BASATA: Wimbo wa WAPO wa Ney wa Mitego kufungiwa, hauna Maadili

BASATA: Wimbo wa WAPO wa Ney wa Mitego kufungiwa, hauna Maadili

KESI YA UCHOCHEZI YA NEY WA MITEGO NA WIMBO WAKE MPYA WAPO

NA
,Mdude nyagali

WAKILI; unasema wewe ni afisa wa polisi ney wa mitego alifanya uchochezi kwenye nyimbo yake na baadhi ya maneno yaliyopo kwenye hati ya mashtaka yameandikwa kichaa kapewa rungu hebu iambie mahakama kichaa aliyemsema ney ni yupi?

SHAHIDI PC;;kichaa aliyemsema ney ni mtukufu

WAKILI;;ifafanulie vizuri mahakama wewe ulijuaje kama kichaa aliyeimbwa na ney ni mtukufu?

SHAHIDI PC.;mimi nilihisi kuwa atakuwa mtukufu kwa kuwa ney ni timu ukawa;

WAKILI;;shahidi hivi unafahamu kuwa ushahidi wa kuhisi na kupiga ramli mahakamani haupo kwa kuwa sio kwa mganga wa kienyeji na haupo kwenye sheria yoyote?

SHAHIDI PC;;ndiyo

WAKILI;;Sasa ebu iambie mahakama bila kuhisi huyu kichaa kapewa rungu aliyemuimba ney ulijuaje ni mtukufu?

SHAHIDI PC;;kimya

WAKILI;kuna maneno mengine unayakumbuka ambayo ni ya kichochezi na yapo kwenye wimbo wa ney?

SHAHIDI PC;ndiyo
WAKILI;;unaweza kuyataja?
SHAHIDI PC;;1,kuna watu hawana malinda,,2.daudi bashite kavoji vyeti,,,3.hutaki ushauri unajifanya ndugu yake yesu

WAKILI;kwa hiyo watu kutokuwa na malinda ni uchochezi?
SHAHIDI PC;ndiyo
WAKILI;ebu iambie mahakama nini maana ya kutokuwa na malinda?

SHAHIDI PC;;kimya

WAKILI ;;jibu mheshimiwa HAKIMU anasubili a note jibu lako

SHAHIDI;;sijui ila nilisikia bungeni mbunge wa mbeya mjini mheshimiwa mbilinyi akiongea kuwa gavana akaguliwe malinda.

WAKILI ;je wewe una hiyo malinda?
SHAHIDI PC;sina na siijui

WAKILI;;Kwa upelezi wako kama afisa wa polisi ulijua ney wa mitego anamsema nani ambaye hana malinda?

SHAHIDI PC;katika kufanya upelelezi tukishilikiana na ofisi ya OCCID na ofisi ya RCO tuligundua ney alikuwa anamsema gavana wa mkoa wetu kuwa ndiye hana malinda

WAKILI;wewe ulijuaje kama ney anamsema gavana huenda alikuwa anakusema wewe na wewe si umesema hapa na mahakama ime note kuwa huna malinda?

SHAHIDI PC;hapana sio mimi ni gavana

WAKILI;;;Kwani kuna mstari wowote wa huo wimbo gavana ametajwa?

SHAHIDI PC;;hapana ila ametajwa kwa jina la daudi bashite;

WAKILI;;;kwani gavana alishawahi kusibitisha popote au kanisani ama kiapo cha mahakama kuwa jina la daudi bashite ni lake?

SHAHIDI PC;;sijui ila naona kwenye mitandao watu wanamuita hivyo.

WAKILI;;huko kwenye mitandao ni akina nani wanamuita hivyo?

SHAHIDI PC;akina Mdude Chadema Nyagali, Malisa GJ, Daniel Ezekiel Daniel Kumbusho Dawson Kagine Michael Mwaikenda Boniface Mwabukusi Yericko Nyerere Bob Chacha Wangwe Boniface Jacob Julius S. Mtatiro mange kimambi Tanzagiza Hilda Newton Chadema Karama Kaila na wengine wengi

WAKILI;;je unaweza kumleta gavana ili aje aisibitishie mahakama kuwa yeye ndiye bashite halafu ndio tuendelee na tafsiri ya neno malinda?

SHAHIDI PC.;itakuwa ngumu mheshimiwa kumleta gavana.

WAKILI;;unafahabu kwa mujibu wa sheria usipo mleta gavana kuthibitisha kuwa yeye ndiye daudi bashite ushahidi wako kuhusiana na malinda unakosa uhalali mbele ya mahakama tukufu?

SHAHIDI PC;kimyaaa

WAKILI;unafahamu kuwa kwa mujibu wa katiba serikali yetu haina dini ila wananchi wake ndio wana dini?

SHAHIDI PC;;ndiyo

WAKILI;;unakubaliana na mimi kuwa kwa mwongozo huo wa katiba ili uwe na undugu na yesu ni lazima uwe myahudi au muisrael?

SHAHIDI;;Ndiyo

WAKILI ;;sasa haya maneno unayosema ni ya uchochezi kwenye wimbo wake kuwa hashauliki ana undugu na yesu ulijua ney anamsema ni nani?

SHAHIDI;;ney alikuwa anamsema ni mtukufu kwa kuwa wapinzani hulalamika kuwa mtukufu hashauriki.

WAKILI;;kwani mtukufu ni muyahudi?au ana vitambulisho vyovyote vinavyoonyesha ni muisrael ama viashilia vinavyoonyesha ana undugu na yesu?

SHAHIDI;;kimyaaa

NINGEKUWA WAKILI MIMI MDUDE HAKIKA KESI YA NEY NINGEJITOLEA KUISIMAMIA BURE.

Mdude nyagali
sumu ya nyigu
Hiv hairuhusiw kurusha ngumi kaka teh teh
 
Basata yenyewe haina maadili, Magogoni kwenyewe hakuna maadili, serikali yote inatumia nguvu nyingi kubwa kutetea vyeti
 
Goma tunalo mtaani, yani karibia kila mwenye smartphone anao, haina maana kuufungia, na bado utasambaa zaidi
 
Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema wataufungia wimbo wa 'Wapo' wa Nay wa Mitego kwani hauna maadili. Amesema haufai unachochea vurugu.

3fc24f5cd49e3585bccaf7c39e2b661c.jpg

Tanzania hii ukisema ukweli ww ni mchochezi na hii tafsl imezagaa dunia nzima
 
Kupigwa radio halikuwa Lego la wimbo huu,

Wimbo umeshawafikia wahusika (targeted market). Utaendelea kusikilizwa tuu.

Roma mkatoliki alitumia mbinu hii 2015 akatusua.

Ney anapita mule mule hakuna kitakacho haribika.

Kwa kuendelea kumshikilia Ney nikuupa 'kìki' wimbo huu, majority watautafuta n.a. kuusikiliza.

Hivyo basi kila kinachoendelea kwa sasa ni sawa na kumpiga chura teke.
 
Watuvamie watunyang'anye simu na flash zetu. Hatuna muda na radio siku hizi!
 
Watu walionao huo wimbo wafanyeje? Waurudishe au waendelee kuusikiliza.?
Utaanzishwa ukaguzi.
Ole wako ukutwe unaumiliki/sikiliza au kuburudishia popote na kwa namna yoyote hata ukiu-google umeulawanya.
Tegemea tamko kama hili.
 
Back
Top Bottom