BASATA yamfungia Harmonize kufanya Muziki, Nandy atozwa Faini

BASATA yamfungia Harmonize kufanya Muziki, Nandy atozwa Faini

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemfungia msanii Rajab Abdulkahali (Harmonize) kujishughulisha na kazi za sanaa kwa namna yoyote ile hadi atakapotekeleza maagizo aliyopewa, ikiwemo kulipa faini ya shilingi milioni tano (Tsh 5,000,000/=) na kushusha video ya wimbo wake wa "Kudos" kwenye mitandao ya kijamii.

Hatua hii imechukuliwa baada ya msanii huyo kubainika kusambaza video ya wimbo huo inayokiuka maadili ya Mtanzania na kuvunja heshima ya msikilizaji au mtazamaji, bila kutoa utetezi au maelezo mbadala kwa baraza hilo.

Kwa upande wa msanii Faustina Charles Mfinanga (Nandy), BASATA limemtoza faini ya shilingi milioni tatu (Tsh 3,000,000/=) kwa kosa la kuvaa nguo isiyokuwa na staha na inayovunja heshima ya mtazamaji wakati akitumbuiza kwenye fainali za Miss Universe Tanzania 2026.

Nandy amekiri kosa hilo, ameshusha video hiyo isiyozingatia maadili kwenye mitandao yake ya kijamii, amelipa faini hiyo, na sasa ameruhusiwa kuendelea na shughuli zake za sanaa chini ya uangalizi.

Msishangilie hii issue.
Kufungia na Ku-GRADE ipi ni sahihi?

Nashauri Harmonize ahamishe shughuli zake kutoka hapa bonĝo
 
Back
Top Bottom