PureView zeiss
JF-Expert Member
- Sep 5, 2016
- 10,786
- 35,916
Waziri wa Ujenzi wa Tanzania Innocent Bashungwa ametoa ushauri wa Mamlaka husika kuruhusu barabara zinazotumiwa na Mabasi ya ‘Mwendokasi’ ziwe zinatumika na magari binafsi hususani wakati wa asubuhi kwenye kuwahi kazini na jioni wakati wa kurudi nyumbani na kusema hiyo itapunguza foleni hasa ukizingatia wakati huu ambao mabasi ya mwendokasi yapo machache.
Akiongea Jijini Dar es salaam leo October 22,2024 wakati wa hafla ya utiaji saini ujenzi wa daraja la Jangwani, Bashungwa amesema wazo hilo linaweza kufanyiwa kazi wakati huu ambao mabasi yako machache lakini pale Mabasi mapya yatakapoanza kazi utaratibu wa zamani utaendelea.
“Wakati foleni ikiwa kali ama ni asubuhi Watu wanaenda kazini au jioni Watu wanatoka kazini kwenda nyumbani naona zile njia za BRT tukishirikiana na Jeshi la Polisi naona haja ya kuweka utaratibu ambao utapunguza foleni, mabasi yatakapokuja tunasitisha lile zoezi lakini haileti maana unakutana Wananchi wapo kwenye foleni halafu katikati (barabara za mwendokasi) unakuta peupe kuanzia point A hadi point B”
“Kwanini tusikae na Jeshi la Polisi, TAMISEMI tukakubaliana lini mabasi mapya yatakuja na kabla mabasi hayajaja basi uratibu wa Matrafiki ku-controll magari, hata hizi barabara zitumike, mabasi yakija tutarudi kwenye utaratibu wa kawaida ili kwa sasa tupunguze foleni, kwahiyo Mh. RC ili naomba nikuachie uratibu” ——— Waziri Bashungwa...
Hili wazo hata Mimi naliunga mkono na liwe endelevu tu
=======
UPDATES:
Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amefunguka na kueleza kuwa pawepo na matumizi ya Barabara za magari ya Mwendokasi ambazo hazijaanza kutumika ili ziweze kupunguza foleni.
Bashungwa ameyasema hayo alipokuwa katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa Daraja la Jangwani leo Oktoba 22, 2024 Jijini Dar es salaam.