Uchaguzi 2020 Barua ya Wazi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu Mwenendo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu (2020) za Mheshimiwa Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Barua ya Wazi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu Mwenendo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu (2020) za Mheshimiwa Tundu Lissu

Lissu anaeleweka kwa wapuuzi tu vibaka waliokosa cha kufanya wanahitaji pesa ya kuja ghafla mfukoni....kama unapiga kazi halali huna neno juu ya magufuri..



Ukweli ni kuwa magufuri anashinda kwa kishindo kikubwa mno ijapokuwa sinaga mambo ya uvyama ila kila maeneo unayopita ushindi uko wazi.alichokosea lissu ni kuwa na siasa za kulalamika kupigwa na hajui nani kampiga.....watanzia wapo wengi wenye matatizo yao awe na siasa za ushawishi siyo za kupaniki ili tuone ana uchungu kumbe ana ajenda yake ya kufinywa kinyeo na wazungu.
Kwanza nakukanusha. Kama huna uvyama ungemuelewa lissu. Lissu halalamiki bali ni political technique ya kumattack mpinzani wako. Lazima lissu aseme mabaya ya magu ili watu wajue maana wanadanganywa sana. Kila anakopita lissu anaongekea ilani ya chama chake.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Sasa hivi ni kipindi cha kampeni, haivumiliki kuongea uongo ambao unaweza kuleta madhara makubwa kwenye umoja, amani na mshikamano wetu Kama taifa.

Tindu Antipas Lissu akataliweeeeeee
Ni uingo upi lissu kasema? Ishu ya zanzibar katoa reference kwa kuwaambia wakasome kitabu kinachoitwa "kwaheri ukoloni, kwaheri uhuru". Nawe kitafute usome afu uje useme wapi lissu kadanganya

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Kura zinapigwa nchi nzima na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ndio inayokusanya, kujumlisha na kutangaza matokeo. Kwa upande wa ubunge na udiwani wanaweza kwenda mahakamani Ila kwa upande wa urais ikishatangazwa imetangazwa na yeye Kama wakili msomi anajua hilo, Sasa barabarani anafuata nini Kama sio kutaka kugongwa na magari?

This time around ndo utajua kuwa wenye akili hawawezi vumilia upam.bavu sababu ya sheria za kibumbavu. Stay tuned!
 
Ana makando kando kibao including kuwa mshukiww wa kwanz wa wasiojilikana. Ni mtu wa kutilia shaka ktk kila angle ya uhalifu tangu ashike madaraka.
"Everyone is innocent against allegations on him//her until proven guilty beyond reasonable doubt" by Amani on Jamii forum 2020
 
Amesema ataingiza watu barabarani ilihali akijua fika njia hiyo ni njia mbaya. Akiona ameonewa, zipo njia za kufuata. Kama vipi anione, nitamshauri bureee email

Awali nilijua una shida ila sio kubwa kama nilivyofikiri. Wewe una ubavu wa kushauri nini matokeo ya urais yakishatangazwa wakati katiba yenyewe inasema hata mahakama haiwezi kutengua matokeo ya urais?
 
Hadi hao wafugaji watakuwa wameshangazwa na Lissu badala ya kuwaambia walau atawatengea sehemu ya misitu ya akiba watumie kwa shughuli zao; yeye anadai akichaguliwa wataenda kulisha mifugo mbugani kabisa kwa raha zao.

Imagine hali ya NEC na vyombo vya ulinzi tangia ameingia Tanzania kuanzia kuvunja kanuni za uchaguzi kwa kuanza campaign mapema, uhamasishaji wa ghasia, mara sijui anataka kutengenezewa ajali ya ndege na jana kaja na hoja za kuvunja muungano nina uhakika huko NEC washamchoka huyo Lissu kwa sasa awajui wafanye nae nini.
Kama wamemchoka wamchukulie hatua za kisheria. Nyie uvccm cjui akili zeny mnaweka wapi

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Ni uingo upi lissu kasema? Ishu ya zanzibar katoa reference kwa kuwaambia wakasome kitabu kinachoitwa "kwaheri ukoloni, kwaheri uhuru". Nawe kitafute usome afu uje useme wapi lissu kadanganya

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Hata shetani alimjaribu Yesu kwa kutumia maandiko.
Shetani: Kama kweli wewe ni mwana wa Mungu, jitupe katika mwamba huu maana imeandikwa atakuagizia malaika wake wakuchukue mikononi mwao".

