Uchaguzi 2020 Barua ya Wazi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu Mwenendo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu (2020) za Mheshimiwa Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Barua ya Wazi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu Mwenendo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu (2020) za Mheshimiwa Tundu Lissu

Kuna kitu Umesahau sijui nikukumbushe anyway , Umesahau hujaacha namba zako za simu
Amesema Kama ataibiwa kura ataitisha maandamano ya amani.sasa haraka za kuja huku umevaa soksi juu ya viatu kunatoka wapi.eti nakala kwa igp wa polisi ama kweli akili Ni nywele.
 
Mgombea wa CCM anapotishia kuwanyima wananchi maendeleo warakapochagua wapinzani unaona ni siasa safi!!

Mgombea wa CCM anapokatisha masomo wanafunzi ili wakasikilize wasichoweza kujibia mitihani unaona sahihi na hukisemi!

Mgombea wa CCM anapohutubia Kisukuma Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita unaona sawa na husemi!

Wewe ni mwanaCCM unatakiwa kuwaeleza wanaCCM wenzio kwenye platform yenu.
Ni yeye, wamewashika pabaya
 
nimekuelewa mkuu wangu , ila mkuu tulipofika nipazuri , namaanisha kwa sasa lissu hajibiwe kwa hoja , na zipo nyingi za kumjibu, kuliko kuchukua vitu vidogo kuvifanya agenda , hii ni kufanya hata ambae alisha sahau aanze kukumbuka , mfano zipo njia 4 7 katika ushindi na katika upanguaji wa hoja je mmeshindwa zitumia baadhi ili kumjibu lissu, mpaka mkuu muhanze tafuta huruma ya tume , shida nini , mkuu
Mkuu shida ni kuwabtunataka amani na unoja wetu udumu na kuwa hatutamvumiliaa yeyote anauetaka kupoka vitu hivyo
 
Na cha kushangaza hata mpira wa miguu watu wanakata rufaa lakini si matokeo ya Uchaguzi wa Urais!

Hakuna njia za kisheria za kupinga matokeo ya Urais acha kuandika uongo.
 
Ndio na kwa hakika hilo wanalijua vizuri tu! Huu mwingine ni ubishi kama wa Magu.
Hilo la kura za vijijini umelisema wewe, mimi nilikuletea na kuongezea Hilo la kura za bure ukidhani vijijini hawajielewi. So usinilishe maneno. Baki mwenyewe na dhambi yako ya ubaguzi
 
Uraisi wa JMT na SMZ hupingwi mahakaman wala popote ndio maana 2015 Jecha alifanya take
Safari hii tunawaambia ninyi watu wa system hatuwaachi salama
Njia pekee ya kupinga uraisi wa jiwe ni kuingia barabaran na mawe
Ninyi njooni na risasi mungu atakuwa kwetu tutawashinda
Barabaranibtutaingia kwaajili ya Usafiri, mazoezi na kutembea lakini so kwaajili ya vurugu.
 
Ndugu mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),

Ninachukua fursa hii kukupongeza wewe na timu yako kwa kazi ngumu mnayoifanya. Mnafanya kazi zenu kwa weledi na kwa mujibu wa sheria. Hongereni sana.

Kama inavyofahamika, nchi yetu hufanya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani kila baada ya Miaka mitano. Hii ni kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ambayo ni nchi inayofuata demokrasia ya vyama vingi.

Ndugu mwenyekiti, mwaka huu, 2020 Tanzania itafanya Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Tayari kampeni za uchaguzi zimeanza kote nchini huku vyama mbalimbali vikizunguka kunadi ilani zao za uchaguzi.

Itakumbukwa kuwa lengo la kampeni hizo Ni kunadi sera za chama husika ili wananchi waweze kufanya maamuzi sahihi siku ya kupiga kura. Kampeni hizi zinatawaliwa na kanuni, sheria na taratibu pamoja na utamaduni wetu Kama watanzania. Hivyo, haitarajiwi kampeni hizi kutumika Kama sehemu ya kuwagawa Watanzania.

Hivi karibuni tumeshuhudia vitendo kadhaa vya uvunjifu wa amani ambavyo mara zote hufanywa na chama kimoja tuu, CHADEMA. Kabla ya kuanza kampeni, tulimsikia Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CHADEMA akiweka wazi kuwa atawaingiza watanzania barabarani Kama hatatangazwa mshindi. Tuliahihudia waandishi wa TBC wakifukuzwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA pale mbagala kwenye viwanja vya zakhiem.

Tundu Lissu akiwa jijini Mbeya aliendeleza mashambulizi kwa viongozi wa nchi kuwa itawaka Moto usiozimika. Huku akijua kabisa analengo gani, anaweza hoja za kuwa atadhuriwa huku akijenga hoja "kijanja" na kuwatumbukiza viongozi wa nchi ili wananchi wakoae imani na viongozi hao.

