Barua ya wazi kwa Tundu Lissu kumuonya dhidi ya kutetea masikini na wapumbavu

Mbona barua hii haimuhusu
Haimhusu kivipi wakati yeye ni rais wa wanyonge hao ambao ni maskini na wapumbavu.

Najua umetumia fasihi kumfikishia ujumbe. Jiandae tunakutafuta ukaeleze upupu mbele ya wazee wa kazi .
 
Niliipitiaga kipindi kabla hata lissu hajarudi bongo nadhan, niliielewa sana na niliiafiki, ktk wakt huu nilikuwa naitafuta sana hii mada bt hatimae imefufuliwa so umeongea ukweli mtupu mkuu, unapigania wa pumbavu na wajinga.
 
Haimhusu kivipi wakati yeye ni rais wa wanyonge hao ambao ni maskini na wapumbavu.

Najua umetumia fasihi kumfikishia ujumbe. Jiandae tunakutafuta ukaeleze upupu mbele ya wazee wa kazi .

Wewe ni panya mdogo tuu,
Jina hilo hapo, namba hizo hapo na location nimekuwekea huna haja ya kunitafuta, piga simu nije. Sitishwagi na panya
 
Unasema, awatetee matajiri na wenye uwezo na akili, SAWA....

Unasema aachane na masikini na wapumbavu kwa sababu hao hao ndiyo wanaoweza kumgeuka na kuanza kumponda mawe, SAWA....

Logic ya hoja hii ni kuwa ajiunge na matajiri, watawala na wanaonyanyasa na kuonea masikini...

Hawa ndiyo kina Magufuli na maCCM wenzake... HII SIYO SAWA. Nitaeleza kwanini;

βˆšβ€’ Umetoa mifano ya watetezi wa masikini wa kale kina Mussa na Yesu Kristo...

Kwamba, hawa masikini waliwageuka hawa wanaharakati na watetezi wao kwa kuwapiga kwa mawe (Mussa) na kuuwawa kabisa (Yesu Kristo)...

βˆšβ€’ Ni kweli, ndivyo ilivyokuwa. Na infact hii ndiyo gharama (price) ya kutetea masikini. Na yeyote anayejitosa kutetea masikini na wajinga anapaswa kujua kuwa anatetea watu ambao hata hawaelewi kuwa wako utumwani na hawastahili kuwa hivyo walivyo. Wao wanajua, hayo ndiyo maisha na stahili yao...

βˆšβ€’ Kwa mwanaharakati yeyote wa haki za binadamu ambaye hajui gharama ya harakati zake, ni vyema asishiriki kabisa kutetea na kuwakomboa masikini, wajinga na wapumbavu...

βˆšβ€’ Lengo la kuwatetea masikini, wajinga na wapumbavu ni ili huo umasikini wao na ujinga wao na upumbavu wao uwatoke. Ili umtibu kichwa, sometimes utalazimika kula makonde na mateke...

βˆšβ€’ Ndivyo ilivyokuwa na ndilo lengo la Mungu aliyewatuma Mussa na Yesu Kristo. Hawa mitume, walijua kabisa wanawatetea na kuwaongoza watu wasiojielewa walq kujitambua, wasiojua wajibu na haki zao...

KWA HIYO;

Binafsi, sikubaliani na onyo lako la kumtaka Tundu Lissu kuachana na mission yake, kuachana na harakati zake kuwatetea masikini na wajinga wengi...

Akiacha ni nani atafanya kazi hiyo?

Umesema, masikini hawa watatetewa na kukombolewa na Mungu muumba wao...

Hii ni kweli kabisa, kwamba Mungu muumba ndiye mkombozi wetu...

Lakini Mungu hawezi kushuka yeye physically na kuanza kufanya kazi hii. Mungu huwatumia watu na kuwapa uwezo wake kufanya kazi ya kukomboa na kutetea watu wake...!

Mimi ningependa kuwaona watu wa aina ya Tundu Lissu na wengine wasonge mbele so long as wana wito wa kuwakomboa na kuwatetea ndugu zao masikini na wajinga wanaoonewa na kunyanyasika maana wafanyalo hakika ni mapenzi ya Mungu Yehova....!!
 
Mwandishi hongera kwa uwezo na kipaji cha uandishi. Ila kwa upande wa mantiki andiko lako ni general falacy.