Yesu: "imeandikwa, usimjaribu bwana Mungu wako".
 
Kwa kweli kampeni zake zinapandikiza chuki,woga na kuchochea vita.ni bahati mbaya kuwa na mgombea wa namna hii.sijui taifa litafanyeje kuunganisha wananchi ambao amewatawanya kwa kiwajaza chuki zisizo na msingi.
Lissu anawapa somo watu. Mfano pale zanzibar alikuwa anapiga pindi la history kuhusu muungano. Sasa nyie na ushamba wenu mshaona hawa watu wakielimika watajawa na chuki dhidi ya mfumo huo kandamizi. Hizo sio chuki bali ni kufunguliwa ufahamu.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Ndugu mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),

Ninachukua fursa hii kukupongeza wewe na timu yako kwa kazi ngumu mnayoifanya. Mnafanya kazi zenu kwa weledi na kwa mujibu wa sheria. Hongereni sana.

Kama inavyofahamika, nchi yetu hufanya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani kila baada ya Miaka mitano. Hii ni kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ambayo ni nchi inayofuata demokrasia ya vyama vingi.

Ndugu mwenyekiti, mwaka huu, 2020 Tanzania itafanya Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Tayari kampeni za uchaguzi zimeanza kote nchini huku vyama mbalimbali vikizunguka kunadi ilani zao za uchaguzi.

Itakumbukwa kuwa lengo la kampeni hizo Ni kunadi sera za chama husika ili wananchi waweze kufanya maamuzi sahihi siku ya kupiga kura. Kampeni hizi zinatawaliwa na kanuni, sheria na taratibu pamoja na utamaduni wetu Kama watanzania. Hivyo, haitarajiwi kampeni hizi kutumika Kama sehemu ya kuwagawa Watanzania.

Hivi karibuni tumeshuhudia vitendo kadhaa vya uvunjifu wa amani ambavyo mara zote hufanywa na chama kimoja tuu, CHADEMA. Kabla ya kuanza kampeni, tulimsikia Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CHADEMA akiweka wazi kuwa atawaingiza watanzania barabarani Kama hatatangazwa mshindi. Tuliahihudia waandishi wa TBC wakifukuzwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA pale mbagala kwenye viwanja vya zakhiem.

Tundu Lissu akiwa jijini Mbeya aliendeleza mashambulizi kwa viongozi wa nchi kuwa itawaka Moto usiozimika. Huku akijua kabisa analengo gani, anaweza hoja za kuwa atadhuriwa huku akijenga hoja "kijanja" na kuwatumbukiza viongozi wa nchi ili wananchi wakoae imani na viongozi hao.

Kubwa kuliko Ni kauli yake aliyoyafanya Zanzibar akisema Hayati mzee Karume alilazimishwa kusaini makubaliano ya Muungano kinyume na mapenzi yake. Aliunda mbali zaidi kuwaambia ndugu zetu wazanzibar wanachaguliwa viongozi wao na Tanganyika huku akijua fika kuwa vikao hufanyika Dodoma kwasababu ndio makao makuu ya chama cha Mapinduzi.

Kauli hizi anazitoa sio kwa bahati mbaya kwani Mheshimiwa Lissu ni wakili msomi mwenye weledi mkubwa wa masuala ya kisheria. Anafanya hivi kwa makusudi akitumia utaalamu wake wa kisheria kuwashawishi watanzania kuamini uongo ambao unaweza kupelekea uvunjifu wa amani.

Ninaomba nikiwa Kama mtanzania mzalendo ninayeipenda nchi yangu kuwa Mheshimiwa Lissu aonywe na aelekezwe kujikita kwenye kueneza sera za chama chake. Ni muhimu Mheshimiwa Lissu akumbushwe kuwa Kuna maisha baada ya Uchaguzi. Mimi na yeye tunaweza tusiwepo, Ila watanzania amvao Ni ndugu, rafiki na watoto wetu wayendelea kuwepo. Hawa wanastahili kesho bora zaidi.