Kubwa kuliko Ni kauli yake aliyoyafanya Zanzibar akisema Hayati mzee Karume alilazimishwa kusaini makubaliano ya Muungano kinyume na mapenzi yake. Aliunda mbali zaidi kuwaambia ndugu zetu wazanzibar wanachaguliwa viongozi wao na Tanganyika huku akijua fika kuwa vikao hufanyika Dodoma kwasababu ndio makao makuu ya chama cha Mapinduzi.

Kauli hizi anazitoa sio kwa bahati mbaya kwani Mheshimiwa Lissu ni wakili msomi mwenye weledi mkubwa wa masuala ya kisheria. Anafanya hivi kwa makusudi akitumia utaalamu wake wa kisheria kuwashawishi watanzania kuamini uongo ambao unaweza kupelekea uvunjifu wa amani.

Ninaomba nikiwa Kama mtanzania mzalendo ninayeipenda nchi yangu kuwa Mheshimiwa Lissu aonywe na aelekezwe kujikita kwenye kueneza sera za chama chake. Ni muhimu Mheshimiwa Lissu akumbushwe kuwa Kuna maisha baada ya Uchaguzi. Mimi na yeye tunaweza tusiwepo, Ila watanzania amvao Ni ndugu, rafiki na watoto wetu wayendelea kuwepo. Hawa wanastahili kesho bora zaidi.

Ni vema Mheshimiwa Lissu akakumbushwa kuwa viongozi wa kisiasa Kama yeye ni watu wenye ushawishi kwa wafuasi wao na kuwa maneno yao yanaweza kuleta Faraja au huzuni, kilio au furaha, upendo au chuki, umoja au utengano zaidi sana kifo au maisha.

Amani Msumari
Tanga

Nakala:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania
Katibu Mkuu - CHADEMA
Katibu Mkuu - CCM
Haya ni Maadili ya Uchaguzi wa Urais, Wabunge na Madiwani, 2020. Msisitizo kwa kinachofanyika kanda ya Ziwa.

Hiyo ni aya 2.1 (k) ikieleza wajibu wa Chama cha Siasa. Kwenda kinyume na maadili haya ni kosa linaloweza kufikishwa katika kamati ya Maadili na kutolewa uamuzi ikiwa ni pamoja na Chama kilichokosea kuzuiwa kufanya kampeni.
Screen Shot 2020-09-08 at 7.25.06 PM.png


ADHABU ZINAZOWEZA KUTOLEWA NA KAMATI ZA MAADILI


Screen Shot 2020-09-08 at 7.37.59 PM.png


Uwezo wa mlalamikaji au mlalamikiwa kufungua kesi mahakamani ikiwa hajaridhika na uamuzi wa Kamati ya Maadili (hii ni pamoja na nafasi ya Urais)

Screen Shot 2020-09-08 at 7.38.23 PM.png


Uamuzi wa Jumla kuhusu chama kutotekeleza maadili ya Uchaguzi
Screen Shot 2020-09-08 at 7.37.41 PM.png
 
Wakuu, Hivi Jukwaa la Siasa limeondolewa? Maana silioni kila napolitafuta
 
Narudia tena, bila machafuko sioni mabadiliko, Afrika hakuna mabadiliko ya kunyimwa haki bila machafuko. Vinginevyo isingewezekana kilio cha tume huru ya uchaguzi na matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani kizidi 25yrs bila kurekebishwa kwa amani. Kwa taarifa yako kukitokea machafuko, tume ya uchaguzi ndio itakuwa ya kwanza kufanyiwa marekebisho. Amani haiji ila kwa ncha ya upanga fullstop.
Hapana hapana hapana Mara tatu
 
Hapana hapana hapana Mara tatu

Nilichokuambia sujakuambia kwa bahati mbaya, nimekuambia nikiwa na akili zangu timamu. Ndio maana huna maelezo kwanini mbali ya kudhihirika marais wetu kuwa sio waadilifu, waendelee kuwa wachaguzi na wasimamizi wa tume ya uchaguzi? Kinachofanya tume isibadilishwe muundo wake, ni kwasababu ya marais wetu wasio waadilifu. Huu ukondoo uitwao amani, ndio pekee unafanya hiyo tume kuendelea kuundwa kwa utashi wa marais wahuni, na wenye uchu wa madaraka.
 
Nilichokuambia sujakuambia kwa bahati mbaya, nimekuambia nikiwa na akili zangu timamu. Ndio maana huna maelezo kwanini mbali ya kudhihirika marais wetu kuwa sio waadilifu, waendelee kuwa wachaguzi na wasimamizi wa tume ya uchaguzi? Kinachofanya tume isibadilishwe muundo wake, ni kwasababu ya marais wetu wasio waadilifu. Huu ukondoo uitwao amani, ndio pekee unafanya hiyo tume kuendelea kuundwa kwa utashi wa marais wahuni, na wenye uchu wa madaraka.
Sema yote lakini uadilifu wa Rais Magufuli sio wa kutiliwa shaka hata kidogo.
 
Back
Top Bottom