Basi la Sauli lapata ajali Picha ya Ndege, Kibaha. Wanne wajeruhiwa, 40 wanusurika

Kuna siku nilipishana nazo mida ya saa 5 asubuhi kuelekea saa sita kule Kilolo zikiwa zimepita Daraja la Ruaha, DPK alikuwa anaongoza anafukuzwa na Sauli 2 kama mbwa koko
Wanapumuliana matakoni kwa distance ndogo sana kiasi kwamba wa mbele akikanyaga breki ya ghafla tu zote tatu zinaumana
 
Na hilo basi juzi hapa simba chawene alilikamata kwa kosa la speed barabarani kumbe hakuwaonea kama walivyokuwa wanalalamika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pamoja na kwamba hii ni ajali, inaonekana aliyekuwa akichukua video ni mtu jasiri sana...

Pole kwa majeruhi
 
Hakuna mtu wa kutupa ripoti zaidi
Hakuna aliyekuwa, watu 4 wamepata michubuko tuu. Jamaa alikuwa ana overtake gari zaidi ya tatu, ghafla akakutana uso kwa uso na gari ingine kubwa mbele, akaamua kuchochora porini hukooo, ndiyo salama yake na abiria. Dereva kafungiwa leseni miezi sita hivyo natumai zile fedha za betting ya kuwahi kuingia stend Mbeya amezitunza ili sasa zimsaidie kwa kipindi hiki cha miezi sita atakachokuwa kijiweni.
 
Ila dpk anatutoa jasho mdau tukubali tu...
Golden Deer New Force, amepata SANA ajali, mpaka ku stabilize na kupata madereva makini.

Hii ajali pia dereva, asingekuwa ngangari, angeua wengi. Tushukuru Mungu, ila space ya viti ndani ya SAULI daah sihami.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Huyo dereva ni bonge la boya.....
 
Ipo video inayoonesha ajali ilivyotokea, dereva wa basi ana makosa sana..
Nimeiona video, tena aliyerekodi ni mtu aliyekuwa kwenye hilo Lori. Alijuaje ilihali Sauli imetokea ghafla hadi akaanza kurekodi bado mapema maana Dereva wa Lori kapishana na magari mengi akiwa anarekodi kabla hajakwaruzana na Sauli.

Pia Dereva wa Lori alikuwa anaonesha jambo kwa mkono jambo ambalo aligundua kitu lakini hakuchukua maamuzi ya kutoa ishara ya hatari na kusimama kama ingewezekana badala yake aliendelea ilihali kashagundua hatari.

Dereva wa Lori angepunguza mwendo, Sauli angejirusha huko mtaroni bila kukwaruzana na Lori.

Anyway, Dereva wa Sauli alifanya kosa, pia dereva wa Lori naye kafanya makosa baada ya kugundua hatar iliyo mbele yake kwani aliishia kurekodi na kuendelea mbele
 
Watu wanamlaumu tu dereva wa sauli ile foleni kuanzia ubungo mpaka kibaha ukifanya masihara masaa matatu yatakukuta hapohapo halafu una safari ndefu ya kwenda tunduma......wengi tu wanaovateki ila leo balaa limemkuta yeye
 
Kuna Kampuni Moja Dar Es Salaam ~Mbeya Ulikuwa Inaitwa Ndenjela Kama Sijakosea Jina Madereva Wake Walikuwa Wakina Dada Siioni Kabisa!!


Hii Sauli Oops!! Njiani Kama Karatasi Vile
Ndenjela Jet kwangu ndio basi Bora ilikuwa nikipanda Full burudani. Mzee Mwanji sijui Nini kilimpata chombo za fundi hazikudumu barabarani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…