BASATA: Mwisho wa Ma-DJ, na MC kufanya kazi bila kujisajili ni Januari 31, 2026

BASATA: Mwisho wa Ma-DJ, na MC kufanya kazi bila kujisajili ni Januari 31, 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Basata.jpg
TAARIFA KWA UMMA

WAONGOZA SHEREHE, BURUDANI NA MATUKIO (MC), MANJU MUZIKI (DJ) NCHINI WATAKIWA KUJISAJILI NA KUWA NA KIBALI HAI CHA BASATA IFIKAPO TAREHE 31 JANUARI, 2026.

29 Disemba, 2025

Baraza la Sanaa la Taifa kupitia kanuni ya 18.- kifungu (1) (a) na (b) ni msajili mkuu na mtoa vibali vyote vya kufanya kazi za Sanaa na kutoa vibali kwa makampuni, wadau wanaotumia kazi za Sanaa.

Kanuni ya 20 ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa za mwaka 2018, zikisomwa kwa pamoja na Jedwali la Pili la Tozo za BASATA za Mwaka 2025, inaelekeza waongoza Sherehe, Burudani na Matukio (Mc), na Manju Muziki (DJ) kupata vibali vya BASATA kwa ajili ya kujishughulisha na kazi hizo.

Kwa taarifa hii, unaelekezwa kuzingatia takwa hilo la kikanuni kwa kuhakikisha unakuwa na KIBALI HAI cha BASATA hadi kufikia Tarehe 31 Januari, 2026, kibali hicho kitakupa uhalali wa kufanya shughuli za Sanaa, watakaofanya kinyume na utaratibu huo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao, ada ya usajili ni shilingi elfu kumi (10,000/=) na ada ya Kibali ni shilingi elfu arobaini (40,000/=), sajili sasa sanaa.go.tz

Kwa mawasiliano zaidi piga; 0625 662933 Mr. Abel Ndaga au 0767 499993 Mr. Gabriel Awe.

Imetolewa na:
Leonidas Tibanga
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Baraza la Sanaa la Taifa.
 
huku kwingine watu wanaiba pesa na kwenda kununua majumba nchi za ulaya...maskin anakamuliwa Hadi mwisho watasema Kodi ya kunya.
 
Mm tokq nilivyoona mawinga walifikiwa na madalali nikajua kweli nchi yetu ni matikiti maji matupu

Unamsaka mtu anaetafuta hela ya kodi na kula unamuacha mtu anaetia nchi nzima umaskini. Mm nasemaga bora nchi hii wizi wa fedha
Urasimishwe tu ili mtu akiiba alipe nusu yq hela tile kodina awekeze humuhumu ili ale na watanzania w3nzie
 
Wanaumwa hawa jamaa.

Taasisi mzigo kama hizi ni za kufutwa, wameshindwa kubuni vyanzo sahihi vya mapato wanataka kuishi na kula kupitia migongo ya watu.
 
DJ anatembea na laptop yake ya zamani nyimbo zenyewe za kuunga unga hakuna kitu chochote anapata mpaka mnataka kuwakamua huku majambazi yanayochukua dhahabu kwetu mnayasindikiza na gari za ambulance hii sio sawa waacheni hao wadogo wafanye kazi yao maana ajira hamtaki kuwapa..
 
Back
Top Bottom