Basi la Abood lagongana na IST wakati dereva 'aki-overtake', Watu wanne wafariki Dunia

U first gentleman na wenyewe kuupata kafara inahusika?
 
Jeshi la polisi wawe wakali
Wasababishaji wa ajali inabidi wahukumiwe kifo tu, Madereva wazembe wanaua watu wasio na hatia. Kama hapo inaonekana wote waliofariki ni abiria na dereva wa IST, ambao hawana hatia ni huyo dereva wa basi mwenye kosa la kuovertake pasipo na sababu. Halafu watasema tumuachie mungu ajali ya haina kinga.
 
Nchi zingine hutoa adhabu kali ya kifungo kirefu na pia leseni ya udereva kufutwa kwa ajali ya kizembe ya namna hii

Kwa Tanzania adhabu kwa madereva wazembe ni ndogo sana.
Hiyo pia inaweza kumfanya Dereva kutojali usalama na uhai wa watu/watumiaji wengine.
 
Hawa jamaa wa mabasi trafiki wanawachekea ... Yani wao hawajali wana overtake tu hasa kama ni gari dogo anakupelekea tu wewe ndiye utafute pa kwenda kama utaingia kwenye mtaro hiyo ni juu yako. Yani hawa wataua wengi
 
Usiombe ukakutana na haya mabasi ya mkoani hapo barabarani. Yaani akiwa nyuma yako ni mateso na akiwa mbele yako ni mateso. Wanasumbua sana barabarani na wana overtake kwa uzembe mkubwa sana
 
Hawa madereva wa mabasi na zile Faw za michanga huwa hawaheshimu kabisa watumiaji wengine wa barabara.huwa yaani wanajiona kama ni untaoucheable.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…