BASATA: Wimbo wa WAPO wa Ney wa Mitego kufungiwa, hauna Maadili

Hiv hairuhusiw kurusha ngumi kaka teh teh
 
Basata yenyewe haina maadili, Magogoni kwenyewe hakuna maadili, serikali yote inatumia nguvu nyingi kubwa kutetea vyeti
 
Goma tunalo mtaani, yani karibia kila mwenye smartphone anao, haina maana kuufungia, na bado utasambaa zaidi
 
bashite ndio hana maadili na anachochea vurugu
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema wataufungia wimbo wa 'Wapo' wa Nay wa Mitego kwani hauna maadili. Amesema haufai unachochea vurugu.
Tanzania hii ukisema ukweli ww ni mchochezi na hii tafsl imezagaa dunia nzima
 
Kupigwa radio halikuwa Lego la wimbo huu,

Wimbo umeshawafikia wahusika (targeted market). Utaendelea kusikilizwa tuu.

Roma mkatoliki alitumia mbinu hii 2015 akatusua.

Ney anapita mule mule hakuna kitakacho haribika.

Kwa kuendelea kumshikilia Ney nikuupa 'kìki' wimbo huu, majority watautafuta n.a. kuusikiliza.

Hivyo basi kila kinachoendelea kwa sasa ni sawa na kumpiga chura teke.
 
Watuvamie watunyang'anye simu na flash zetu. Hatuna muda na radio siku hizi!
 
Watu walionao huo wimbo wafanyeje? Waurudishe au waendelee kuusikiliza.?
Utaanzishwa ukaguzi.
Ole wako ukutwe unaumiliki/sikiliza au kuburudishia popote na kwa namna yoyote hata ukiu-google umeulawanya.
Tegemea tamko kama hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…