asilia nje ya nchi zao.
Sema Magufuli hawezi hili jambo kwakuwa vitalo vimeishauzwa kwa wageni.Na ni watu wachache wenye nia thabiti pia wenye real know how na uzoefu wa kina nayo ni big issue.
Malaysia aliibiwa na Shell miaka 100,Norway aliibiwa miaka 20.Sijui sisi tutaibiwa miaka mingapi hadi tutie akili?
 
Hilo wazo lako si geni miaka ya sabini ilipogunduliwa gesi asilia huko Songo Songo nia ilikuwa kujenga kiwanda cha Mbolea pale Kilwa kilichoitwa KILAMCO.
Kilamko ingekuwa mji wa watu 50,000. Nje kidogo ya Kilwa.
Nchi zenye gesi kama Qatar,Thailand ,Malaysia wameitumia kuzalisha:
Perfume
Plastic
Mafuta ya magari aina ya platinum
Gesi ya kuendeshea magari kama mabasi na daladala.
Urea
Tindikali
Umeme kama mitambo ya Ubungo na Kinyerezi.
Na kwa kuwa ina mazao mengi baadhi ya nchi wamekuwa hawataki kuuza gesi asilia nje ya nchi zao.
Sema Magufuli hawezi hili jambo kwakuwa vitalo vimeishauzwa kwa wageni.Na ni watu wachache wenye nia thabiti pia wenye real know how na uzoefu wa kina nayo ni big issue.
Malaysia aliibiwa na Shell miaka 100,Norway aliibiwa miaka 20.Sijui sisi tutaibiwa miaka mingapi hadi title akili?
Hakika Mungu atusaidie, maendeleo yataletwa na sisi wenyewe.
 
Wazo lako ni zuri sana mtoa mada. Ila kwa bahati mbaya hiyo sekta ya gesi ni kaa la moto kwa Rais Mgufuli! Ujanja wake wote, aliweza kuwabana tu wale jamaa wa Acacia na wenzao wengine, ila siyo Mabeberu walio uziwa hivyo vitalu vya gesi yetu asilia.

Kwenye suala la gesi naona amekubali kushindwa. Kitambo sana Serikali ya Ccm ilishawagawia Mabeberu wavune watakavyo zaidi kwa manufaa yao, huku sisi tukiambulia lile bomba la Dar Mtwara na ile mitambo ya Kinyerezi.

Usisahau pia Mikataba yenyewe ya uvunaji wa hiyo gesi ilipitishwa pale Bungeni enzi za JK nyakati za usiku na kwa haraka haraka ili Mabeberu wamilikishwe raslimali za Watanzania.
 
Mimi nilikuwa napendekeza tujenge kiwanda kikubwa cha mbolea kupitia michango ya wananchi. Kwamba wakuu wetu wa wilaya waanzishe michango ya kujenga kiwanda cha mbolea, nadhani tukifanya hivyo hiyo trillion 7 ni ndogo sana. Badala ya kusubiria mabeberu waje wawekeze ni bora tutumie fedha zetu za ndani. Ndugu Mh. Rais Kama shule tulijenga viwanda hatuwezi shindwa.

Ni wazi kwamba tukiendelea kuwategemea mababeru waje na mitaji yao kuwekeza kwenye miradi yetu, tutachelewa sana kupata maendeleo yale tunayo yahitaji. Maana wahenga walisema mtegemea cha nduguye hufa maskini. Hivyo mimi naungana nawewe katika kutumia fedha zetu za ndani kujenga miradi yetu.

Ndugu Mh. Rais Mimi sina mengi
Nashukuru kwa kuipata barua yangu.

Jina: Meneja wa Makampuni
Elimu: BSc. Oil and Gas Chemistry (Aberdeen University)
Naunga mkono hoja, na huu ndio uzalendo wa kweli.
P
 
Biashara ya Petro-chemicals ni uwekezaki wenye return ya haraka sana na kutoa ajira kwa watu wengi sana kwa muda mfupi..

Mwafrica hawezi kupoteza muda na vitu vigumu, ngoja tuendelee kutia nia twende bungeni tukasosomole na wengine tuonekane kwenye uteuzi..Mwafrica anapenda mteremko na ile lugha ya kupiga kazi kwa maendeleo ya haraka nayakudumu kwake haiwezekeni..

Mkuu nenda tu kwenye marig kapige kazi ujenge ufalme wako na familia yako, hongera kwa degree ya aberdeen (home of oil and gas)...jitahidi kuwaencourage vijana,ndugu na jamaa wakasome hayo madude wawe madriller, fishing engineers, well completion engineers, tool pusher, motor man, roughneck, Trs etc wakapige hela mbele waendeshe mabenzi kwa marehemu babu yao Nyerere hapa tuwaachie wanasiasa nchi yao na mambo ya kusadikika wakiendelea kuwaambia vijana siasa ni ajira..
 
Back
Top Bottom