Ni vema Mheshimiwa Lissu akakumbushwa kuwa viongozi wa kisiasa Kama yeye ni watu wenye ushawishi kwa wafuasi wao na kuwa maneno yao yanaweza kuleta Faraja au huzuni, kilio au furaha, upendo au chuki, umoja au utengano zaidi sana kifo au maisha.

Amani Msumari
Tanga

Nakala:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania
Katibu Mkuu - CHADEMA
Katibu Mkuu - CCM
Nchi imeharibiwa sana hakuna utawala wa haki na sheria. Tusiwe washabiki wa dhulma; ni makosa makubwa, ni sawa kuanza kula nyama ya Binadamu, haitaishia hapo! Ukimaliza wapinzani utaanza kudhulumu ccm wenzio, kwani hatujashuhudia haya?
Nape Nauye aliwahi kunyooshewa bastola mchana kweupeee na maccm wenzake.
 
Acha uongo basi.
Jimbo la Tanga mjini, Arusha mjini, Kibamba, Ubungo, Mbeya mjini n.k yalikuja chini ya upinzani na yamepelekewa Maendeleo. So piga kimya mzee baba.

Tukusikilize wewe au mwenyekiti wa chama anaetoa vitisho kwa wapiga kura kwenye kampeni ikiwa hawatachagua ccm watajuta na maendeleo watayasikia tu? Unataka ushahidi gani tena?
 
Nchi imeharibiwa sana hakuna utawala wa haki na sheria. Tusiwe washabiki wa dhulma; ni makosa makubwa, ni sawa kuanza kula nyama ya Binadamu, haitaishia hapo! Ukimaliza wapinzani utaanza kudhulumu ccm wenzio, kwani hatujashuhudia haya?
Nape Nauye aliwahi kunyooshewa bastola mchana kweupeee na maccm wenzake.
Kamwe siwezi kutetea uovu na dhulma, nitavipinga daima.
 
Maneno anayotamka yako wazi. Huyu jamaa amejipanga kumwaga damu

Unataarifa kwamba damu yake nyingi ilimwagwa kihuni tu na wapumbavu wachache ambao bila aibu hadi leo wanasema hawajui kitu gani kilitokea? Mbaya zaidi mmoja tena mwenye dhamana ya usalama wa raia anasema wanamtafuta TAL.
 
Hakuna njia za kisheria za kupinga matokeo ya Urais acha kuandika uongo.
walokataza kuhoji matokeo mahakamani ndio watakaotuletea shida, maana wametuachia option moja tu ya lissu
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Point hapo ni " Uchaguzi wa huru a haki". Ikitokea umeona hujatendewa haki basi Kuna njia za kisheria za kufuata na sio kumwaga damu ya wananchi
Hiyo haki MAALIM SEIF alipewa lini tofauti na kufuta uchaguzi
 
Nani kakwambia??? Lissu anashinda kihalali uchaguzi huu kwa sababu watanzania tumemuelewa kweli na Sera zake!
Sio kuwa atashinda, hata sasa anashinda sana na njaa. Hilo sio jema kwa afya yake. Ushindi wa kura huo atasubiri Sana. Watanzania wanamrudisha, jembe na mzalendo #1 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili aendeleze mambo makubwa aliyoyafanya na akamilishe ndoto za watangulizi wake.
 
CCM Wamefanya kampeni miaka 5 hakuna aliyewazuia..
Acha kuwapangia wenzio cha kuongea.. Mlipotaka kumtoa uhai hamkumwaga damu?
Waliozamishwa ziwani na kuchomewa nyavu zao sio damu hiyo?
Waliotekwa, kupotezwa na kuokotwa wamekufa sio damu ni mkojo wako sio?
 
Hapa
Tundu Lissu shikilia hapo hapo baba...... imeisha hiyo!
Hapati kitu tanzania hapa, na atakae enda barabarani ajipange kuishi mapolini kama nyumbu na sio mapoli ya tanzaia kwa sababu nyumbu wetu wa Serengeti ni wastaarabu, sema ahawatumii akiri wanapo vuka MTO.
 
Back
Top Bottom