Ulichokiandika kina ukweli katika mazingira flani ila haina ukweli wa jumla.

Ulichokiandika hakina back up ya kimantic na kihistoria ya maumbile bali ni hisia na imagination tu.

Funzo la historia ni kuwa reward iko kwa mtu aliyepigana kuleta au kuongeza thamani kwenye humanity

Unyonyaji, ubinafsi , kutokuwajibika na kujinufaisha kuliwezesha watu kujenga makasri, kumilki nguvu ya kiutawala na kunufaisha wachache. Kwa bahati mbaya mambo kama haya hayajawahi kuthaminiwa wala kukumbukwa na vizazi bali wahusika wanapokufa na historia yao uzimika kama mshumaa.

Najiuliza Nyerere angekua na akili kama hizi taifa letu lingekuaje?

Najiuliza Nelson mandela angekua na akili za kibnafsi kama hizi SA historia yake ingekuaje?

Najiuliza Patrick Limumba angekua na akili kilema kama hizi harakati za pan africanism zingekua wapi ?

Twende sasa kwenye hoja ya msingi.

Imagine Musa, joshua, Samsoni, Daudi, Isaya, Yeremia na wengine kama hao ambao walitoa maisha yao ya kitume kujaribu kuongeza heshima kwenye utu wa mwanadamu, wengi wao walipitia magumu sana ila wito wao uliwafanya wafike mwisho.

Jamii zote zina matabaka . Liko tabaka lenye nguvu na tabaka la malofa na lingine ni tabaka la kati. Kilicho cha ajabu harakati nyingi uhibuka kulitetea kundi la malofa ambalo umeliita la masikini na wapumbafu. Sijui kwa nini hakuna historia inayoonyesha harakati ya jamii ililenga kulifanya tabaka lenye nguvu liimarike na kuzidi kuwa bora zaidi. Nazani kuna uungu na nguvu ya kiasili ambayo mwanadamu ameumbiwa ya kujali na kupenda kukiongezea thamani kilicho kinyonge.

Musa alichokifanya ni kuongeza thamani ya ndugu zake watumwa. Walimpinga toka nchi ya Misri ila kwa msaada wa Bwana kizazi kipya kilifaidi matunda ya kuishi kwenye nchi ya ahaadi ilijaa maziwa na asali.

Kristo pia alifanya the same. Alisalitiwa na rofa aliyemfanya rafiki na mwanafunzi. Aliposhikwa rafiki zake hawakuweza kumtetea, aliposurubiwa baadhi ya akina mama na wanaume wachache wanyonge waliishia kumlilia na kumbea. Thanks to God kumbe sadaka ya kifo chake kimekua msingi wa maisha ya matumaini kwa vizazi vyote duniani. Ni mpambanaji na mwanafalsafa mwenye wafuasi wengi kuliko wote waliowahi kuishi. Injiri yake inanguvu hadi leo. Mafundisho yake yakifanyiwa reference hadi leo wakuu na wenye mamlaka wanapiga magoti hata kama ni kwa unafiki?

Kwa mifano chanya kama hii ambayo inaongeza thamani katika maisha ya binadamu nani atasimama na kuwaziba midomo wana harakati , watetezi wa wanyonge, sauti ya wasio na nguvu kama hawa?

Tundu lisu ni miongoni mwa nafsi zilizojitoa sadaka. Achilia maumivu anayotembea nayo mwilini mwake na moyoni mwake ila amebaki kama mshumaa wa shujaa kwa jamii hii ya kitanzania.

Tulio wengi tutamuombea daima na mungu amtangulie.
 

Here we Goo
 


Huwezi ukatetea masikini au wajinga ukafika popote
 
Lissu, watanzania wanakuelewa na ndiyo maana kama mifumo ya kiutawala ingekuwa sawa leo hii wewe ungekuwa Rais wa nchi. Tatizo la nchi yetu mifumo yote inatetea na kulinda utawala uliopo madarakani na ndiyo maana wewe unatuongoza leo tupate KATIBA MPYA ambayo itaweka sawa check & balance ya mihimili yote, na msingi wa utawala wa nchi yetu urudi mikononi mwa wananchi wenyewe.

Usikate tamaa, ukiona mbu wanashambulia miguuni kwa ushirikiano mkubwa basi elewa panakaribia kucha.
 


πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
A touch of genius - with a light touch, for sure. Salute!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…