1. Tusimamie haki, tutende haki na tuhamasishe watu wetu kutotumia nguvu inayo dhuru mtu, ua watu , kupoteza watu na kuharibu uchaguzi. Toka tulipoanza na tulipofikia kuna matukio mengi tayari (kwa mujibu wa picha na malalamiko). Tunakokwenda na baada ya uchaguzi matukio hayo yasiwepo kamwe.
2. Kuna maisha baada ya uchaguzi, maisha haya yanaweza yakawa ya kuhangaika na mahakama hapa nchini au nje ya nchi popote pale huwezi jua, kwa tetesi ni kwamba kuna ushahidi unakusanywa mwingi kwenye ngazi zote kutoka kwa waliodhurika, waliokuwepo eneo la tukio na wanaoishi maeneo ya tukio, ushahidi ni wa picha, makovu na sauti, hii ni mbaya sana kwetu sisi watanzania kufikia hatua hii au watu wengine wa nje kupewa ripoti kama hizi (kuna ripoti imeandikwa na mwanasheria flan ina ukurasa zaidi ya 27) hatujafurahia kuisoma sio nzuri kwetu mtu wa nje kupokea na kuandika.
3. Dunia imebadilika na watanzania wamesoma sana, sio kama ile ya miaka yote. Tukumbuke kilicho mtokea Rais wa Kenya, Makamu wake na mwandishi wa Habari hakikuwa kizuri, walihangaika sana na mahakama hawakuwa na amani mioyoni mwao, ni Umoja wa Africa tu ndio uliwasaidia kuwaombea wasishtakiwe kwa majukumu waliyo nayo ila walijuta na walisikitika sana kwa kilichotokea ndio maana sasa hivi maisha yao ya uongozi hawataki kamwe kujihusisha na lolote lile ovu maana wanaelewa, tunaweza tukajifunza kutoka kwao.
4. Madaraka yasitulevye, kuna maisha baada ya vyeo tulivyo navyo, tuandalie vizazi vyetu maisha mema ya badae, tusiache kumbukumbu ya vitu ambavyo havitaleta Baraka na havitaacha alama ya kazi nzuri kwa nchi yetu. Kisheria hamna mwenye hati miliki ya nchi ya Tanzania, kwanza Tanzania ipo kisheria kuanzia ngazi ya umoja wa mataifa hadi huku chini hakuna mwenye uwezo wakuongeza mipaka ya ramani yake nje ya nchi ndivyo ilivyo hakuna mwenye mamlaka wa kujimilikisha kuwa ni yakwake binafsi. Tutakufa tutaiacha na itaendelea kuwepo tu.
5. Ushahidi anao ukusanya huyu Robert Amsterdam kutoka kwa Mwananchi mmoja mmoja au makundi kama alivyoandika kwenye twitter yake; nimeambatanisha hapa, ipo siku tutashangaa aliupataje, sio mzuri tuhakikishe ushahidi huo haupatikani ni pamoja na kuwasisitiza watu tunao waongoza waache tamaa na wasimtendee yeyote yule chochote kile.
MUNGU ATUSAIDIE NA MUNGU AIBARIKI TANZANIA YETU