Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Dkt. John Pombe Magufuli.
Kwako Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Natumai unaendelea vizuri na shughuri zako za kila siku.
Mimi ni kijana wako mtanzania halisi mpenda maendeleo na mchapa kazi wa kweli.
Nakupongeza kwa kuendelea kuishikilia vyema sera ya kujenga viwanda Tanzania ili kuweza kuinua uchumi wa nchi yetu.
Mh. Rais ni kweli ili nchi yeyote iweze kuendelea inahitaji, moja miundo mbinu bora na imara, viwanda, bila kuisahau elimu n. k.
Katika swala la viwanda mh Rais ni kweli nchi inahitaji viwanda mh Rais, vikubwa kwa vidogo. Viwanda vikubwa vipo vya aina nyingi, kuna viwanda vya magari, viwanda vya kemikali n.k.
Ndugu Mh. Rais Mimi naomba niegemee kwenye viwanda vikubwa vya kemikali mfano viwanda vya mbolea za ammonia, urea, CAN, DAP n. k. Ni wazi kwamba asilimia kubwa ya wananchi wa Tanzania ni wakulima wadogo kwa wakubwa. Lakini hata waajiriwa katika makampuni mbalimbali huutumia muda wao unaobaki baada ya kazi kujishughurisha na kilimo. Na hili ndilo linafanya kilimo kionekane kuwa uti wa mgongo wa maisha ya Watanzania.
Hivyo basi kama tukiweza kutengeneza mbolea bora kupitia viwanda vyetu tutakuwa tumelinuafaisha taifa hili kwa kiasi kikubwa sana. Kuhusiana na soko, soko la mbolea Tanzania ni la uhakika japo tunahitaji kuwaelimisha wananchi kutotegemea kilimo cha msimu mmoja. Tukifanya hivyo biashara ya mbolea itakuwa ni ya uhakika.
Ndugu Mh. Rais nchi yetu imebarikiwa kuwa na gesi asilia (methane) ambayo ndio malighafi kuu katika utengenezaji wa mbolea. Ambapo katika utengenezaji huo methane hubadirishwa ili kupata carbon monoxide na hydrogen gesi. Baada ya hapo Nitrogen huchukuliwa angani na kuunganishwa na hydrogen kikemikali kwa kutumia Haber process na kupata ammonia.
Ammonia kama ammonia yenyewe tu ni mbolea ikiwa katika mfumo wa hewa au inaweza kubadirishwa kuwa katika mfumo wa, majimaji au yabisi. Lakini pia ile carbon monoxide nayo pia inaweza kubadirishwa kuwa carbon dioxide kisha kuunganishwa na ammonia na kutupatia mbolea ya urea. Kutokea kwenye urea hapo tunaweza kupata mbolea nyingi tu.
Mbolea ambazo tunaweza kuzipata kwa kuunganisha kemikali zingine na Ammonia ni
1. Carbamide (urea)
2.Monoammonium phosphate (MAP)
3.Diammonium phosphate(DAP)
4.Ammonium nitrate (AN)
5.Sodium nitrate
6.Calcium Ammonium Nitrate
7.Ammonium sulphate (SA)
8.Calcium Nitrate
9.Urea ammonium nitrate (UAN)
Ndugu Mh. Rais kutokana na maelezo yangu hapo juu nilikua napendekeza gesi yetu asilia itumike zaidi kutengenezea, mbolea ili tukiinue kilimo chetu. Kilimo kitawezesha nchi yetu kupanda zaidi kiuchumi pia.
Ndugu Mh Rais ili kutengeneza mbolea tunahitaji kiwanda kikubwa (Fertilizer Petrohemical Plant). Ni kweli kabisa kwamba ili kuwekeza na kujenga kiwanda inahitaji pesa nyingi kwa makadirio ni dola billion 3 ($3B) ambazo ni sawa na Sh Trillion 7.
Mimi nilikuwa napendekeza tujenge kiwanda kikubwa cha mbolea kupitia michango ya wananchi. Kwamba wakuu wetu wa wilaya waanzishe michango ya kujenga kiwanda cha mbolea, nadhani tukifanya hivyo hiyo trillion 7 ni ndogo sana. Badala ya kusubiria mabeberu waje wawekeze ni bora tutumie fedha zetu za ndani. Ndugu Mh. Rais Kama shule tulijenga viwanda hatuwezi shindwa.
Ni wazi kwamba tukiendelea kuwategemea mababeru waje na mitaji yao kuwekeza kwenye miradi yetu, tutachelewa sana kupata maendeleo yale tunayo yahitaji. Maana wahenga walisema mtegemea cha nduguye hufa maskini. Hivyo mimi naungana nawewe katika kutumia fedha zetu za ndani kujenga miradi yetu.
Ndugu Mh. Rais Mimi sina mengi
Nashukuru kwa kuipata barua yangu.
Jina: Meneja wa Makampuni
Elimu: BSc. Oil and Gas Chemistry (Aberdeen University)